Sasa ni Zamu ya Wazanzibar...

Kichumi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
588
515
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.
 
Hapa patamu,pigania alaf wakiwanyima zbar msiwape kura,na wakiwapa zbar mtoe rais,cdm hatutapiga kampeni,tutasubiri kuhesabu kura maana najua wazbar ni washika dini hawataiba kura. Utasikia yakhee nakubali yaishe,yakhe! Hapo cdm itaibua ushindi kiulaini! Mkuu ebu lete chochoko,tuwachokoze ccm ili tuipasue kiulaini!
 
Tunajua hujuma ambayo wabara wanatufanyia sisi watu wa Zanzibar hasa kwa kuhakikisha kila mara makamu wa rais wa muungano anatoka Pemba na pia tunajua jinsi mlivyomnyima rais wetu wa znz asime makamu wa pili wa rais wa muungano ila ukweli unabaki pale pale 2015 ni zamu ya znz najua manasara hawapendi hilo
 
nilijaribu kuipitia katiba yetu na siajaona kifungu kisemacho urais ni wa kupokezana bara na zanzibar.tafadhalini ndugu zangu msitake leta chokochoko.zilizopo zatosha
 
Mambo ya zamu yanatoka wapi kwenye demokrasia ya vyama vingi. Tena Zanzibar imefanya vizuri kutangaza wazi kuwa ni nchi na dola yenye mipaka inayojulikana na kutambuliwa. Swala kubwa ni kupunguza mambo ya Mwungano kuwa kama yalivyokubaliwa mwanzoni bila nyongeza. Hapo swala la zamu halitakuwepo. Sijui kama kuna mwana CDM katika kamati kuu yao toka ZNZ ambaye ataweza kusimama kama mgombea. CCM labda, hivyo maombi haya yaelekezwe huko. Halaf mchakachue matokeo.
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.

Tena mara 2 mfululizo kama yaani mpaka miaka 20 imalize kama vile wao walivyofanya
 
Mtumbwi ni chombo muhimu zenji ila ni gogo la kuachwa shambani litafunwe na mchwa hapa tabora (bara)...............so unachotaka kwetu ni gogo we dont care
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.

Urais siyo mbio za kupokezana vijiti. Rais ni mtu anaye qualify. Kama ni Zanzibar, Dodoma, Arusha, Mbeya......
 
Baada ya wananchi wa upande wa bara kutoa rais wa Jamhuri ya Nuungano mara 2 mfululizo ni vema sasa wanzetu wa Bara mkatuachia ndugu zenu wa Visiwani urais hapo mwaka 2015. Hii itasaidia kuenzi muungano wetu ulionzishwa na wale viongozi wetu mahiri mzee Karume na Mwalimu Nyerere.
huo ujinga wa kupeana madaraka kama mbio za vijiti ulishaisha zamani-sasa ni muda wetu watanganyika kufanya mambo yao wenyewe-hata hawa viuongozi wa zanzibar huku tanganyika ni wa kuondoa kabisa-
 
Tunajua hujuma ambayo wabara wanatufanyia sisi watu wa Zanzibar hasa kwa kuhakikisha kila mara makamu wa rais wa muungano anatoka Pemba na pia tunajua jinsi mlivyomnyima rais wetu wa znz asime makamu wa pili wa rais wa muungano ila ukweli unabaki pale pale 2015 ni zamu ya znz najua manasara hawapendi hilo

ZNZ mna mchango gani kwa maendeleo ya bara!!!????
Mgombea akitoka ZNZ=kura kwa CDM
 
Urais siyo mbio za kupekezana vijiti. Rais ni mtu anaye qualify. Kama ni Zanzibar, Dodoma, Arusha, Mbeya......
zanzibar haifai waje watutawale huku tanganyika-ni sawa na wewe uende kenya then utake kuwa rais wao-kuna kiongozi gani wa zanzibar ambe ni mtu wa tanganyika?
 
Kwanza nyie si mmesema hamtaki Muungano?

Ni kweli hatuutaki lakini kwa sababu nyie mnaung'ang'ania basi na sisi ni haki yetu kutoa rais tena mara mbili mfululizo kama nyi yaani 2015 na 2025
 
huu muungano sisi pia hatuutaki-ngoja katba ibadilike ndo mtajua tunamaanisha nini
 
Ni kweli hatuutaki lakini kwa sababu nyie mnaung'ang'ania basi na sisi ni haki yetu kutoa rais tena mara mbili mfululizo kama nyi yaani 2015 na 2025
hamna mtu mwenye quality za urais kwa sasa.Salim Ahmed alifaa sana ila kwa chuki na fitina za wazenji mkamkataa sasa sikilizieni sana tu
 
Back
Top Bottom