Mipangomingi
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 2,713
- 2,058
Mkuu Mipangomingi.
Nikushukuru kwa dhati kabisa kwa ushauri wako.
Mkuu. Challenge ambayo ipo ya Muungano leo ni matokeo ya watu kama wewe waliokuwa na mipangomingi na usiri mkubwa katika kufanikisha mipango hiyo.
Mkuu hakuna katika dunia hii muungano unaolingana na huu wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini hakuna muungano unaozifuta nchi waanzilishi wa Muungano huo.
Kwa hiyo lilikuwa ni kosa kubwa kujaribu kuifuta Tanganyika..unaijua "Tanzania bara"? lakini ni kosa pia kujaribu kuifuta Zanzibar au kuimeza Zanzibar. Katika sehemu moja pia nimewahi kuonesha kuwa Tanganyika ipo na Taasisi zake nyengine zinaonekana wazi. Sio wizara zote kuwa ni za Muungano. mfumo wa mahakama wa Tanzania bara. sasa mkuu ujuha unakujaje hapa?
Mimi sijazungumzia kuongezeka kwa mambo ya Muungano kuwa ni batili au ubabe au vyenginevyo. ninachosema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa wa mambo kumi na moja. Sasa mkuu, mambo kumi na moja vipi yanaunda nchi moja?
kwa hiyo ni wazi zilikuwepo mamlaka tatu za kisheria. Mamlaka ya Tanganyika, Mamlaka ya Zanzibar na mamlaka ya Muungano.
Kama kuna ujuha katika hili basi ni "ujuha" wetu sote. Kwa sababu hatuujui Muungano wetu, asili yake wala hadhi yake. Sishangai kwa hili kwani wakati wa Utawala wa Mwalimu kuudadisi muungano ilikuwa ni uhaini.
Asante sana kwa ushauri huu "Acha ujuha wee nonda". Nitajitahidi kuutekeleza ushauri wako.
Sorry ikiwa nimekukwaza kidogo, lakini we huwa unapenda kurudiarudia point ambazo useless, niliwahi kuona katika post zako huko nyuma kabla sijawa member hapa jf namna ulivyobishana juu ya eneo la zanzibar, kwa kweli hoja zako hazikuwa na mashiko. Katika hili nimetumia neno ujuha kwa maana, ukisoma yale mambo kumi na moja ya muungano, yaliingizwa kama kumi na moja lakini in practice siyo kumi namoja ni yooooote yahusuyo nchi kama sovereign state, so mistake ilifanyika pale kwa ku-rely katika figure ya kumi na moja wakati applicability yake yanaifuta zanzibar kama nchi bali wilaya/mkoa/kata etc. Ukifikiria saana utaona hakuna mambo ambayo si ya muungano(kwani mambo ambayo si yamuungano ni subset ya mambo ya muungano) means hakuna mambo yasiyo ya muungano kama unavyoona ww. Dawa ya haya mambo ni nyie wazenj msimame na kusema muungano no, wala siyo kutoa rais wala kuvusha magari bila kulipiwa wala nni! Think deeply.