Sasa ni wakati BOT mjitambue na kuondoa ada za mwezi zibaki za miamala tu

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Nov 30, 2022
607
553
Habarini,

Hivi sasa kumekuwa na wizi wa mabenki kwa kuweka tozo nyingi kwenye akaunti za wateja wa mabenki hivyo kujikuta hela zina katwa tu bila sababu za msingi.

Mteja ameweka hela zake benki na benki wanazikopesha kwa riba sasa nani amlipe mwenzie benki au mteja?

Kwanini mabenki yakate ada kwenye hela ambayo haitolewi huduma ipo tu?

BOT liangalieni hili hasa pale ambapo akaunti haina hela mabenki yanalimbikiza deni tu manake nini mteja akiweka hela wanakata limbikizo lote kufidia ada huu nao ni wizi.
 
BOT imeshindwa kazi yake kusimamia Mabenki, kwa sasa mabenki yanavuna faida kupitia gharama zao
 
Habarini,

Hivi sasa kumekuwa na wizi wa mabenki kwa kuweka tozo nyingi kwenye akaunti za wateja wa mabenki hivyo kujikuta hela zina katwa tu bila sababu za msingi.
Mkuu haukupata muongozo, au kujulishwa kuhusiana na hizo tozo??. Mara nyingi hizi ni kwa ajili ya ku-support kazi bank
Myeja ameweka hela zake benki na benki wanazikooesha kwa riba sasa nani amlipe mwenzie benki au mteja?
Mkuu bank kazi yake sio kuweka hela zako store, ni kizizungusha ili kukuza uchumi pamoja na uwekezaji. Pia pamoja na haya matumizi ya pesa zako zinavyotumiwa na bank risk zote zinachukuliwa na bank. Mfano juzi juzi hapa kuna video ilikua hapa jukwaani inaonesha jamaa amkimbia na 50M za CRDB amewaachia pumba na uchafu, hii inamanisha iyo 50M in hasaya ya CRDB sio ya mteja.

Kama ungependa pesa zako sisitumike na bank unayotumia tafafhali kafungue current account (akaunti ya biashara)
Kwanini mabenki yakate ada kwenye hela ambayo haitolewi huduma ipo tu ?
Mkuu mfano unatumia DSTV umelipia kifurushi cha mwezi, ikiwa haujaangalia TV kwa siku 10 haimaanishi hii izo siku hazita kuwa deducted kenye package yako.

Ni adda gani imeongezewa kwenye account yako???, umejaribu kumtafuta mtoa huduma wako??
Bot liangalieni hili hasa pale ambapo akaunti haina hela mabenki yanalimbikiza deni tu manake nini mteja akiweka hela wanakata limbikizo lote kufidia ada huu nao ni wizi.
Mkuu hata usipo tumia account yako kwa mpesa au tigo pesa kwe miezi 6 inafungiwa na pia utakutana na garama unazotakiwa kulipa ili kuendelea kupata huduma hizo
BOT imeshindwa kazi yake kusimamia Mabenki, kwa sasa mabenki yanavuna faida kupitia gharama zao
Mkuu sijaelewa, BOT imeshidwaje kusimamia mabank??, Ungependa BOT izuie au kuongeza kodi kwenye faida za bank??

Mkuu pamoja na kusimamia bank BOT pia ina wajibu wa kukuza uchumi.

Ukiona bank zinapata faida jua mzunguko wa pesa umeongeza na watu wengi wapo kwenye financial inclusion hii ni habari njema sawa sio kwa mabank pake yake pia kwa shareholders.

Mkuu nakushauri tembelea DSE upate kununua hisa za bank tofauti tofauti, hii itakusaidia kupata faida wakati bank zikipata faida.
 
Back
Top Bottom