Sasa mbona ananisumbua?

Sasa mbona ananisumbua?

Mtarudiana na atakupa mtoto mwingine maana nyie wanawake kumbukumbu mnazo ila siyo za kudumu ndiyo maana kuzalishwa watoto watano kila huyo na baba yake rahisi mno kama simba kuwafunga yanga huku wakiwa pungufu.
 
Huyo mtoto ana haki ya kumsalimia babake lakini isiwe ndo gia ya wewe kutaka kurudiana na mtalaka wako. Alikuacha mwenyewe, hivyo vitisho ni vya nini. Alikuwa hakupendi na hatokaa akupende milele, anatumua udhaifu wako aje afaidi ulivyonavyo. Wala usimtie maanani
Mbona una mzibia baba watoto kurudi!!?
Mwache walee mtoto
 
Huyo mtoto ana haki ya kumsalimia babake lakini isiwe ndo gia ya wewe kutaka kurudiana na mtalaka wako. Alikuacha mwenyewe, hivyo vitisho ni vya nini. Alikuwa hakupendi na hatokaa akupende milele, anatumua udhaifu wako aje afaidi ulivyonavyo. Wala usimtie maanani
Ahsante
 
Hivi hii busara umeitoa wap shunie Jaman khaa mbna sio wa hvyo wewe.
Back to the topic kama unaomba ushaur means bado unampenda other wise usingejisumbua nae.
So kama unamtaka mrudie otherwise usje ukaanzisha thread nyengne
mm nina busara Bonny basi tu huwa haunikubali unaniona kiazi

huyo dada anampenda huyo jamaa acha wakaongeze mtto mwingine wa pili, kuna vitu vingine ujue sio kila kitu kinachokukuta unakimbilia jf kuomba ushauri vingine unamalizana navyo mwenyewe.
 
Huyo mtoto ana haki ya kumsalimia babake lakini isiwe ndo gia ya wewe kutaka kurudiana na mtalaka wako. Alikuacha mwenyewe, hivyo vitisho ni vya nini. Alikuwa hakupendi na hatokaa akupende milele, anatumua udhaifu wako aje afaidi ulivyonavyo. Wala usimtie maanani
hivi Dada mtto wako uliyemzaa kweli atakupanda kichwani
 
Wewe ndio unaweza kuamua, kama humtaki kaa mbali naye. ukitaka mrudiane ili mlee mtoto sawa, na kama bado unampenda ni vizuri urudiane
May be kabadilika.
Mkuu mbona kama unamrudisha mleta uzi kwenye moto wa jehannam??
 
Wewe ndio unaweza kuamua, kama humtaki kaa mbali naye. ukitaka mrudiane ili mlee mtoto sawa, na kama bado unampenda ni vizuri urudiane
May be kabadilika.
Simpend Tena na siko tayar kurudiana nae
 
Chimbuko la matatizo yote ni wewe mwenyewe kulazimisha ndoa kwa mtu asiyekutaka kwa kigezo cha eti 'alishakula tunda'....pole

Huyo mwanaume tangu mwanZo hakuwahi kukufaa...usitarajie atakufaa sasa hivi
Niliona alishaniharibia yeyote mwengne acngeniamn
 
ila dada yote aliyokufanyia huyo mwanaume kweli una hamu ata ya kuja kumwanzishia thread uombe ushauri ww bado unampenda huyo jamaa kazi kwako
Baada ya hii post yako ilitakiwa thread ifungwe.
Huyu dada ni mpumbavu.
Hilo toto nalo lina akili za baba yake.
Ni lipumbavu pia.

Kungekuwa na chuo kinachofundisha nyodo ningekulipia ukasomee.
Huyo mumeo kwanza hutakiwi hata ujibu meseji zake. Block kabisa.
Kama mwanae anataka kwenda kwa baba yake na umri unaruhusu mwache aende.
Wewe kufa na maisha yako.
Mwanaume kama huyo ukimkubali tu ni mkosi. Utashangaa unafikisika na unaanza kuhangaika tena na atakukimbia.
Kwanza lazima atakuwa ni mchawi. Binadamu wa kawaida hawezi kujitoa ufahama kiasi hiki
 
Yy ndio anaemtafuta mtoto anaenda hadi shule na kwa Bibi yake pia anaenda kumtia maneno mpk yameshamjaa ukizingatia jamaaa Mambo yamemchachia sa iv Ni fundi cm
Lazima yamchachie cuz "to every action,there is equal&opossite reaction".
Malipo ni hapahapa duniani,
Hivyo akili kumkichwa mkuu..
 
Huyo mapenzi hana anachopenda pesa kama na ww sikio la kufa basi rudiana nae
 
Mm Ni kijana mwenzenu, Nina utata kidogo ktk maisha yangu naomba mawazo yenu.

Nilipata kuwa na mahusiano na kijana mwenzangu wakat tukiwa chuo. Mapenz yetu yalikuwa matam tu tulipendana sana, mpk ilipofika hatua ya kumaliza chuo yule kijana akaenda kwao na mm nikawa nipo tu home.

Kwa vile kila mmoja alikua anakaa mbali na mwenzie na mm nilikuwa cwez kukaa mbali nae nikaamua kumshauri aje nyumbn kuniposa anioe. Yaani kumuambia suala la ndoa tu akawa km nimemfukuza.

Nikafanya jitihada nikamtafuta nikamuambia lazima anioe Mana alishakula tunda langu, ikawa ugomvi hataki mpk wakaingia wazee akalazimishwa akalazimishwa ndo akakubali kunioa.

Baada ya kunioa nilijuta Bora ningekaa nyumbani nikatafuta issue nikafanya , yn mume alikuwa ananipiga, ananisimbulia, ananisimanga kila baya ananifanyia. Huduma Hana ukimuambia anasema kachukue kwenu me sikutak.

Dah nikastahmili nikapata mimba, nilipopata tu mimba mume wangu alizid vituko harud kabisa cjui analala wap. Siku Moja akaniambia nenda kwenu me nataka kusafr, apo nilikuwa na mimba 6 months.

Kumbe yule bwana hakusafr Wala nn anaonekana mjini anadunda nikaja kusikia keshaoa mke mwengine kwangu hapiti kabisa. Nikimpgia cm hapokei Hana mawasiliano na mm iliniuma sana. Kwa uchungu na hacra nikazaa nikiwa na mimba miez Saba.

Baada ya kujifungua niliumwa sana na mtoto pia alikua mgonjwa, babaake alibadlisha namba na tulipokuwa tunakaa akahama.

Ndipo nilipoenda kwao kumuulizia lkn nashangaa ndugu zake walinidharau na kunicheka Kisha wakanipa waliosema mzigo Wangu ambayo ilikua Ni talaka.
Mume wangu aliniacha ktk Hali hii ngumu mm naumwa na mtt anaumwa kwa kweli nilikua namuhitaji nikaondoka nikashukuru mungu.

Kwa kwel nilipoteza muelekeo nikakosa dira nikijiangalia baba yangu alishakufa, mama nae mtu mzima Hana kitu. Nilisomeshwa kwa msaada wa jumuia fulan lkn nilishindwa kufanya vizur kutokana na mapenz nilijuta na kulia sana.

Sikua na msaada nikawa nauza maandazi kwa ajili ya kujikimu mm na mtoto na mama pia.

Siku Moja katika pita pita zangu nikakutana na rafiki yangu wa zamani alinishangaa kuona nilivyochoka akaniuliza yamenikuta yepi? Nikamuhadithia akanihurumia sana nilishaanza kukonga wakati nilikuwa na 23 years old.

Rafiki yangu akaniuliza unataka kufanya kaz za ndani Oman nikamuambia ndio, akanipeleka kwa mtu fulan hivi akaniambia yy atanifanyia Safari. Bac nikaondoka Tanzania nikaenda Oman mwanangu akiwa na miaka 3 na alikua anaendelea vizur japo alikua mwembamba sana.

Nashkuru mungu kumbe hii ilikua ndio njia yangu ya kunifungulia milango ya kheri na barka, nikawa napata pesa Sasa natuma nyumbani. Niliporud nikakuta nyumba yetu ishajengwa vizur na milango ya maduka miwili. Sikutosheka nikarud Tena Oman tukafungua biashara pale home duka Moja la vyakula na Moja stationaries Kuna ndugu zangu wanauza pamoja na mama. Niliporud Tena nikajenga nyumba yangu na biashara ikakua nimekod mlango mjini nikaweka nguo za kike. Huu mwaka wa tano nipo Oman nataka nikirud next year iwe ndo mwisho sirud ntakuwa na kila kitu nilichokuwa nahitaji.

Tatizo Sasa yule kijana aliyeniacha kwa dharau akanifanya nichukie wanaume wote amepata habari zangu na mtoto kampa namba yangu ananipigia kila sekunde ananiambia mke wangu turudiane tulee mtoto wetu. Jaman na mtoto nae anasema nirud kwa babaake km sitak nikiolewa na mtu mwengine atamuua.

Nipo njia panda nampenda sana mwanangu Ila siko tayar kurudiana na yule babaake nifanyeje jamani!!
Wewe ni hayawani!
 
Baada ya hii post yako ilitakiwa thread ifungwe.
Huyu dada ni mpumbavu.
Hilo toto nalo lina akili za baba yake.
Ni lipumbavu pia.

Kungekuwa na chuo kinachofundisha nyodo ningekulipia ukasomee.
Huyo mumeo kwanza hutakiwi hata ujibu meseji zake. Block kabisa.
Kama mwanae anataka kwenda kwa baba yake na umri unaruhusu mwache aende.
Wewe kufa na maisha yako.
Mwanaume kama huyo ukimkubali tu ni mkosi. Utashangaa unafikisika na unaanza kuhangaika tena na atakukimbia.
Kwanza lazima atakuwa ni mchawi. Binadamu wa kawaida hawezi kujitoa ufahama kiasi hiki
Nimeshablock Ila sometimes anatumia namba ya mtt kunipigia
 
Back
Top Bottom