Sina mengi ya kueleza katika hili zaidi ya yale ambayo nimeshaeleza sana kwa jamvi hili! Kilichopo, ni kurudia rudia tu yale yale! Sijapata sababu ya kubadilisha msimamo wangu ktk hili; kwa hakika kama kilichotokea ndicho ambacho tumekuwa tukikisoma kwenye magazeti basi ni lazima matokeo yatenguliwa! Mwenye hamu ya kuikosoa serikali, asubiri jambo lingine na sio hili la kutaka kutumika viwango vya zamani!
I've the same standing......it's wasn't fair at all! Mitihani imefanyika somewhere around October - November huku wahusika wakuu (wanafunzi wakiwa wanafahamu wazi kwamba grading ipo vipi)!! Mitihani wameshafanya, wametulia nyumbani wanasubiria matokeo; huku nyuma wapuuzi wachache wanakaa na kuweka viwango vipya....NO, UNACCEPTABLE! Narudia, wengi wetu tunatamani kila wakati tupate sababu ya kuilaumu serikali; hapa wasilaumiwe kwa kurudisha viwango vya zamani bali walaumiwe kwa kutumia viwango vipya kinyemela (bila wahusika waathirika wakuu wanafunzi) kufahamu! Tuache ubinfasi wa kujiona tumeshavuka mto!
Let's be sincere, hapa JF nafahamu kuna wanafunzi wengi wa vyuo vikuu! Assume, tangu unaingia First Year unafahamu (say) C inaanzii 50-64; na umefanya paper unafahamu hivyo ndivyo viwango! Hatimae unarudishiwa paper yako, unakuta umepata 52; unapumua kidogo coz' unafahamu umepata C. Matokeo yanawekwa notice board, unakuta somo husika umewekewa D; unakuja kuhoji unaambiwa mara baada ya mitihani kwisha; board ilikaa na kuweka viwango vipya ambavyo C inaanzia 55-69! Let's be honest here...hivi kweli huko vyuoni kungekalika?! Yaani from nowhere, muambiwe viwango vimebadilishwa tena kimya kimya! HAPANA, HILI HALIKUBALIKI! Hao wote waliokaa na kupitisha maamuzi sio waathirika wa moja kwa moja, waathirika wa moja kwa moja ni wanafunzi waliohusika na wazazi/walezi wao!
Huyo Mkandara kama ataona haridhiki na lolote litakalofanywa katika hilo, ana haki ya kujiuzuru. Sipingi kubadilishwa grading, napinga kubadilishwa grading wakati watoto wameshafanya mitihani yao! Hili, halikubaliki hata kidogo! Halikubaliki duniani, wala ahera! Wakibadilisha kwa hawa 2013 ni sawa, coz' tayari issue imeshafahamika! Just imagine, hata walimu kadhaa wa shule za skondari ikiwamo ya Azania walipohojiwa kuhusu kutumika kwa viwango vipya; walisema hawakuwa na taarifa hiyo! Kama si upumbavu kuwa nini? Yaani watu wachache wakae ofisini kufanya maamuzi yanayoathiri maelfu ya watu, HAPANA!