Sarakasi za Matokeo zaendelea!

Sarakasi za Matokeo zaendelea!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Katika kile kinachoonekana kama kufanikisha mipango ya kuyaidhinisha kwa lazima Matokeo ‘mapya' ya Kidato cha Nne,Serikali imedhamiria kutumia ipasavyo nafasi ya kutokuwepo kwa Prof .Rwekaza Mukandala kuyapitisha.

Prof.Mukandala ,ambaye ni Mwenyekiti wa NECTA na Makamu Mkuu wa UDSM, hayuko nchini kwasasa.Taarifa rasmi zinaoonesha kuwa Prof.Mukandala yuko nchini Marekani kuhudhuria Mahafali ya mtoto wake ambaye anahitimu katika chuo kimojawapo nchini humo.

Huku yeye akitarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa juma lijalo,Serikali imeapa kuyapitisha na kuyaidhinisha matokeo hayo bila ya uwepo wa Mwenyekiti wa NECTA. Yuko kigogo mmoja wa NECTA ambaye amepangwa kukaimu Uenyekiti wa NECTA kwa ajili ya kupitisha matokeo hayo mapya tu.

Prof.Mukandala,akiungwa mkono na Katibu Mtendaji waNECTA,Dr.Joyce Ndalichako,tangu mwanzo wa mchakato wanapinga kusahihishwa au hata kupangwa upya kwa Matokeo ya Kidato IV-2012 kwa kile wanachosema kuwa Serikali ilishiriki kuyaidhinisha ya mara ya kwanza na hivyo haiwezi kuyabadili.

Katika siku za hivi karibuni,kumekuwa na mvutano mkali kati ya Maafisa Waandamizi wa NECTA na wale wa Serikali juu ya upangwaji upya wa matokeo hayo. Serikali inasisitiza kuwa matokeo hayo lazima yabadilishwe ili kukidhi haja ya Taifa kupata ‘elimu bora'.

Mengi yatajitokeza na mtayajua waungwana wote wa Tanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Kumbe yameshabadilishwa imebaki kumwaga saini peke yake?!!! Ya nini kuviziana kama majogoo yanapigana? Kama serikali imetumia superiority yake kusema matokeo yabadilishwe, then Mkandara na Ndalichako wapishe hizo nafasi, ili serikali kufanya kile ambacho inataka kufanya... Wakifanya hivyo historia itawakumbuka. Kuna haja gani ya kuficha mihuri na kutatalia na saini zao?
 
God have mercy on the Tanzanians!We have the most corrupt and incompetent Government in history.We are heading right to the collapse as a Nation.Sadly some ------ are just smiling and gigling while we are all in the same ship-wreck?
 
Yaani kumbe Profesa yeye mtoto wake anasomea Marekani? Najaribu kufikiria ni viongozi wangapi wana watoto wao wanaosoma nje ya shule za serikali na kwa maana hiyo hata wanashindwa kujali ubutu wa elimu yetu kwa wakati huu. Ndio maana haishangazi wanapochukua maamuzi ya ajabu ajabu kama haya ya kubadilisha alama ili watoto wafaulu au kushusha viwango vya ufaulu ili watoto wengi waende sekondari. Haya yote yanapatikana Tanzania tu kwa hisani ya watanzania..
 
Individuals wenye msimsmo thabiti wa kuipinga serikali katika nchi yetu ni kama vile hakuna na hasa kwa watumishi wa umma.Ninachoamini ni kuwa mwisho wa siku viongozi hao wa NECTA watafanya kile serikali inachokitaka.

Ni swala la muda tu!

Hakuna wa kujiuzulu hapo na wala msidanganyike!
 
Hapa kuna somo. Necta mpya baada ya katiba mpya should be independent. Kwa sasa gvt itafanya inavyotaka kwa kuwa demokrasia sasa pembeni ' ni liwalo na liwe'.
 
Sina mengi ya kueleza katika hili zaidi ya yale ambayo nimeshaeleza sana kwa jamvi hili! Kilichopo, ni kurudia rudia tu yale yale! Sijapata sababu ya kubadilisha msimamo wangu ktk hili; kwa hakika kama kilichotokea ndicho ambacho tumekuwa tukikisoma kwenye magazeti basi ni lazima matokeo yatenguliwa! Mwenye hamu ya kuikosoa serikali, asubiri jambo lingine na sio hili la kutaka kutumika viwango vya zamani!

I've the same standing......it's wasn't fair at all! Mitihani imefanyika somewhere around October - November huku wahusika wakuu (wanafunzi wakiwa wanafahamu wazi kwamba grading ipo vipi)!! Mitihani wameshafanya, wametulia nyumbani wanasubiria matokeo; huku nyuma wapuuzi wachache wanakaa na kuweka viwango vipya....NO, UNACCEPTABLE! Narudia, wengi wetu tunatamani kila wakati tupate sababu ya kuilaumu serikali; hapa wasilaumiwe kwa kurudisha viwango vya zamani bali walaumiwe kwa kutumia viwango vipya kinyemela (bila wahusika waathirika wakuu wanafunzi) kufahamu! Tuache ubinfasi wa kujiona tumeshavuka mto!

Let's be sincere, hapa JF nafahamu kuna wanafunzi wengi wa vyuo vikuu! Assume, tangu unaingia First Year unafahamu (say) C inaanzii 50-64; na umefanya paper unafahamu hivyo ndivyo viwango! Hatimae unarudishiwa paper yako, unakuta umepata 52; unapumua kidogo coz' unafahamu umepata C. Matokeo yanawekwa notice board, unakuta somo husika umewekewa D; unakuja kuhoji unaambiwa mara baada ya mitihani kwisha; board ilikaa na kuweka viwango vipya ambavyo C inaanzia 55-69! Let's be honest here...hivi kweli huko vyuoni kungekalika?! Yaani from nowhere, muambiwe viwango vimebadilishwa tena kimya kimya! HAPANA, HILI HALIKUBALIKI! Hao wote waliokaa na kupitisha maamuzi sio waathirika wa moja kwa moja, waathirika wa moja kwa moja ni wanafunzi waliohusika na wazazi/walezi wao!

Huyo Mkandara kama ataona haridhiki na lolote litakalofanywa katika hilo, ana haki ya kujiuzuru. Sipingi kubadilishwa grading, napinga kubadilishwa grading wakati watoto wameshafanya mitihani yao! Hili, halikubaliki hata kidogo! Halikubaliki duniani, wala ahera! Wakibadilisha kwa hawa 2013 ni sawa, coz' tayari issue imeshafahamika! Just imagine, hata walimu kadhaa wa shule za skondari ikiwamo ya Azania walipohojiwa kuhusu kutumika kwa viwango vipya; walisema hawakuwa na taarifa hiyo! Kama si upumbavu kuwa nini? Yaani watu wachache wakae ofisini kufanya maamuzi yanayoathiri maelfu ya watu, HAPANA!
 
Katika kile kinachoonekana kama kufanikisha mipango ya kuyaidhinisha kwa lazima Matokeo ‘mapya' ya Kidato cha Nne,Serikali imedhamiria kutumia ipasavyo nafasi ya kutokuwepo kwa Prof .Rwekaza Mukandala kuyapitisha.

Prof.Mukandala ,ambaye ni Mwenyekiti wa NECTA na Makamu Mkuu wa UDSM, hayuko nchini kwasasa.Taarifa rasmi zinaoonesha kuwa Prof.Mukandala yuko nchini Marekani kuhudhuria Mahafali ya mtoto wake ambaye anahitimu katika chuo kimojawapo nchini humo.

Huku yeye akitarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa juma lijalo,Serikali imeapa kuyapitisha na kuyaidhinisha matokeo hayo bila ya uwepo wa Mwenyekiti wa NECTA. Yuko kigogo mmoja wa NECTA ambaye amepangwa kukaimu Uenyekiti wa NECTA kwa ajili ya kupitisha matokeo hayo mapya tu.

Prof.Mukandala,akiungwa mkono na Katibu Mtendaji waNECTA,Dr.Joyce Ndalichako,tangu mwanzo wa mchakato wanapinga kusahihishwa au hata kupangwa upya kwa Matokeo ya Kidato IV-2012 kwa kile wanachosema kuwa Serikali ilishiriki kuyaidhinisha ya mara ya kwanza na hivyo haiwezi kuyabadili.

Katika siku za hivi karibuni,kumekuwa na mvutano mkali kati ya Maafisa Waandamizi wa NECTA na wale wa Serikali juu ya upangwaji upya wa matokeo hayo. Serikali inasisitiza kuwa matokeo hayo lazima yabadilishwe ili kukidhi haja ya Taifa kupata ‘elimu bora'.

Mengi yatajitokeza na mtayajua waungwana wote wa Tanzania!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

Unao uhakika? Au unaropoka tu. Tena bora ungechangia na si kuanzisha mada ambayo hauna uhakika hata chembe. Acha kupotosha umma kwa mambo ya udaku na kufikirika. Hujui lolote kuhusu unachoongea
 
Kwa niijuavyo hii Serikali ya Kikwete,Kanuni na misingi yao mikuu katika uendeshaji wa shughuri za kila siku a Serikali ni:Siasa kwanza Taaluma na Utaalamu baadaye;Ujinga kwanza Weledi baadaye;Uongo kwanza Ukweli baadaye;Dhuluma kwanza Haki baadaye; Ukatili kwanza Huruma baadaye;Uchama kwanza Utaifa baadaye;Usaliti kwanza Uzalendo baadaye;Matusi kwanza Heshima baadaye na orodha bado ni ndefu mno na mno!
 
Watoto wao wanasoma nje ya nchi .. Kwa nini wasiya duplicate matokeo yenu ili mkienda wote kwenye intavieu nyie muonekane vilaza zaidi
 
Hii ni dhambi mbaya sana. Iko siku Mungu atashusha hasira yake na hakuna kiongozi atakayebaki. Mimi nitadumu kwenye maombi. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Linaandaliwa taifa la vilaza kwa faida ya magambas lakini yatakiona cha mtema gogo (sio mtema kuni tena).....
 
Yaani kumbe Profesa yeye mtoto wake anasomea Marekani? Najaribu kufikiria ni viongozi wangapi wana watoto wao wanaosoma nje ya shule za serikali na kwa maana hiyo hata wanashindwa kujali ubutu wa elimu yetu kwa wakati huu. Ndio maana haishangazi wanapochukua maamuzi ya ajabu ajabu kama haya ya kubadilisha alama ili watoto wafaulu au kushusha viwango vya ufaulu ili watoto wengi waende sekondari. Haya yote yanapatikana Tanzania tu kwa hisani ya watanzania..

nadhani hii ni njia ya kutengeneza matabaka ktk jamii.. Wameona elimu sio thabiti nchini.. Wanawapeleka watoto zao nje ili waje kuwatawala wale wengi ambao wanaelimu ya kustandardiziwa .. Hatari mkuu
 
Sina mengi ya kueleza katika hili zaidi ya yale ambayo nimeshaeleza sana kwa jamvi hili! Kilichopo, ni kurudia rudia tu yale yale! Sijapata sababu ya kubadilisha msimamo wangu ktk hili; kwa hakika kama kilichotokea ndicho ambacho tumekuwa tukikisoma kwenye magazeti basi ni lazima matokeo yatenguliwa! Mwenye hamu ya kuikosoa serikali, asubiri jambo lingine na sio hili la kutaka kutumika viwango vya zamani!

I've the same standing......it's wasn't fair at all! Mitihani imefanyika somewhere around October - November huku wahusika wakuu (wanafunzi wakiwa wanafahamu wazi kwamba grading ipo vipi)!! Mitihani wameshafanya, wametulia nyumbani wanasubiria matokeo; huku nyuma wapuuzi wachache wanakaa na kuweka viwango vipya....NO, UNACCEPTABLE! Narudia, wengi wetu tunatamani kila wakati tupate sababu ya kuilaumu serikali; hapa wasilaumiwe kwa kurudisha viwango vya zamani bali walaumiwe kwa kutumia viwango vipya kinyemela (bila wahusika waathirika wakuu wanafunzi) kufahamu! Tuache ubinfasi wa kujiona tumeshavuka mto!

Let's be sincere, hapa JF nafahamu kuna wanafunzi wengi wa vyuo vikuu! Assume, tangu unaingia First Year unafahamu (say) C inaanzii 50-64; na umefanya paper unafahamu hivyo ndivyo viwango! Hatimae unarudishiwa paper yako, unakuta umepata 52; unapumua kidogo coz' unafahamu umepata C. Matokeo yanawekwa notice board, unakuta somo husika umewekewa D; unakuja kuhoji unaambiwa mara baada ya mitihani kwisha; board ilikaa na kuweka viwango vipya ambavyo C inaanzia 55-69! Let's be honest here...hivi kweli huko vyuoni kungekalika?! Yaani from nowhere, muambiwe viwango vimebadilishwa tena kimya kimya! HAPANA, HILI HALIKUBALIKI! Hao wote waliokaa na kupitisha maamuzi sio waathirika wa moja kwa moja, waathirika wa moja kwa moja ni wanafunzi waliohusika na wazazi/walezi wao!

Huyo Mkandara kama ataona haridhiki na lolote litakalofanywa katika hilo, ana haki ya kujiuzuru. Sipingi kubadilishwa grading, napinga kubadilishwa grading wakati watoto wameshafanya mitihani yao! Hili, halikubaliki hata kidogo! Halikubaliki duniani, wala ahera! Wakibadilisha kwa hawa 2013 ni sawa, coz' tayari issue imeshafahamika! Just imagine, hata walimu kadhaa wa shule za skondari ikiwamo ya Azania walipohojiwa kuhusu kutumika kwa viwango vipya; walisema hawakuwa na taarifa hiyo! Kama si upumbavu kuwa nini? Yaani watu wachache wakae ofisini kufanya maamuzi yanayoathiri maelfu ya watu, HAPANA!

Nadhani kuna mengi yaliyosemwa ambayo bila shaka hukuyasikia au hutaki kuyatilia maanani. Maelezo yako ni kana kwamba kilichofanywa na NECTA ilikuwa ni maamuzi yao wenyewe.

Utaratibu waliotumia kupanga matokeo ilikuwa ni baada ya michakato iliyoendeshwa na serikali chini ya waziri wa elimu na katibu akiwa Mulugo, na hatimaye wakatoa maagizo rasmi kwa NECTA juu ya utaratibu wa kupanga matokeo.

Sasa cha ajabu watu wale wale waliotoa maagizo ya awali wanakuja na maagizo mapya yanayoashiria kupinga maagizo yao ya awali, kweli hapo utaendelea kutupa lawama kwa NECTA?

Cha ajabu kinachonishangaza, Tume iliyoundwa inaongozwa na mtu ambaye alikuwa mjumbe kwenye kikao kilichoamua kubadilisha utaratibu wa upangaji wa matokeo hayo, leo anakuja na fikra mpya ya kutengua wazo lao la awali. Nadhani haikuwa sahihi Tume kuwa chini ya aliyeshiriki kwenye kutengeneza huo utaratibu
 
Back
Top Bottom