Sasa Au Sio Sasa.

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
Sasa Au Sio Sasa.
Tumekuwa tunajidanganya sana, na katika kujidanganya huku tumekuwa tukipoteza muda mwingi na kushindwa kukamilisha yale ambayo ni muhimu sana kwetu.

Kuna mambo mengi ambayo tunafikiri tunataka kuyafanya, na hivyo kusema tutayafanya baadae. Lakini hii baadae huwa haifiki, na wakati mwingine tunasahau kabisa kama tulishafikiria baadae tutafanya jambo kama hili.

Kwa kuwa baadae haifiki, na kwa kuwa sasa ndio tunapanga jambo, kuna njia nzuri sana ya kuhakikisha unafanya kile kilicho bora kwako kwa wakati sahihi.

Njia hii ni kutumia dhana ya SASA AU SIO SASA.
Kwa dhana hii unaangalia jambo unalotaka kufanya na kujiambia je nipo tayari kulipafanya sasa? Kama ndiyo basi unalifanya. Kama siyo unaachana nalo na kuendelea na lile muhimu unalofanya sasa. Kwa dhana hii kila wakati unakuwa unafanya jambo ambalo ni muhimu kwako.

Chochote unachotaka kufanya, ni utakifanya sasa, kwa kuacha unachofanya sasa au hutakifanya sasa kwa kuendelea na unachofanya.

Ukiweza kutumia hilo vizuri utakuwa na matumizi mazuri ya muda na utafanya yale ambayo ni muhimu kwako.
Kwa mfano kuna kipindi nilikuwa nafungua makala nyingi sana kwenye browser ya tablet yangu. Labda unakuta napita facebook, halafu naona link ya makala nzuri, naifungua lakini najiambia nitaisoma baadae. Siku moja naangalia nikakuta kuna makala kama 80 nimefungua na zote sijasoma na umeshapita kama mwezi.

Nilichofanya ni kufura zote na kujiwekea utaratibu kwamba kama nafungua makala au kitu chochote ni nakisoma sasa au sitakisoma kabisa. Nidhamu hii ndogo imenifanya kuchagua makala chache ambazo ni bora sana, na hata ninapoanza kusoma makala na kuona sio bora kama nilivyofikiri naifunga mara moja
 
Ukweli mtupu. Baadae baadae ikizidi unakuja kushtuka mda umekupita
 
Back
Top Bottom