Sasa Nchi inaanza kutengamaa

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
naam wanabodi!

kuna kila dalili Nchi inaanza kuelekea kule tukutakako! watumishi wa umma wameanza kuhisi uwepo wa serikali bila kujali wapo umbali gani kutoka makao makuu ya serikali.kuanzia Mtwara hadi Kagera,Songea mpaka Manyara, Kigoma hadi Tunduma, mkono wa serikali unafika.Muda siyo mrefu utawala bora utatamalaki!

jana nilikuwa naongea na kiongozi mmoja mwandamizi akaniambia hospitali nyingi sasa zimeanza kukusanya mapato mara tano zaidi ya walizo kuwa wanakusanya kabla ya serikali ya Magufuli kuingia madarakani! Kila mtu anaogopa kuzifanyia ujanja.Ofisi za Ardhi sehemu nyingi wameanza kufanyakazi kwa kuzingatia taratibu.

Muda siyo mrefu serikali itakuwa inakusanya shiling Trilioni mbili kwa mwezi! Yes,hii itamaanisha kwamba kwa mwaka serikali itakusanya zaidi ya shs trilioni 24.bajeti ya serikali ni trilion 22.Maana yake ni kwamba Nchi itajitegemea asilimia mia na kuweka akiba Trilioni mbili.Muda siyo mrefu Wazungu watakuja kukopa fedha ketu!!
 
Mawazo yako mazuri sana.

Tunachosubiri sasa ni pale Magu atakapoanza kuipanga bajeti yake mwenyewe na kuweka vipaumbele vyake.
Lakini kikubwa ni jinsi atakavyoanza kupanga vyanzo vya mapato kwa hili taifa.

Utalii tu peke yake akijipanga vyema anaweza kuingiza zaidi ta Trillioni 6 kwa mwaka ambazo kwa wastani ni ongezeko la Billioni 500 kwa mwezi kwenye makusanyo yake.
Bado Bandari.
 
Ndio Mabadiliko tuliyo yataka
Sio mabadiliko ya kuzungusha mikono ya Wanywa Viroba
Hapo umekosea! watu walichoka utawala holela na ndio maana walitaka mabadiliko kwa hamu na ghamu! Magufuli kaja kwa mpango wa Mungu na kwamba yeye mwenyewe ana hamu ya kuifanyia Nchi jambo Special.na muda siyo mrefu atafanikiwa kutuunganisha watanzania kuwa kitu kimoja.
 
Tuwe na subra walau tathmini tuifanye mwaka mmoja toka tarehe ya uchaguzi tusije tukala matapishi yetu wenyewe
 
Back
Top Bottom