SAMWEL SITTA hatima yako ipo Chadema

Sidhani kama inalipa kuendelea kuhangaika na huyu Sitta maana ni mtu anayedhani kuwa ana nafasi ya kupata madaraka makubwa ndani ya CCM kupitia mtandao aliopo ndani ya chama hicho, ikibidi urais, hivyo hawezi kufikiria kuja CDM, labda itokee kuwa kabanana sana na hana jinsi.Sitta ni mtu mzima, huu ushauri wala hakustahili kupewa bali angekuwa ameshachukua hatua siku nyingi sana hata kabla wadau hamjaanza kumfikiria na kumshauri kama kweli ni alikuwa mpiganaji wa kweli, huyu naye ni opportunists kama walivyo wengine wengi ndani ya CCM, Mwakyembe, Magufuli, Tibaijuka, n.k. , just few to mention!Wadau naomba msisahau jinsi huyu mzee alivyomkejeri Dr. Slaa wakati wa kampeni kuwa JK sio saizi yake bali yeye (Sitta). Pamoja na kejeri hiyo ya kijinga, lakini bado Slaa alimpa ushauri wa kutokuukubali uteuzi aliopewa wa uwaziri wa EA. Sasa kama kakataa kupokea ushauri wa mtu makini kama Dr. Slaa, je atapokea huu ushauri wenu? Tusubiri kwanza ajeruhiwe halafu atatia akili!N.B: Kama kweli Sitta ni mpiganaji, kwa nini baada ya kutishiwa kunyang'anywa uanachama wa CCM wakati anasimamia mjadala wa Richmond, aliamua kufunika kombe ili kuwanusuru mafisadi na chama chake akidai kuwa maazimio yote 23 ya kamati teule ya Bunge yameshatekelezwa na serikali?
 
Mtu anweza kuwa Waziri na bado akawa mpambanaji,kilichoongelewa ni hatima yake kisiasa.upambanaji si wa kimatukio,ni wa kimchakato

Hapo sawa. Ni mchakato madhubuti endelevu usiokwamishwa na mazingira, hali au vikwazo vya watu mpaka kieleweke.
 
kweli kabisa,lakini vipi kama nje kuna mvua?
kwanini usijikinge ndani ya gari bovu afu utoke baadae kulisukuma mvua ikiisha?

But kumbuka mvua ikizidi kuwa kubwa kunamafuriko, na mafuriko yakikukumba unakuwa umepoteza gari kikubwa zaidi maisha yako. Kumbuka wahenga walisema Heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Mwenye Haki, hutafuta haki mpaka aipate haijalishi kaangushwa mara ngapi, akiinuka lake ni moja tu Haki. Na Upiganiaji wa haki ni mchakato yaani tendo endelevu lisilokoma wala kukomeshwa na mtu yeyete mpata kinachotafutwa kipatikane. Usiogope, yupo kwa ajili ya watanzania.

Kusaliti wenzio ndiyo kutafuta haki, nadhani mara mbili inatosha huyu ni wa kustaafu tu siasa!
 
Sidhani kama inalipa kuendelea kuhangaika na huyu Sitta maana ni mtu anayedhani kuwa ana nafasi ya kupata madaraka makubwa ndani ya CCM kupitia mtandao aliopo ndani ya chama hicho, ikibidi urais, hivyo hawezi kufikiria kuja CDM, labda itokee kuwa kabanana sana na hana jinsi.Sitta ni mtu mzima, huu ushauri wala hakustahili kupewa bali angekuwa ameshachukua hatua siku nyingi sana hata kabla wadau hamjaanza kumfikiria na kumshauri kama kweli ni alikuwa mpiganaji wa kweli, huyu naye ni opportunists kama walivyo wengine wengi ndani ya CCM, Mwakyembe, Magufuli, Tibaijuka, n.k. , just few to mention!Wadau naomba msisahau jinsi huyu mzee alivyomkejeri Dr. Slaa wakati wa kampeni kuwa JK sio saizi yake bali yeye (Sitta). Pamoja na kejeri hiyo ya kijinga, lakini bado Slaa alimpa ushauri wa kutokuukubali uteuzi aliopewa wa uwaziri wa EA. Sasa kama kakataa kupokea ushauri wa mtu makini kama Dr. Slaa, je atapokea huu ushauri wenu? Tusubiri kwanza ajeruhiwe halafu atatia akili!N.B: Kama kweli Sitta ni mpiganaji, kwa nini baada ya kutishiwa kunyang'anywa uanachama wa CCM wakati anasimamia mjadala wa Richmond, aliamua kufunika kombe ili kuwanusuru mafisadi na chama chake akidai kuwa maazimio yote 23 ya kamati teule ya Bunge yameshatekelezwa na serikali?

Ndugu, hayo ni mapungufu madogo sana ambayo kila mtu anaweza kuwa nayo, tunachoangalia hapa ni dhamira na nia yake ya moyoni juu ya watanzania. Mi naamini kuwa huyu ni mpiganaji, na itakapofikia muda wa yeye kung'atuka basi atang'atuka, anachohitaji zaidi ni uhakika tu. Kingine mwanafunzi wakati mwingine hawezi kujifunza bila viboko hata kama utatumia lugha inayoeleweka na kila mtu, kuna mahala lazima achapwe tu. Vitendo vibaya vitakavyompata Sitta kutoka kwa ccm vitamfunza zaidi na Hii ndiyo sababu ya kusema kuwa Hatima yake ipo Chadema.
 
Tatizo letu ni umasikini.............sitta hawezi kuhama ccm kwani anafikiria zaidi marupurupu anayoyapata iwapo akiikacha ccm........kwa hiyo watz wengi tu tunajua hata haki zetu lakini hatutaki kudai kwa kuhofia wakubwa na kuhofia kibarua kuota nyasi na familia yako kuhangaika.................sitta hajafikiria uzalendo wa kuamua kuacha mapochopocho ya ubunge na kuisaliti ccm............."msimamo wa siitta ni kuwa< mwanaume hakimbii mwanaume ananpigana hadi mwisho"
 
Nataka kwa idhini yako nitafute mail yake niifowadi kwake au niombe gazeti lolote waichapishe! asante
 
Nataka kwa idhini yako nitafute mail yake niifowadi kwake au niombe gazeti lolote waichapishe! asante

Powa, it's okay kabisa tena itakuwa saaafi, you do have positive permission. Do as you wish.
 
Kusaliti wenzio ndiyo kutafuta haki, nadhani mara mbili inatosha huyu ni wa kustaafu tu siasa!

Inategemea umemsaliti vipi,katika mazingara yapi na katika malengo yapi

Maharamia wakisalitiana,akajitokeza ambaye anachukia uharamia bado itakuwa vibaya?Sioni ambacho sitta amefanya kuitwa msaliti.Yupo Sahihi kabisa
 
Natumai mzee Sitta anatafakari nini cha kufanya baada ya kuporomoka kisiasa huku akiwa hana uhakika wa kushine katika chama.Tusubiri tuone kama anaweza kuchukua maamuzi magumu ya kuhamia chama kingine na kuendeleza mapambano.
 
CHADEMA ndiko nyumbani kwa wapambanaji wa Kweli.Si kwa Sitta tu na hata kwa watu wasafi kwenye vyama vingine.Mwenye hulka ya Kifisadi hawezi kukaa ndani ya CHADEMA kwa Raha.Hiyo ndiyo Reality

Chadema ipi? Hii iliyoingiliwa na mafisadi au nyingine? Msitubabaishe hapa, the difference is the same!
 
Chadema ipi? Hii iliyoingiliwa na mafisadi au nyingine? Msitubabaishe hapa, the difference is the same!

It appears you cannot read.What is wrong with having 'newer' politicians that are in touch with today's world other than these very old people In your party stuck in the '60's.

Stop raising your adrenaline,your too Emotional for God's sake.
 
MZEE SITTA,kweli ni mpambanaji na hilo halina ubishi.ila kuja au kutokuja cdm ni uamuzi wake binafsi anàopasw kuufànya bila kulazimishwa,ni suala la kusoma alama za nyakati tu
 
Naamini Sita ni Mpambanaji, lakini pia kama ni mtu safi hataogopa katu kuachana na CCM lakini kama ana madudu ambayo yamesikika pia! anaogopa watamchafua, ila sio vibaya kutubu pale ulipojikwaa na kuendeleza mazuri yaliyopo, karibu Chadema mkuu Samweli Sitta.
 
Mbogo,

Ni kweli kabisa mkuuu
 
Karibu 6 uwe chachu ya mageuzi, ila utuletee mbinu za kuiba kura maana kwa wizi CCM hawajambo.
 
Back
Top Bottom