sasa ni rasmi: babu wa samunge ni bilionea!!

Uelewe kuwa huyo so-called "Babu" anagawa kikombe cha dawa tu (and not so much "kutibu" kama Daktari afanyavyo Hospitalini.) Kama ni kugawa "dawa", sioni kwa nini ashindwe kuwapatia "kikombe" Wagonjwa 23 au hata zaidi kwa dakika (maana ni wazi hawezi kugawa dawa kwa masaaa 24.)

Mkuu nimekukubali ila umesahau kuwa hagawi kikombe kwa 24 hrs bali masaa takriban 10 tu.

hivi na wewe unaweza kujiita great thinker kweli?

mbona dada wa watu kanukuu habari ya gazetini na kaweka link pale ya kubonyeza, unawezaje kusema kuwa kuwa kaokoteza data? unataka kutuambia kuwa gazeti la tz daima nalo linasoma hadi magomeni tu?

wewe sasa nimegundua kama sio demu lenye ID na avatar ya kidume, basi una matatizo binafsi na huyu binti kigori! no wonder umeamua kujiita nyau jimi! very funy

Sawasawa Mkuu,Nadhani kuna tatizo binafsi kati ya Miss na Huyu Paka,There has to be somethings that we dont understand!!
Lakini zaidi,UTETEZI wake wa Tiba ya Babu ni MKUBWA mpaka unanishangaza,nahisi kuwa na fikra mbilimbili kuhusu Uhusiano wake yeye Paka Jimmy na Huduma ya Babu!!
Being sour,Cynical,constantly nagging and criticising other contributors doesnt necessarily establish that one is a great thinker!!!
Wakati Mwingine Unapiga Kimya tu,Ndiyo Kiume!!

babu wa samunge ameleta miujiza,kwa kusikia na kuona ndugu wanaokwenda huko,ila mpaka leo hata ndugu zangu wanasema wanajisikia vizuri.
ila hamna kati ya wanao jiskia vizuri ameshatoa uhakika wa ki-hostpitali kuwa vipimo vimeonyesha kupona kabisa.

nashindwa kuelewa babu mpaka leo amepata wageni milioni3,lakini ktk wote hawa hamna aliyetoa majibu Rasmi ya hosptiali kuwa ameponyeshwa na babu wa samunge

Sawasawa Mkuu,Nadhani kuna tatizo binafsi kati ya Miss na Huyu Paka,There has to be somethings that we dont understand!!
Lakini zaidi,UTETEZI wake wa Tiba ya Babu ni MKUBWA mpaka unanishangaza,nahisi kuwa na fikra mbilimbili kuhusu Uhusiano wake yeye Paka Jimmy na Huduma ya Babu!!

Being sour,Cynical,constantly nagging and criticising other contributors doesnt necessarily establish that one is a great thinker!!!
Wakati Mwingine Unapiga Kimya tu,Ndiyo Kiume!!

mkuu, nikuweke sawa hapo kwenye bold,

kwa mujibu wa ufahamu wangu binafsi, sina tatizo lolote la binafsi na huyu mheshimiwa. hata siajawahi kuonanan naye hata siku moja na sifahamiani naye kwa namna yoyote zaidi ya namna ninavyowafahamu wengine hapa JF, kama kuna tatizo basi mniwie radhi ila mimi kiukweli kila ninalochangia hapa nafanya kama wengine wanavyochangia tu na huwa simlengi yoyote, ikitokea nataka kumwambia mtu kitu huwa natumia PM tu, nikiweka wazi jua ni kwa wote tupate kujadiliana au kusaidiana kwa kuwa "sharing is caring", basi na si zaidi ya hapo

unavyoshangaa ndivyo hata mimi ninavyoshangaa!

ubarikiwe sana

mkuu, nikuweke sawa hapo kwenye bold,

kwa mujibu wa ufahamu wangu binafsi, sina tatizo lolote la binafsi na huyu mheshimiwa. hata siajawahi kuonanan naye hata siku moja na sifahamiani naye kwa namna yoyote zaidi ya namna ninavyowafahamu wengine hapa JF, kama kuna tatizo basi mniwie radhi ila mimi kiukweli kila ninalochangia hapa nafanya kama wengine wanavyochangia tu na huwa simlengi yoyote, ikitokea nataka kumwambia mtu kitu huwa natumia PM tu, nikiweka wazi jua ni kwa wote tupate kujadiliana au kusaidiana kwa kuwa "sharing is caring", basi na si zaidi ya hapo

unavyoshangaa ndivyo hata mimi ninavyoshangaa!

ubarikiwe sana

pole sana dada yangu, ............... huyu PJ hata mimi namshangaa sana, toka alipoibuka babu mwenye kikombe, amekuwa mtu hatari sana, ukimkosoa babu tu anakumeza................. nimeishaona mwnendo wake kwa kweli ni mtu hatari.................... lakini nakuomba mpendwa cool down, akiropoka wewe potezea tu........... huna utakachopoteza, huyu na babu nahisi wana ka-ubia fulani na kwa vyovyote vile huyu jamaa anaufaika na hii biashara ya babu! haiwezekani akawa hata tayati kukosana na watu eti kwa sababu ameizimikia tiba ya kikombe ....................... hahah................. ingekuwa hivyo angekwishageuzwa na wajanja upande a pili kama kibua cha mombasa!!!.................. hahah............... au tayari???................... hahahahaaaaaaaaaaa................. mi simo, napita tu wakuu................

Hesaabu zenyewe ziko hivi:

Hadi leo amehudumia watu 3,000,000/- x 500 = 1,500,000,000/-!!

Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo

Na Mwandishi wetu

ZAIDI ya wagonjwa milioni 3 wamepata kikombe kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila ‘Babu’ katika kijiji cha Samunge Loliondo wilayani Ngorongoro tangu aanze kutoa huduma hiyo Agosti mwaka jana.

Takwimu zilizotolewa jana na mmoja wa wasaidizi wa Babu, Jackson Dudui, zinaonyesha bado wanategemea idadi kubwa ya wagonjwa kuendelea kumiminika kijijini hapo kufuata kikombe hicho kinachotibu magonjwa sugu na kwamba juzi pekee wagonjwa 17,065 walipata huduma hiyo.

Magonjwa sugu yanayodaiwa kutibiwa na kikombe hicho kinachokwenda na imani zaidi ni kisukari, shinikizo la damu, pumu, saratani na ukimwi.

Alisema jana magari zaidi ya 400 yenye wagonjwa zaidi ya 3000 yalikuwa yakimsubiri Mchungaji Mwasapila atoke kanisani, ili awapatie tiba hiyo mbadala ambapo alieleza raia kutoka Kenya wamekuwa wakimiminika kwa wingi kijijini hapo.

“Foleni ya magari si kubwa sana kwa siku ya leo kwani hivi tunavyozungumza yapo magari zaidi ya 400 yakimsubiri Babu atoke kanisani na kuanza kuwahudumia kuanzia saa 8 mchana na hakika atawamaliza leo hii,” alisema.

Msaidizi huyo alisema kuwa katikati ya wiki iliyopita walipata ugeni wa wachungaji zaidi ya 10 kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati waliokuwa kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano wao mkuu wa mwaka wakiongozwa na Mkuu wa Jimbo aliyetajwa kwa jina moja la Nangole.

Alisema mbali na wachungaji hao kushiriki mkutano huo waliungana na Babu kutoa vikombe kwa wagonjwa waliokuwepo kijijini hapo kupata tiba hiyo.

Habari zaidi zilizopatikana zimeeleza kuwa Babu amepiga marufuku wagonjwa kutoka Kenya wanaosafirishwa kutumia magari yasiyoruhusiwa kama malori na gari ndogo ‘saloon’ wakiwa wamejazana hali aliyosema ni mateso kwa wagonjwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alieleza kuwa utoaji tiba unaendelea vizuri kijiji hapo, na alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa ukusanyaji ushuru wa magari na helikopta alisema hayo ni mambo ya kisiasa zaidi na kumtaka mwandishi wa habari hizi kusubiri maamuzi ya kikao halali kitakachofanyika leo kijijini hapo.

Alisema bado maamuzi hayajafikiwa kujua ni mamlaka ipi itakayokuwa ikikusanya ushuru huo kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngoromngoro na serikali ya kijiji cha Samunge.

“Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuzungumzia suala hilo naomba usiandike chochote kwani kesho kutakuwa na kikao kitakachozungumzia suala hilo na tutawapeni taarifa,” alisema.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mgogoro wa kugombea ushuru wa magari na helikopta kati ya pande hizo na wakati fulani iliripotiwa kuwa serikali ya kijiji iliwafukuza watoza ushuru toka halmashauri.

source: Milioni 3 wanywa kikombe Loliondo
Ukiwa na bilioni 1.5 ni billionaire? Kwanza mzee anachukua sh.100 kwa kichwa. Hivyo kwa idadi hiyo atakuwa kapata million 300.

Back
Top Bottom