Mkuu.
Ningefurahi sana kama tutaacha ushabiki na kejeli katika kujadili hoja ambazo zinagusa mishipa ya fahamu ya taifa kama hii.
Mkuu, miungano mengine duniani..taja EAC, EU, SADC,..au nchi UK, nitajie Muungano wowote duniani ulioumikarika kwa kuua au kufuta waanzilishi wake au kuishusha hadhi nchi mbia wa Muungano.
Sisi tunafanya utani lakini utani huu unatupeleka pabaya.
Je unaelewa kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa wa mambo kumi na moja tu. EAC inashughulika na mambo ya pamoja mangapi?
Je unaelewa kuwa kuna nchi ndogo zaidi ya Zanzibar duniani?
Tuache utani, tufungue bongo zetu, tufikiri na tutafakari. Baada ya hapo watu wajadili je kuna umuhimu wa Muungano wa Tanzania wakati EAC ndio imo safarini inaziunganisha nchi za Afrika Mashariki?
Ndio sababu ya kupendekeza Mjadala wa Muungano na muundo wake utangulie ule wa Katiba ya Muungano. Kosa kubwa ambalo sote tunaliepuka ni kusema pia uwepo mjadala wa kuifufua katiba ya Tanganyika. Hili ndilo linaleleta kejeli na utani tunapojadili hoja za Katiba ya Muungano na Muungano wenyewe.