Sasa mke basi!

Sasa mke basi!

hivi hao wakwe ujana wao wamekula wapi hawajajenga uje kuwajengea wewe.... hapo biga mimba mfulululizo kisha wote kimya, pia jitahidi kukomaa nao!
 
Duuh hiyo kari mkuu cjawahi ona me niungane na mdau mmoja yeye amekwenda mbali na kutofasili nyumba kuwa mimba me nafikli nikwel hayo ni mafumbo we wakiendelea kukusumbua wambie waandae matilio we utakwenda kujenga kwan wao siwalianda mkeo ndo ukafika hapo ili kuowa hivyo nanyumba waadae matilio we ukajege au mnasemeje wadau.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Chukua ndugu zako uwapange waanze kudai mkeo awajengee nyumba uone reaction yake itakuwaje.

Halafu mpeleke mkeo shule maana inaonekana kichwani ni mtupu hata kama anaelimu haijamsaidia chochote.
 
ww acha mambo ya ajaabu. mwambie my wife wako mjenge nyumba fasta sana. usirembe. (MIMBA TU WANATAKA)
 
Asalaam alaykum wanajamvi,

Ni mara yangu ya kwanza kushiriki kwa namna ya kutuma post mpya, nimekuwa nikishiriki kwa kusoma tu post za wanajf wengine, lkn sasa msaada wenu wa kimawazo unaweza kunisaidia nikajua ni jinsi gani naweza kufanya.

Kiufupi ni muda mfupi nimejipatia jiko baada ya kukaa kwa muda mwingi sana bila mke, nimejikusanya saana kwa muda mrefu na kwa kujibana ili nipate mke ambaye tutasaidiana kupata suluhisho la matatizo ya kimaisha, lakini sasa naona ndio kwanza matatizo yameongezeka, nimeoa kama mwezi mmoja uliopita na namshukuru mwenyezi Mungu mke wangu nampenda sana ila kikwazo kikubwa kinakuja upande wa wakwe zangu, nimekuwa nikisumbuliwa tangu siku ya pili kugunga ndoa kuwa natakiwa kuwajengea.

Mara ya kwanza nilifikiri labda ni utani wa mashemeji zangu wa kike maana ndiwo walianzisha maada hiyo lkn siku zinavyozidi kwenda napigiwa simu na watu waheshima sana kwangu [wakwe] na kusisitiza jambo hilo, nikajaribu kumueleza habari hizo mwandani wangu nikakuta naye anawaunga mkono, sina uwezo wa kifedha ni maisha ya kawaida saaaaana ambayo sioni sababu ya kukandamizwa kiasi hiki kwa kitu ambacho sii ridhaa yangu au kwa muda mfupi kiasi hiki? yaani kwakweli mpaka sasa nimekoswa furaha na ndoa yangu hata hamu ya kuwa karibu na mke wangu pia imetoweka.

Sasa ndugu zngu nishaurini maana mpaka sasa naanza kujuta kuoa sababu uwezo wa kuwatimizia kile wanacholazimisha kwasasa sina na pia inaonekana hawanielewi na utafikiri labda tulifunga nao mkataba huo.

Asanteni sana.
pole xan mkuu..nahc ulwaonyesha ka una pesa wakati unamchumbia binti yao ndo tatzo
 
Haina haja mkuu, dawa ni kusimama katika nafasi yake!Mkwe hawezi kumpelekesha bwana!!Mbona sie tumeolewa na wazazi wetu wana heshima sana kwa waume zetu?Kama shida wanazipata na wanazitatuzawao, ukiona wamemshirikisha mume wa binti yao basi ni tatizo kubwa sana!Tatizo hapa ni familia ya mke, inaelekea ni wale ambao hufurahia kuzaa watoto wa kike ili waje wawaoze kwa mahari kubwa au wame tegemezi kwa watoto wao.
i got u sana tu ila uko mbeleni lazima pawe na shoda kama akiamua kuvumilia yaani wezi mmoja tu wa ndoa unadai ujengewe nyimba what if ikifika miaka miwili wataomba wajengewe nini,ofcourse mume anaweza akasimama kwenye nafasi yake lakini hilo swala lityakuwa linamtafuna kuona hamna maelewano mazuri na uopande wa mkwe coz mtu unaoa ili upatye amani ya moyo na pumziko kama inakuwa vinginevyo its boring
 
Makubwa jamani ndoa ina mwez wakwe wanaomba wajengewe nyumba mh bas wana njaa sana wapo kimaslahi zaidi
 
Kuna mdau kasema labda mtoa mada ni fundi ujenz ndo alikuwa anaombwa akapunguze garama za fundi hahaha
 
Wajengee mimba kwenye tumbo la binti yao.... Ndicho wanachomaanisha..... Lugha za mafumbo madogo zinawapiga chenga sana. Au ulifikiri wanataka umlishe tofali binti yao?

ahahahahaaa mkuu umetisha mweeeeeeeeeeee
 
Mkwe wangu hawezi kuniomba hata hela kama ana tatizo anaongea na mtoto wake ndo ananiambia ni kama ni shida ya msingi naisolve wala si kulazimishana! Sembuse kujengaB-) lo!
 
Back
Top Bottom