Samuel Sitta awapa somo Kagame (Rwanda), Museveni (Uganda)

Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !
unaohiajika
hiyo mbona inaeleweka ni kweli kwamba hakuna ugomvi kati ya tz na rwanda ila ni kutokuelewana kwa wanasiasa wakuu wa nchi mbili hizi........................................that is too obvious mkuu sita hajatofautiana na bosi wake hapo ni uelewa tu
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ugomvi wa wanasiasa katika jumuia hiyo hauwezi kuathiri shughuli za kibiashara na uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wanaangalia faida zaidi katika shughuli zao.

Sitta alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua athari za kiuchumi zitakazopatikana baada ya kuwapo kwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kutaka kupitisha mizigo yao katika bandari ya Mombasa badala ya ile ya Dar es Salaam.

Alisema kuwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kuazimia kutumia bandari ya Mombasa si za ukweli na kwamba wanaofanya hivyo ni wale waliokosa zabuni mbalimbali ambazo pia hakuzitaja ni zabuni ya nini.

“Mimi ninachojua suala la hapa ni uchumi. Huu ugomvi wa wanasiasa wawili hauwezi kuwakimbiza wafanyabiashara na ukiangalia wanaopitisha mizigo ni wafanyabiashara na si serikali zinazolumbana,” alisema.

Aliongeza kuwa migongano baina ya nchi na nchi haiepukiki hususan zilizo jirani na kuita hali hiyo ya mpito huku akisisitiza kuwa maelewano baina ya Tanzania na Rwanda yatarejea muda si mrefu.

Waziri Sitta alisema umbali kati ya Mombasa na Kigali ni kilometa 2300 na kutoka Dar es Salaam hadi Kigali ni kilometa 1400, suala alilodai wafanyabiashara wataangalia umbali katika kutafuta faida ya kazi wanazozifanya.

Alieleza kuwa mkakati mwingine wa kuwafanya wafanyabishara wazidi kuitumia bandari ya Dar es Salaam ni kupunguza vizuizi vya njiani kutoka 15 vya sasa hadi vitatu.

Alisema kuwa na vizingiti vingi barabarani ni tatizo huku akiwashangaa askari wanaosimamisha magari yenye lakiri ambazo hawawezi kuzifungua na kueleza hali hiyo ni kero kwa madereva na wafanyabiashara.

Juzi, msemaji wa Chama cha mizigo nchini (Tatoa) Elias Lukumay, aliiambia kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi za Rwanda na Uganda zimekubaliana kutumia bandari ya Mombasa kutokana na urasimu unaodaiwa kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.

Alisema nchi hizo zimekubaliana kuanza kutumia bandari ya Mombasa kuanzia Septemba mwaka huu.

Uamuzi huo wa Rwanda na Uganda unatafsiriwa kuwa unatokana na msigano wa kisiasa ulioibuka hivi karibuni baina ya Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda baada ya ushauri wake wa kumtaka Kagame akutane na waasi kwa ajili ya kujadili amani ya taifa lao

SITA kachemka. Halafu kwa nini yeye kama waziri wa kikwete anajitenga na bosi wake zaidi pale anaposema kuwa ni ugomvi wa watu wawili akimaanisha kagame na Kikwete. Kwa nini anazidiwa na yule mama Mushukiwabo wa Rwanda anayeonesha wazi kukaa upande wa bosi wake Kagame. Nina mashaka sana na MH. Sita. Sijui huyu Sita akifika Kampala huwa anajiita MSIX kama ilivyo kwa bwana M7. Na kimsingi mh. Kikwete hana ugomvi na kagame. Kagame ndiye anayeigombeza tz na rais wake kwa sababu ambazo hataki kuziweka wazi. Mheshimiwa Kikwete, sisi tuko nyuma yako hata kwa kumtafuat PK hata kwa kumfichua kuytoka kwenye bomba la maji taka.
 
unaohiajika
hiyo mbona inaeleweka ni kweli kwamba hakuna ugomvi kati ya tz na rwanda ila ni kutokuelewana kwa wanasiasa wakuu wa nchi mbili hizi........................................that is too obvious mkuu sita hajatofautiana na bosi wake hapo ni uelewa tu

Acha ushamba. Kutoelewana kati ya marais wawili maana yake ni kuwa hizo serikali mbili hazielewani. Marais wawili wakigombana huwa hawarushiani ngumi na mateke bali huamuru majeshi ya nchi hizo na kuanza kupigana, yaani huo ni ugomvi wa nchi na nchi. Kikwete anapoitwa rais anakuwa anawakilisha nchi na wananchi wake na siyo familia yake tu na hivyo huongea kwa niaba yetu. kwa hiyo hata ushauri alioutoa kule addis alifanya hivyo kwa niaba ya serikali anayoingoza na watu wake.
 
Mh sita na kagame ni mtu na kaka ake so hawezi kumuudhi ndugu yake hata ck moja,,,,,,atakosa hifadhi 2015 ,,,,wkt chadema inachukua nchi
 
Jk alisema "husiano baina ya tz na rwnd unapitia kipindi kigumu........."
"Viongozi wa Rwanda wamekua wakitoa maneno ya kashfa dhidi yangu............"
"Maneno tunayoyasikia hatutaki kuyaamini lakini pia hatuta yapuuza"
"Tunaamini mambo haya yataisha kwa njia za kidiplomasia"
Na majuzi pm kasema wanaomba mu7 awemsuluhishi tena katamka bungeni

Naomba nipewe tafsida halisi kinaga ubaga ni nini walakini ambao haushabihiani kati ya tamko hizi kimantiki kati ya Jk, Pinda na Sitta?
 
Acha ushamba. Kutoelewana kati ya marais wawili maana yake ni kuwa hizo serikali mbili hazielewani. Marais wawili wakigombana huwa hawarushiani ngumi na mateke bali huamuru majeshi ya nchi hizo na kuanza kupigana, yaani huo ni ugomvi wa nchi na nchi. Kikwete anapoitwa rais anakuwa anawakilisha nchi na wananchi wake na siyo familia yake tu na hivyo huongea kwa niaba yetu. kwa hiyo hata ushauri alioutoa kule addis alifanya hivyo kwa niaba ya serikali anayoingoza na watu wake.
ucnilazimishe nikubali unachoamini wewe, acha niwe mshamba kuliko kuwa mjumbe ndiyo ..............hayo ni maelezo kwa mujibu wa uelewa wako.........natambua positions za marais na flags wanazobeba so nilichoandika nakielewa na nakiamini upo hapo
 
Kielewe kwa kutumia mawazo yako na siyo kwa hisia ya moyo wako.
 
yeye ni mwasheria na mwanasiasa asiyachanganye mambo hayo na biashara.
 
Kagame huwa haangalii mbali ili swala asipoangalia litapandisha mfumuko wa bei nchini mwake
 
Kwisha kagame....frm 15 road barriers to 3 road barriers!!!!.ama kweli watz tunajua fitina
Hapo ni kama tumemtengenezea mgogoro mpya kati yake na wafanyabiashara wa rwanda ambao kama sikosei ndo walipa kodi.na hata hivyo vitatu navyo viondelewe kabisa ili pk apate kiwewe zaidi.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ugomvi wa wanasiasa katika jumuia hiyo hauwezi kuathiri shughuli za kibiashara na uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wanaangalia faida zaidi katika shughuli zao.

Sitta alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua athari za kiuchumi zitakazopatikana baada ya kuwapo kwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kutaka kupitisha mizigo yao katika bandari ya Mombasa badala ya ile ya Dar es Salaam.

Alisema kuwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kuazimia kutumia bandari ya Mombasa si za ukweli na kwamba wanaofanya hivyo ni wale waliokosa zabuni mbalimbali ambazo pia hakuzitaja ni zabuni ya nini.

“Mimi ninachojua suala la hapa ni uchumi. Huu ugomvi wa wanasiasa wawili hauwezi kuwakimbiza wafanyabiashara na ukiangalia wanaopitisha mizigo ni wafanyabiashara na si serikali zinazolumbana,” alisema.

Aliongeza kuwa migongano baina ya nchi na nchi haiepukiki hususan zilizo jirani na kuita hali hiyo ya mpito huku akisisitiza kuwa maelewano baina ya Tanzania na Rwanda yatarejea muda si mrefu.

Waziri Sitta alisema umbali kati ya Mombasa na Kigali ni kilometa 2300 na kutoka Dar es Salaam hadi Kigali ni kilometa 1400, suala alilodai wafanyabiashara wataangalia umbali katika kutafuta faida ya kazi wanazozifanya.

Alieleza kuwa mkakati mwingine wa kuwafanya wafanyabishara wazidi kuitumia bandari ya Dar es Salaam ni kupunguza vizuizi vya njiani kutoka 15 vya sasa hadi vitatu.

Alisema kuwa na vizingiti vingi barabarani ni tatizo huku akiwashangaa askari wanaosimamisha magari yenye lakiri ambazo hawawezi kuzifungua na kueleza hali hiyo ni kero kwa madereva na wafanyabiashara.

Juzi, msemaji wa Chama cha mizigo nchini (Tatoa) Elias Lukumay, aliiambia kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi za Rwanda na Uganda zimekubaliana kutumia bandari ya Mombasa kutokana na urasimu unaodaiwa kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.

Alisema nchi hizo zimekubaliana kuanza kutumia bandari ya Mombasa kuanzia Septemba mwaka huu.

Uamuzi huo wa Rwanda na Uganda unatafsiriwa kuwa unatokana na msigano wa kisiasa ulioibuka hivi karibuni baina ya Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda baada ya ushauri wake wa kumtaka Kagame akutane na waasi kwa ajili ya kujadili amani ya taifa lao

Msuguano wa kisiasa hauwezi kuathiri shughuli za EAC - anatoa statement kama hii ni mvivu wa kusoma historia au ana matatizo ya memory. Mimi nilisoma kuwa moja ya sababu za kuvunjika kwa EAC 1 ni migongano ya kisiasa hasa kati ya marehemu Idd Amin na Nyerere kwani walifikia kutokuonana kabisa hivyo vikao vikawa vigumu; sasa leo mwingine anasema haiwezekani, simwelewi. Hay angalia mpango wa watatu kuimalirisha bandari ya Mombasa, haya kuongeza kodi kwa malori ya Tanzania, bado mtu anasema hamna hathari kweli hapo?!
 
Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !

Haha.....haya ni mamabo ma CCM hawawezi yaona.Wao watakuwa busy kumpa pongezi kwa vile hawala bigger picture. Mwingine atakataa,mwingine atakubali kwa kujijua au kutojijua, na mwingine atawapiga wote.Halafu watasema CCM sasa ni moja kuliko ktk kipindi chochote cha historia yake.Huku sifa akipewa JK kwa pamoja na Mungu(Km wapo sawa vile) kwa uongozi shupazi.
 
Jambo lamuhimi ili wafanya biashara wazidi kuitumia bandari ta DAR ni kufanya marekebisho na kuwaondoa walafi wote. Wafanya biashara wengi wanalalamika kuhusu mizigo yao na containers zao, bandari zingine Pia zijengwe ili kurahisisha utoleaji wa mzigo. Hapo kutakua hakuna tena mzizi wa fitna. Na ushuru wa bidhaa iwekwe waazi kwa mfano ushuru wa elekronics ijulikane, nguo ijulikane ili iwe rahisi kwa mfanya biashara. Leo Hii unaambia mzigo ukija ndio tutakadiria, huo ni chanzo cha uwizi
 
Ina maana Sitta hafahamu kuwa hawa wanasiasa wawili ndio nchi zenyewe?
Anaongea kama vile anamaanisha Mwenyekiti wa kijiji huko Malampaka ya hapa Tanzania anagombana na Mwenyekiti wa kijiji huko Rutiringarire nchini Rwanda
 
Back
Top Bottom