Sasa mke basi!

Nsame

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
474
250
Asalaam alaykum wanajamvi,

Ni mara yangu ya kwanza kushiriki kwa namna ya kutuma post mpya, nimekuwa nikishiriki kwa kusoma tu post za wanajf wengine, lkn sasa msaada wenu wa kimawazo unaweza kunisaidia nikajua ni jinsi gani naweza kufanya.

Kiufupi ni muda mfupi nimejipatia jiko baada ya kukaa kwa muda mwingi sana bila mke, nimejikusanya saana kwa muda mrefu na kwa kujibana ili nipate mke ambaye tutasaidiana kupata suluhisho la matatizo ya kimaisha, lakini sasa naona ndio kwanza matatizo yameongezeka, nimeoa kama mwezi mmoja uliopita na namshukuru mwenyezi Mungu mke wangu nampenda sana ila kikwazo kikubwa kinakuja upande wa wakwe zangu, nimekuwa nikisumbuliwa tangu siku ya pili kugunga ndoa kuwa natakiwa kuwajengea.

Mara ya kwanza nilifikiri labda ni utani wa mashemeji zangu wa kike maana ndiwo walianzisha maada hiyo lkn siku zinavyozidi kwenda napigiwa simu na watu waheshima sana kwangu [wakwe] na kusisitiza jambo hilo, nikajaribu kumueleza habari hizo mwandani wangu nikakuta naye anawaunga mkono, sina uwezo wa kifedha ni maisha ya kawaida saaaaana ambayo sioni sababu ya kukandamizwa kiasi hiki kwa kitu ambacho sii ridhaa yangu au kwa muda mfupi kiasi hiki? yaani kwakweli mpaka sasa nimekoswa furaha na ndoa yangu hata hamu ya kuwa karibu na mke wangu pia imetoweka.

Sasa ndugu zngu nishaurini maana mpaka sasa naanza kujuta kuoa sababu uwezo wa kuwatimizia kile wanacholazimisha kwasasa sina na pia inaonekana hawanielewi na utafikiri labda tulifunga nao mkataba huo.

Asanteni sana.
 

kayimukaa

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
356
250
shee, polel mkuu, ila huyo mke ni kabila gani na katokea mkoa gani ili tuanze kujihadhari, kweli ukistaajabu ya musa utaona ya firauni.
 

g click

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
2,429
1,225
Wajengee mimba kwenye tumbo la binti yao.... Ndicho wanachomaanisha..... Lugha za mafumbo madogo zinawapiga chenga sana. Au ulifikiri wanataka umlishe tofali binti yao?

hahaha mambo ya lugha ya picha
 

MWAMUNU

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
669
250
Sasa mbona kwenye kichwa cha habari umesema sasa mke baaasi ! Mi nikajua umeshammwaga !!
Hii story yako imekaa ki uongo uongo kajipange uje upya, haiwezekani umeoa mwezi uliopita leo wakudai nyumba? Labda kama ulitongoza kwa gia ya kuwajengea nyumba wazazi wake.
Ndo ujenge nyumba ya watu sasa !!!
 

mkwawa1

Member
May 2, 2014
58
0
pole sn kk.ila inaonyesha hilo walikuwa wanaliombea litokee mapema sn na imetokea km hvo.
nadhan kaa na mkeo mwelekeze hali halis kuwa hata nyie hamjajijenga bado,hvo wawape muda mjipange kwnz kwa kujenga nyumba/familia yenu kwnz.then mnaweza kuwasaidia na wao maana huwez kuwasaidia wao wakat na nyie bado mnauhitaj .
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,236
2,000
Pole kaka. Ila hilo lisikuumize akili hata kidogo. Wewe si mwanaume kamili? Chora mstari wa maisha yako na watu wasikuzoee. tena waambie kama vipi waje mamchukue wamuozeshe kwa kina Bahresa ili wajengewe nyumba. Washajipanga hao na ukijenga tu anakutoroka huyo mke. walaah nakuapia. Kingine nenda kwa viongozi wa dini upate ushauri na pia usisahau kuwashirikisha ndugu zako ili wakupe ushauri. Pole sana ndo maisha yalivyo, Umeoa Tanga nini kijana?.
 

Baba Matatizo

JF-Expert Member
May 5, 2011
334
195
pole mkuu.hata mimi juzi ndo shemeji yako karud home kwa mgogoro mdogo.sasa ushauri wangu ni huu.waeleze wazazi wa mkeo kwamba huna uwezo wa kuwajengea kwani si lazima ila ni kama hisani.pia mkeo mwambie kwamba wewe umemwoa ili mjikomboe na kizazi chenu na si vınginevyo.kuwajengea huwa kunakuja automaticaly na sio kwa kulazimishana.pia mgogoro ukizid peleka kwa wazee wa msikiti au kanisa mjadili kwa pamoja.mwishownakupa pole kuoa kwa familia masikin wa mawazo na kipesa.mimi kwa dini yangu moja kati ya sababu ya kumuoa mke ni mali alizonazo.POLE SANA PIA USIMWACHE MKE WAKO.
 

Munkari

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
8,091
2,000
Mmmh hapo ndo linapokuja suala la NDOA NDOANO!! hivii mnawaokotaga wapi wanawake wenye akili fupifupi kama hao?? Bila shaka unakaudhaifu flani bwana wee!! I wish ungekuwa kakangu afu unaniambia hizi habari! Anyway simama kama mwanaume fanya unaloweza ukiwaendekeza haki ya nani nakwambia UTAFANYWA MTUMWA wa wakwe zako.btw huyo mkeo ni kabila gani??? Nalo linachangia!!
 

lad3

Senior Member
May 25, 2014
186
195
mh! pole sana,,,jaribu kuongea nao hali halisi ya maisha yako,,, ikishndikana pia tafuta watu wenye hekima na viongozi wa dini uwaambie wakaongee nao wakwe wasipokuelewa hapo unaweza kufanya maamuzi magumu kwa kuwa mkeo nae anawaunga mkono wazazi wake.
 

Vituka

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
2,238
2,000
Hilo sio jambo la kukufanya wewe uichukie ndoa yako!Huwa nasema siku zote jamani, ebu wanaume kuweni WANAUME KWELI kwenye ndoa zenu!!!Hivi shemeji yako anapata wapi ujasiri wa kukuambia eti ni lazima ukajenge kwao? Wanaume wetu siku hizi yaani hampo serious kabisa ndo mana mnayumbishwa ovyo!Sasa hizo habari wakisikia ndugu zako hiyo ndoa ndo basi tena!

Ushauri wangu kwako ndugu, kwanza mkalishe mkeo chini, AKUSIKILIZE WEWE NA AFUATE KILE UKITAKACHO WEWE!!AJue kuwa nyie wawili ndo mnatakiwa muijenge familia yenu SIO YA WAZAZI WAKE!Tena umwambie hivyo ndivyo unataka na hauko tayari kujenga kwao kwa sasa labda hapo baadae kama utapata uwezo huo. ANGALIZO, kama upo timamu kichwani na mkeo anajua upo timamu basi atakuelewa ila kama ndo ivyo tena ushachezewa mchezo mchafu na mkeo ujue UTAJENGA TU HATA IWEJE?Pole lakini
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,970
2,000
Kwani wewe mleta mada ni mjenzi? kama sio mjenzi waambie ukweli tuu. Inawezekana wakwe zako wanafikiri proffesion yako wewe ni mjenzi.
 
Mar 12, 2014
16
45
Lakini mke wako si anajua hali halisi ya maisha yenu?yeye ndo alitakiwa kuwa mstari wa mbele kuwaeleza wazazi wake kwamba bado hamko tayar kwa sasa na pili kuwajengea ni hiari yako na si lazima kama itakupendeza ukiwa na uwezo huko mbele utawajengea.
 

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,499
2,000
Wajengee mimba kwenye tumbo la binti yao.... Ndicho wanachomaanisha..... Lugha za mafumbo madogo zinawapiga chenga sana. Au ulifikiri wanataka umlishe tofali binti yao?

umetisha sana mkuu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom