Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

Mkuu Chakaza, lets don't assume and insinuates anything!. Mkuu wetu yuko kwao Chato kwa mapumziko, na baada ya mapumziko anaendelea na kazi akiwa Ikulu ya Chato akiendelea kupiga kazi kama kawaida, hayo mengine sii yetu, waachie wenyewe!.
P
Sasa mbona tunaambiwa Rais ni wetu? Kwanini kama ni wetu tusihoji mambo yake tukiyahoji tupewe jibu na Pascal kuwa hayo sio yetu tuwaachie wenyewe? Wenyewe kina nani ambao Rais ni wao?
Hebu tuwe wakweli, tokea aingie madarakani nchi hii imewahi kupita katika mapambano (vita) hatari yeyote kama hii? Kwa nini vita hatari kama hii ambayo yaweza kusambaratisha maisha ya watanzania na uchumi wao HQ ya mapambano ihamie Chato Nyumbani? Kwa sababu katika hali hii anahitaji kuonana na kujadiliana na kiongozi wenzake, wataalamu wa Afya na uchumi kila siku jee lawezekana hilo?
Kujidanganya sio jambo zuri, kama anatatizo la afya na anaogopa maambukizi ajiengue au tuambiwe. Kwa ni maambukizi ya kiingia pale alipo atakimbia na kwenda wapi tena? Madagascar kuliko gunduliwa chanjo asili?
 
Nilitegemea ungeenda kwenye hicho kitengo cha mawasiliano alichoenda yule mama yetu aliyekuwa wizara ya siha
. Pascal Mayalla. Huyu hawezi kupewa nafasi fuatilia vizuri michango yake utaelewa maana anachostahili sifa anapongeza na anachostahili kukosoa anakosoa kwa mafumbo.
Pascal Mayalla. ni muoga tu ila anaandika ukweli tatizo ukweli unawasilishwa katika mafumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ati chlorine haiuwi virusi
Chlorine ndo kemikali inayotumika kusafisha maji dhidi ya virusi na bakteria ili yawe salama kwa matumizi ya binadamu na inatumika sana kwenye mitandao ya maji mijini pamoja na maji yanayotumika Ikulu. Inashangaza kusikia Mkemia mwenye PhD katika fani hiyo anasema kemikali hiyo haiui virusi na kupendekeza dawa za jadi. Hata viongozi wa halimashauri za miji watumiaji wakubwa wa kemikali hiyo hawasemi kitu kuhusu matamshi ya Rais juu ya Chlorine. Watalaam wa Kemia pia wanakaa kimya tu badala ya kulinda taaluma yao.
 
Ukiona MTU mkali mkali sana kwakutumia nafasi yake (majeshi yake) na kujisema kuwa yeye ningangari mara nyingi huwa ni muoga!!
Mtu anaogopa kupanda ndege, anaogopa haendi misibani, majanga anatanguliza wengine nasasa korona anacharu kujifichamo kijjni... Hizi hazifai kuwa sifa za amir jeda mkulu
 
Kabisa maana ingekuwa Corona inapigwa kwa mizinga naona leo anga nzima ya Tanzania ingekuwa imejaa moshi tupu ila ndiyo hivyo tena Covid-19 ni sayansi tu hapo inatakiwa lazima Bwana Mkubwa ajitafakari mara mbili thou it's too late
Paskali subiri mtu wako wa karibu afe halafu serikali ndo imzike huku ukiona idadi ya waliokufa kwa korona ikibaki hio hio 10 ndipo utajua namna vifo vinavyoongezeka bila kutangazwa.
 
Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete:

1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa
kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato. Corona ilipoanza kuchanganya, Rais wetu aliondoka Dar na kubanisha pale Dodoma, makao makuu. tulishuhudia Rais wetu akifanya MEDITATION kwenye majabali.

Naona baadaye akaona hiatoshi, akaamua kwenda mbali zaidi na hii Corona. na sasa tumeshuhudia akitoa Major Speech yake kutoka Chato. pia ni vema kukumbuka kwamba Rais wetu huwa ni mwoga sana wa majanga. amekuwa na kawaida ya kujitenga mbali na majanga, na kumwachia PM wake. hali kwa sasa ndio hiyo hiyo. Kamanda mkuu kaingia mitini. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

2) Hotuba inayochanganya
Katika hotuba aliyotoa, badala ya kutoa mwanga katika mapambano na Corona, imeleta giza. badala ya kutia matumaini, imeleta hofu zaidi. siyo ajabu sekeseke la Amana lilifuatia mara moja. Hotuba yake inaonesha anatumia zaidi uelewa wake na hisia zake, badala ya kutoa msimamo kutokana na sayansi ya kisasa kabisa, utafiti mpana, mjadala makini na wasaidizi wake, ushauri mpana na makini, na tafakari iliyo pevu. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

3) Anaongea na wakuu wa vyombo vya usalama
Rais Magufuli siku zote anapenda sana majeshi. akikwama popote pale anaita majeshi, na ni zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia. akikwama ujenzi, Jeshi. akikwama madaraja, Jeshi. na hata katika lile JANGA ALILOCHUMA MWENYEWE, JANGA LA KOROSHO, aliita jeshi. Katika kipindi hiki alichochanganyikiwa kabisa, aliona badala ya kuita maprofesa wa tiba na wataalamu wa magonjwa, wizara ya afya na wizara zingine, au hata Task force aliyounda mwenyewe kupambana na Corona, aliita wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi.

Na kama alivyoita wanajeshi ili ikiwezekana wabangue korosho kwa buti, kasema wazi kabisa kwamba anataka kutumia jeshi kupambana na korona. na kweli, IGP akatafakari atafanya nini hapa kwa kutumia upolisi wake, akaamua kufanya kile ambacho wengi walishasema siku nyingi. kuzuia raia wa kutoka nje. sasa tunasubiri CDF Mabeyo yeye atafanya nini , atoe amri wanajeshi waitandike buti Corona? Au yule wa Magereza aitie gerezani Corona? Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

4) Visingizio vya ajabu
Labda katika hali inayoonesha kukwama zaidi, Rais ametoa visingizio. Badala ya kufuata njia sahihi za kukabiliana na Corona, aliamua kuziba masikio na kupokea sifa kutoka kwa wale waliomuona kwamba ni shujaa pale mwanzo.

sasa vifo vinaongezeka kwa kasi, analaumu dawa za kupulizia, analaumu kwamba pengine amehujumiwa kwa kuletewa Barakoa zenye virusi vya Corona! Huyu ni mtu asiyetaka kubeba lawama begani na kujisahihisha. kukubali na kukiri alikosea, na kusonga mbele. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
Rubbish
 
Nimesoma comments mbalimbali nilichobaini ya kuwa humu hamna wenye hoja za msingi,wengi wanabwabwaja tu maneno kisa sijui Magufuli yupo Chato.

Mtapiga sana kelele Kwa kutumia hisia zenu lakini hamtampunguzia au kumwongezea chochote kile hizi kelele zitaishia humu humu jamii forum hakuna Impact yoyote. Poleni sana, kuwa kwake Chato kama hajavunja katiba basi sioni shida.

Akiwa huko bado kazi anapiga kama kawaida,shida yenu nn msilete Maisha ya kukariri hapa. Mjiongeze tangu muanze kupiga kelele sio leo,Angekuwa amekuja.

Kelele tu hakuna lolote. Mtaongea Kila lugha mpaka lugha gongana hazita mtoa Chato,au mjikate Kate Kwa viwembe labda atasikia yani inaonekana kama mnamuabudu vile bila kujua. Au lieni basi,punguzeni kelele.
 
Sasa mbona tunaambiwa Rais ni wetu? Kwanini kama ni wetu tusihoji mambo yake tukiyahoji tupewe jibu na Pascal kuwa hayo sio yetu tuwaachie wenyewe? Wenyewe kina nani ambao Rais ni wao?
Hebu tuwe wakweli, tokea aingie madarakani nchi hii imewahi kupita katika mapambano (vita) hatari yeyote kama hii? Kwa nini vita hatari kama hii ambayo yaweza kusambaratisha maisha ya watanzania na uchumi wao HQ ya mapambano ihamie Chato Nyumbani? Kwa sababu katika hali hii anahitaji kuonana na kujadiliana na kiongozi wenzake, wataalamu wa Afya na uchumi kila siku jee lawezekana hilo?
Kujidanganya sio jambo zuri, kama anatatizo la afya na anaogopa maambukizi ajiengue au tuambiwe. Kwa ni maambukizi ya kiingia pale alipo atakimbia na kwenda wapi tena? Madagascar kuliko gunduliwa chanjo asili?
Yes rais Magufuli ni wetu, ila kuna vitu vyake ni public, sisi wote tuna ruhusa kuvijua ikiwemo alipozaliwa, wazazi, kabila, elimu, marital status na family issues, na akiugua ugonjwa public pia tunapaswa kujua.

Kuna vitu ni private, hatupaswi kujua, hivyo ni kuingilia his right to privacy na kuna vitu ni Confidential vinalindwa na the clauses of confidentiality, maadam tumemuona rais yuko Chato ni kwao, yuko kule mapumzikoni, ila kama ilivyo status ya urais ina two sides, upande mmoja ni human side, rais ni human being, ni binaadamu kama binaadam wengine hivyo akiwa mapumzikoni kwao Chato anakuwa ni binaadamu anayehitaji mapumziko na Chato japo ni nyumbani, pia Chato ni sehemu tulivu, hata mimi nimefika na nina ifahamu, kuna hadi traffic lights, barabarani yanatembea magari ya punda, hayana kelele kabisa!, kwa vile ni kwake na ni kutulivu, rais wetu anatakiwa upumzike kwa amani na utulivu mahali tulivu na salama salmini.

Upande wa pili wa rais, ni Taasisi, presidential institution, hii Taasisi sio human ni Taasisi takatifu, haipumziki, haili wala hailali, hivyo akiwa Chato japo ni nyumbani kwa rais, lakini pia ni Ikulu kwa ile Taasisi ya urais, kazi zote za urais ikiwemo kuendesha nchi, zinaendelea kama kawaida na kila kinachofanyika Ikulu ya Magogoni, au ya Chamwino, kinaweza kufanyika Ikulu ya Chato, au kama kwako Ikulu ni wale ndege tausi na wale wanyama, tunaweza kuwaleta Chato, au hata kama kwako Ikulu ni yale majabali ya Chamwino ili umuone Magufuli akilala juu ya mawe, Chato tunaweza kuyapeleka, lakini kama ni rais Magufuli kuchapa kazi akiwa Chato, mbona anachapa kazi kama kawaida?, sasa why lazima Magogoni au Chamwino?.
P
 
Nimesoma comments mbalimbali nilichobaini ya kuwa humu hamna wenye hoja za msingi,wengi wanabwabwaja tu maneno kiss sijui Magufuli yupo Chato.

Mtapiga sana kelele Kwa kutumia hisia zenu lakini hamtampunguzia au kumwonezea chochote mile hizi kelele zitaishia humu humu jamii forum hakuna Impact yoyote. Poleni sana kuwa kwake Chato kama hajavunja katiba basi sioni shida.
Una familia?
Una umri gani?

Yaani huoni kabisa umuhimu wa watu kupiga kelele kupitia mitandao ya kijamii? Kama unafikiri huwa zinaishia humu humu jaribu kutafuta clip ya IGP ya jana au tafuta Hotuba ya trh 22 kutokea Chatto ndio utaelewa umuhimu wa hiki kinachofanyika.
Asante!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wewe siku hizi akili yako inatumika vizuri humo kichwani mwako au imeondolewa kiwekwa kitu kingine ambacho hata wewe hujui ni nini kimewekwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una familia?
Una umri gani?

Yaani huoni kabisa umuhimu wa watu kupiga kelele kupitia mitandao ya kijamii? Kama unafikiri huwa zinaishia humu humu jaribu kutafuta clip ya IGP ya jana au tafuta Hotuba ya trh 22 kutokea Chatto ndio utaelewa umuhimu wa hiki kinachofanyika.
Asante!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna lolote, mipanho yao ndo wanayo tekeleza, acheni kelele eti GPM mnampangia pa kukaa unajua ni sababu gani yupo kule je kalazimishwa? Au ni hiari? au wanamlinda wamempangia?

Maana swala la kumlinda raisi sio t Kwa mabomu ni !Mambo mengi na huyo kazi ueue hausiki ni walinzi.
Na hivyo ndicho kinachonikera hamjui lolote mnabaki kubwabwaja maneno.

Acheni kelele na zimejaa humu jf,cha ajabu mnaongea msichokijua,mnakera sana au kama amevunja katiba basi mtoe evidence uwepo wake Chato
 
Paskali subiri mtu wako wa karibu afe halafu serikali ndo imzike huku ukiona idadi ya waliokufa kwa korona ikibaki hio hio 10 ndipo utajua namna vifo vinavyoongezeka bila kutangazwa.
Mkuu Mafuta Mingi, mimi ni professional wa habari, hivyo natakiwa kutangaza only the official data, so far kwa Tanzania watu waliokufa kwa Corona ni watu 10 tuu!.
Hii haimaanishi watu hawafi kwa magonjwa mengine, hata kama ni kweli wanakufa kwa dalili za Corona, kama hawapo kwenye the official data, then watakuwa wamekufa kwa magonjwa mengine and not Corona!.
P
 
Yes rais Magufuli ni wetu, ila kuna vitu vyake ni public, sisi wote tuna ruhusa kuvijua ikiwemo alipozaliwa, wazazi, kabila, elimu, marital status na family issues, na akiugua ugonjwa public pia tunapaswa kujua.

Kuna vitu ni private, hatupaswi kujua, hivyo ni kuingilia his right to privacy na kuna vitu ni Confidential vinalindwa na the clauses of confidentiality, maadam tumemuona rais yuko Chato ni kwao, yuko kule mapumzikoni, ila kama ilivyo status ya urais ina two sides, upande mmoja ni human side, rais ni human being, ni binaadamu kama binaadam wengine hivyo akiwa mapumzikoni kwao Chato anakuwa ni binaadamu anayehitaji mapumziko na Chato japo ni nyumbani, pia Chato ni sehemu tulivu, hata mimi nimefika na nina ifahamu, kuna hadi traffic lights, barabarani yanatembea magari ya punda, hayana kelele kabisa!, kwa vile ni kwake na ni kutulivu, rais wetu anatakiwa upumzike kwa amani na utulivu mahali tulivu na salama salmini.

Upande wa pili wa rais, ni Taasisi, presidential institution, hii Taasisi sio human ni Taasisi takatifu, haipumziki, haili wala hailali, hivyo akiwa Chato japo ni nyumbani kwa rais, lakini pia ni Ikulu kwa ile Taasisi ya urais, kazi zote za urais ikiwemo kuendesha nchi, zinaendelea kama kawaida na kila kinachofanyika Ikulu ya Magogoni, au ya Chamwino, kinaweza kufanyika Ikulu ya Chato, au kama kwako Ikulu ni wale ndege tausi na wale wanyama, tunaweza kuwaleta Chato, au hata kama kwako Ikulu ni yale majabali ya Chamwino ili umuone Magufuli akilala juu ya mawe, Chato tunaweza kuyapeleka, lakini kama ni rais Magufuli kuchapa kazi akiwa Chato, mbona anachapa kazi kama kawaida?, sasa why lazima Magogoni au Chamwino?.
P
Paskali Njaa bhana.....(Mayalla = Njaa)

Kama inakuja, inakataa, inakuja inakataaa....
Nakuelewa sana tu. Asie kuelewa wacha aendelee kutokwa na mapovu ilhali kumbe wote mnavuta kamba upande mmoja
 
Yes rais Magufuli ni wetu, ila kuna vitu vyake ni public, sisi wote tuna ruhusa kuvijua ikiwemo alipozaliwa, wazazi, kabila, elimu, marital status na family issues, na akiugua ugonjwa public pia tunapaswa kujua.

Kuna vitu ni private, hatupaswi kujua, hivyo ni kuingilia his right to privacy na kuna vitu ni Confidential vinalindwa na the clauses of confidentiality, maadam tumemuona rais yuko Chato ni kwao, yuko kule mapumzikoni, ila kama ilivyo status ya urais ina two sides, upande mmoja ni human side, rais ni human being, ni binaadamu kama binaadam wengine hivyo akiwa mapumzikoni kwao Chato anakuwa ni binaadamu anayehitaji mapumziko na Chato japo ni nyumbani, pia Chato ni sehemu tulivu, hata mimi nimefika na nina ifahamu, kuna hadi traffic lights, barabarani yanatembea magari ya punda, hayana kelele kabisa!, kwa vile ni kwake na ni kutulivu, rais wetu anatakiwa upumzike kwa amani na utulivu mahali tulivu na salama salmini.

Upande wa pili wa rais, ni Taasisi, presidential institution, hii Taasisi sio human ni Taasisi takatifu, haipumziki, haili wala hailali, hivyo akiwa Chato japo ni nyumbani kwa rais, lakini pia ni Ikulu kwa ile Taasisi ya urais, kazi zote za urais ikiwemo kuendesha nchi, zinaendelea kama kawaida na kila kinachofanyika Ikulu ya Magogoni, au ya Chamwino, kinaweza kufanyika Ikulu ya Chato, au kama kwako Ikulu ni wale ndege tausi na wale wanyama, tunaweza kuwaleta Chato, au hata kama kwako Ikulu ni yale majabali ya Chamwino ili umuone Magufuli akilala juu ya mawe, Chato tunaweza kuyapeleka, lakini kama ni rais Magufuli kuchapa kazi akiwa Chato, mbona anachapa kazi kama kawaida?, sasa why lazima Magogoni au Chamwino?.
P
Pascal umejibu vizuri Ila mwisho umechapia! Kwa nini imemchukua muda mrefu kuhamia Dodoma kama Ikulu? Ni wazi Ikulu ni zaidi ya majengo na vitanda vya kulalia. Kuna mengi sana ya kuyaweka sawa hasa miundo mbinu ya ulinzi, usalama,mawasiliano na mazagazaga mengine.
Anaweza kufanya kazi zake Chato au hata Tunduru katika mazingira ya kawaida kabisa lakini sio katika taharuki kama hii wiki NNE haupo ofisini?
US kule Camp David kuna kila kitu, lakini wao kama mkuu yuko kule anapumzika lolote likitokea basi anarudi haraka
 
Nimesoma comments mbalimbali nilichobaini ya kuwa humu hamna wenye hoja za msingi,wengi wanabwabwaja tu maneno kisa sijui Magufuli yupo Chato.

Mtapiga sana kelele Kwa kutumia hisia zenu lakini hamtampunguzia au kumwongezea chochote kile hizi kelele zitaishia humu humu jamii forum hakuna Impact yoyote. Poleni sana, kuwa kwake Chato kama hajavunja katiba basi sioni shida.

Akiwa huko bado kazi anapiga kama kawaida,shida yenu nn msilete Maisha ya kukariri hapa. Mjiongeze tangu muanze kupiga kelele sio leo,Angekuwa amekuja.

Kelele tu hakuna lolote. Mtaongea Kila lugha mpaka lugha gongana hazita mtoa Chato,au mjikate Kate Kwa viwembe labda atasikia yani inaonekana kama mnamuabudu vile bila kujua. Au lieni basi,punguzeni kelele.

Hili povu siyo la bure! Kama siyo Jesca wewe basi utakuwa ni Daudi Albert Bashite bila shaka. All in all, tunamtaka Kamanda mkuu aonekane mstari wa mbele vitani!

Kujificha uvunguni mwa kitanda na wakati vita imepamba moto halafu anasukumizia mzigo makamanda wasaidizi, haileti picha nzuri.
 
Back
Top Bottom