MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,144
Ninayaheshimu majeshi yote ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania yakiwemo Police, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na TISS, lakini kusema kweli walichokifanya JWTZ pale Ukonga kimenifanya niende mbali sana.
Baada ya Rais Magufuli kuona ule ujenzi una suasua akaingilia kati kwa kutoa wito kwa JWTZ kuchukua tenda ile na wajenge nyumba zile za gorofa ili mradi ukamilike na askari magereza wawezee kuishi pale na familia zao.
Magereza walichukua muda mwingi sana huku kazi ikilala, sijui kama walikosa rasilimali fedha ama vipi.
Kufumba na kufumbua leo nimepita Ukonga kweli nimeshangaa sana baada ya kuona majengo marefu meupe yakiwa yameota kama uyoga.
Hapo ndipo nikajiuliza kwanini Magereza walishindwa kumalizia mradi pamoja na kupewa muda mrefu, halafu JWTZ with no time vitu vimesimama tena kwa muda mfupi