Sasa najiunga na ACT Tanzania

chama kimoja kimeanzishwa kwa ajili ya kugawanya upinzani na hiyo ni ajenda yake kuu ili kufanikisha kuendelea na majoka wa makengeza na wao wakiwa wanufaika. Hiyo vita ni dhahiri
 
Kiongozi nenda mapema kaungane na zito. Ila ukifika huko uliza kama walioko ni malaika. Msalimie Zito ukifika mwambie akumbuke nyayo za mkigoma mwenzake KABURUO.
 
Chadema ni chama makini ever, hatuishi na wanafiki na wafuata mkumbo. Better we get rid off of fuc.... members
 
Kan'tangaze, Nimieipenda hiyo:
After Cheating, They go there!!!!
Haa haa haa Ukweli usiofichika. na

'There' they will taste it. Watasaga meno.
 
yaani mfa maji kweli akosi kutapatapa!!! HEHE sasa nataka kujua Mgombea Uraisi ACT ni nani au bdo Hamjaanza mchakato..Anyway time will tell the true colour of ACT once mkianza kupinduana kwenye katiba yenu katika kufanikisha maazimio na malengo yenu.hii ni kwasababu watukutu wote wapo ACT,notorious politicians wapo ACT-Tanzania,Unpatience politicians wapo ACT-Tanzania,Arrogant politicians wapo ACT-Tanzania....Time will tell to ssee their true colour
 
Michadema zitto atawatoa kamasi mwaka huu kila mtu nikiangalia anahasira na chadema kwa unafiki,uzandiki na ukabila wao.
 
Naona bado mnaishi kwenye fikra za CDM kwani ukamanda ndio asili yake nashauri mtafute jina lingine la hamasa waachieni CDM na jina lao
 
Walioshindwa sikuzote Yao matusi tu ACT karibun sana tunahitaji ukombozi wenu
 
Usikonde kiongozi, tayari huku Moshi nimeandaa wanachama wapya elfu kumi na nane, namsubiri zito aniletee kadi.
 
Vua gamba na gwanda vaa uzalendo act oyeeee tuko pamoja

ACT ni ujinga na kujitoa uewela. Eti uzalendo, nani mzalendo, uzalendo hauji kwa kuuandika kwenye katiba au kuutamka bali matendo. ZZK ni kama Augustn Mrema na hoja zake za kukamata dhahabu airport eti huo ni uzalendo, uzalendo ni dhana pana sana.
 
Unafuata nini huko ACT? Zile za escrow au zile za ccm walizokuwa wanamtumia yule mama wa kijerumani?????????
Au hizi alizohongwa na bunge za kiinua mgongo ambazo hakuzistahili? Nakuuliza mtoa hoja hivi ukifukuzwa kazi unalipwa kiinua mgongo au unapewa nauli ya kukurudisha utokako? Makinda zitendee haki pesa za watanzania na acheni kupindisha sheria za ajira.
 

Demokrasia ya ukweli utaisikia tu kwa nchi za wenzetu. Ni ndoto kwa nchi za dunia ya tatu kupractice pure democracy! Binafsi naona wote ni wasaka tonge. Ndo maana wanasiasa wapo kwa ajili yao na familia zao! Huna lolote zaidi ya njaa kali.
 

Ni sawa na ngoma ivumayo sana...! Tangu lini ngozi ya kitimoto ikawamba ngoma? Shy land wee ni mshkaji wangu sana tu hapa JF lakini kwa hili nina maoni tofauti
Kwanza ni dhambi kabisa tena ni kejeli kubwa kwa Zito kujilinganisha na Nyerere R.I.P, Mwalimu hakujijenga binafsi na alipigania ukombozi wa kweli wa taifa hili, mwalimu hakuwa na tamaa ya Mali na alikuwa na maono
Zito ni mbinafsi, hii ni hulka yake hashauriki na haambiliki, yeye anajiona ni bora zaidi na popote alipo na chochote anachofanya hupenda kuwa juu/ kujikweza
Zito si mnyenyeku na akifanya hivyo hufanya kwa manufaa binafsi
Zito si mtu wa kutaka changamoto, kitu ambacho kitamgharimu hata huko ACT, akitokea mwanachama atakayepingana na misimamo yake ndipo hapo rangi zake halisi Zitakapoonekana

Kwasasa yupo HONEYMOON!kila kitu ni shangwe tu. Fungate hili likiisha akatulia ofisini ajenge chama ndipo hapo tutakaposhuhudia maajabu! Ni suala la muda tuu..!!!
 
Last edited by a moderator:
Katika nchi kama ya kwetu ambayo ujenzi wake uliishia kwenye msingi ambao tunaubomoa, hakuna chama cha siasa kilicho bora. Ili kuwa na kikundi kinachojiita cha siasa, inabidi uwe na taifa linalojitambua na kujielewa. Taifa linalofahamu wapi limetoka na wapi linaenda. Taifa la namna hiyo linakuwa na dira na falsafa inayofahamika kwa kila mtu. Hili tumeliua Tanzania, nchi pekee katika Afrika kusini mwa jangwa la Sahara iliyoanza kujijenga. Bado safari ni ndefu. Tunaoangalia mbali, tunakazia Pan-Africanism.
 
Makamanda CDM Wote acheni kujadili hawa vibaraka wa CCM-ACT, kikubwa tupange mikakati ya ushindi. Kuendelea kuwajadili hawa wasaliti ni kupoteza wakati bure.
Rai yangu; Elimu ni muhimu kwa wanachi, kila kamanda awe mjumbe kwa jirani yake katika kumng'oa mkoloni mweusi huyu CCM na vibaraka wake.
MUNGU nibariki Mimi pamoja na familia yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…