Sarafu ya sh 500 haina ubora!

Sarafu ya sh 500 haina ubora!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,956
Reaction score
25,345
Siku moja tu baada ya BoT kuzindua sarafu mpya ya sh 500 kwa mbwembwe za hali ya juu, imebainika kwamba sarafu hiyo ni kanyaboya! Ni dhahiri kwamba hapa serikali imeingia choo cha kike kwa makusudi yanayofanywa na mafisadi wachache baada ya kujitoa akili na kujitia upofu. Kwanini?

Sehemu kubwa ya sarafu hiyo imetengenezwa kwa madini ya chuma (iron), na tabaka (layer) dogo sana la madini ya nikeli (nickel). Kama mjuavyo, madini ya chuma hupata kutu kwa urahisi sana. Na kwa kuwa tabaka la nikeli ni dogo mno, pindi sarafu hiyo ikipata mkwaruzo kidogo chuma kitakuwa exposed na kupata kutu, hivyo kuharibu sarafu mzima. Kwa maana hiyo sarafu ya sh 500 ikiguswa na unyevu kidogo tu imekula kwako! Wataalamu wa BoT waliochagua kutumia madini ya chuma kutengeneza sarafu hii ama walitumia akili za bandia au walijitoa akili kwanza ndipo wakafanya maamuzi hayo. Walipaswa kumuomba hata mtoto wa shule ya msingi awape ushauri. Ni bora wangetumia madini ya fedha au bati kwa kuwa madini haya hayapambani (unreactive).
sarafu 500.jpg

:yield:
 
Hujui 10% nchi yetu ita tu cost sana,Tanzania sio nchi masikini hata kidogo
 
Lengo la kubadilisha noti ya shilingi 500 kuifanya sarafu ilikuwa ni kutokana na noti hizo kuchakaa mapema kutokana na mzunguko mkubwa. Sasa kama hii sarafu ya 500 ambayo tunategemea pia itakuwa na mzunguko mkubwa imetengenezwa kwa viwango duni kama ulivyoandika basi itachakaa mapema zaidi ya ile noti ya 500. Sasa hapo BOT watakuwa wamefanya nini cha maana?



Nasubiria majibu ya vituko toka BOT. Usishangae ukaambiwa kuwa kupiga kutu kwa hiyo sarafu mpya ya jero ni moja ya alama ya ubora kwani nakumbuka wakati BOT walipobadili noti na watu kulalamika kuwa noti mpya zilikuwa zinachakaa mapema na zinatoa rangi na kuchafua walleti na mifuko yao Gavana alisema kuwa kutoka rangi kwa hizo noti ni moja ya alama ya ubora!
 
Da! aisee! yaani jamaa wakilala wakiamka wanatuletea jambo jipya hata kama halina tija! kazi ipo!
 
No No No mie niwaulize hivi kwanini hizi coin zinapoteza thamani haraka,mfano hakuna karanga ya 50.pia hakuna chungwa ya 100!...wataalam tuelezeni vizuri sio kuwa thamani ya pesa yetu kwisha habari?
 
Nini ni mpango wa CCM kupata hela za uchaguzi
 
Why ,one year before or after g election . Hii biashara huwa ina take place.

Believe it or not, this is a new EPA, Richmond, Meremeta, Escrow and the like!
 
wametengeneza kama sarafu za bandia zinazotumika Hollywood kuigizia muvi

Bora hata zile za Hollywood zina ubora mzuri. Hizi sarafu za Tanzania ni takataka kabisa, uhai wake utakuwa haumalizi hata mwaka mmoja!
 
Back
Top Bottom