Sarafu ya Afrika Kusini yaanguka

Sarafu ya Afrika Kusini yaanguka

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Sarafu ya Afrika ya Kusini, Rand, imeporomoka hadi kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na ile ya dola na hivyo basi kusababisha hasara kubwa katika miezi 19 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ukuwaji mdogo wa uchumi wa China.

Sarafu hiyo ilishuka na kubadilishana kwa 14 dhidi ya dola.

Ni sarafu ambayo imeathiriwa vibaya zaidi miongoni mwa masoko 25 yanayoinuka baada ya wawekezaji kuuza mali zao zilizo hatarini zaidi kutokana na wasiwasi wa ukuwaji wa uchumi wa taifa la uchina ambao ni wapili kwa ukubwa Duniani.


Chanzo: BBC
 
kwa hiyo rand moja inabadilishwa kwa sh za Kitanzania?
 
Ni ngumu sana kuripoti taarifa za kiuchumi....., kwa kweli sijakuelewa. Kwa mbali nimeelewa hivi, sarafu ya Africa kusini (RAND) imeshuka hadi kufikia RAND 14 kwa USD1, hii ni kutokana na mdororo wa ukuaji wa uchumi wa taifa la china uliosabisha wawekezaji kuuza mali zao. Sijui kama nimekupata sawia: Maswali ni haya

Wawekezaji hao wapo china au south africa? kama wapo china mbona sioni direct link? China wameshusha dhamani ya hela yao kwa makusudi, hii inaweza athiri mataifa mengi duniani, lakini kwa nini iwe zaidi south africa? Inategemewa hata US na Europe zitaathirika kwa viwango tofauti (sababu zipo).

Ushauri, weka source ili tupate taarifa kamili kutoka kwa waandishi wa habari za kiuchumi.
 
Zuma's bad economic policies are the major reasons behind the Rand decline.
 
Sarafu nyingi sana zimeanguka hasa za zile nchi zinazoinukia. Na ndo ambazo nyingi zinategemea moja kwa moja kwenye uchumi wachina.
 
Back
Top Bottom