Sanamu za wanyama mzunguko (roundabout) wa Msamvu, Morogoro.

Ta Nanka

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
1,232
1,905
Wiki iliyopita nimepita roundabout ya Msamvu na kuona kazi nzuri ya kutengeneza sanamu zinazoonesha vivutio vyetu. Moja ya sanamu hizo ni ile ya chui akimkamata mamba. Nina tatizo na hii sanamu. Jamii ya chui wenye tabia na uwezo wa kukamata mamba wanaitwa jaguars wanaopatikana bara Amerika. Hawa wanafanana kwa muonekano na hawa chui (leopards) tulionao hapa nchini. Na jamii ya mamba ambao huweza kukamatwa/kuliwa na hawa jaguars wanaitwa caimans ambao hupatikana pia bara Amerika. Caimans wanafanana na mamba (crocodiles) hawa tulionao hapa nchini ila wao, pamoja na tofauti zingine, ni wadogo kwa umbile.

Kwa ufahamu wangu hatuna jaguars wala caimans hapa nchini. Kama hivyo ndivyo, nini mantiki ya kuweka sanamu za wanyama ambao hawapatikani hapa nchini wakati tunao wanyama wengi tu ambao tungeweza kuweka sanamu zao?
 
Picha ipo wapi? Kusindikiza uzi wako
 
Back
Top Bottom