Sasa ni wakati wa kukusanya kodi za ndani kikamilifu

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Waziri wa Fedha Dr Mpango tunakutegemea sana katika kumsaidia Rais Magufuli katika kutumiza ahadi zake za uchaguzi hasa elimu bure mpaka Form IV, mikopo kwa elimu ya juu kwa wakati, huduma bora za afya, tzs 50m kwa kila kijiji nk. Haya yote yanahataji fedha. Kwa hiyo fanya yafuatayo haraka:
1. Weka utaratibu wa kutoa mashine efd bure kwa wafanyabiashara wote wanaostahili.
2. Ili kuhakikisha wanazitumia TRA iajiri vijana watakaotawanywa mitaani kuwakumbusha wateja wote wachukue risiti za efd kila wanaponunua bidhaa na kuwapiga faini wafanyabiashara watakaokaidi.
3.TRA kurudisha utaratibu wa kuweka vizuizi barabarani kukagua magari ya mizigo kama bidhaa wanazosafirisha zina risiti za efd.

Natumaini hatua hizi zitaongeza sana mapato ya kodi za ndani na wafanyabiashara watakusanya VAT na watalipa kodi ya mapato inayostahili. Kwa sasa wafanyakazi wanatozwa kodi kubwa kwani hawawezi kuikwepa na unaweza kutetekeleza ahadi ya Rais ya kuwapunguzia.
 
Kukosa maoni kwenye uzi huu kunaonyesha jinsi tusivyotaka kulipa kodi. CCM na upinzani wote kimya. Inanikumbusha siku mbunge wangu alipowaambia madiwani wa chama chake kuwa" KWENYE MASLAHI HAKUNA CHAMA". yaani tule wote na tuache siasa. SHAME ON US!!!!!!!
 
Back
Top Bottom