Samuel Sitta awapa somo Kagame (Rwanda), Museveni (Uganda)

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ugomvi wa wanasiasa katika jumuia hiyo hauwezi kuathiri shughuli za kibiashara na uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wanaangalia faida zaidi katika shughuli zao.

Sitta alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua athari za kiuchumi zitakazopatikana baada ya kuwapo kwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kutaka kupitisha mizigo yao katika bandari ya Mombasa badala ya ile ya Dar es Salaam.

Alisema kuwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kuazimia kutumia bandari ya Mombasa si za ukweli na kwamba wanaofanya hivyo ni wale waliokosa zabuni mbalimbali ambazo pia hakuzitaja ni zabuni ya nini.

"Mimi ninachojua suala la hapa ni uchumi. Huu ugomvi wa wanasiasa wawili hauwezi kuwakimbiza wafanyabiashara na ukiangalia wanaopitisha mizigo ni wafanyabiashara na si serikali zinazolumbana," alisema.

Aliongeza kuwa migongano baina ya nchi na nchi haiepukiki hususan zilizo jirani na kuita hali hiyo ya mpito huku akisisitiza kuwa maelewano baina ya Tanzania na Rwanda yatarejea muda si mrefu.

Waziri Sitta alisema umbali kati ya Mombasa na Kigali ni kilometa 2300 na kutoka Dar es Salaam hadi Kigali ni kilometa 1400, suala alilodai wafanyabiashara wataangalia umbali katika kutafuta faida ya kazi wanazozifanya.

Alieleza kuwa mkakati mwingine wa kuwafanya wafanyabishara wazidi kuitumia bandari ya Dar es Salaam ni kupunguza vizuizi vya njiani kutoka 15 vya sasa hadi vitatu.

Alisema kuwa na vizingiti vingi barabarani ni tatizo huku akiwashangaa askari wanaosimamisha magari yenye lakiri ambazo hawawezi kuzifungua na kueleza hali hiyo ni kero kwa madereva na wafanyabiashara.

Juzi, msemaji wa Chama cha mizigo nchini (Tatoa) Elias Lukumay, aliiambia kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi za Rwanda na Uganda zimekubaliana kutumia bandari ya Mombasa kutokana na urasimu unaodaiwa kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.

Alisema nchi hizo zimekubaliana kuanza kutumia bandari ya Mombasa kuanzia Septemba mwaka huu.

Uamuzi huo wa Rwanda na Uganda unatafsiriwa kuwa unatokana na msigano wa kisiasa ulioibuka hivi karibuni baina ya Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda baada ya ushauri wake wa kumtaka Kagame akutane na waasi kwa ajili ya kujadili amani ya taifa lao
 
Well said sitta

mmh.....sitta alifaa abaki tu kwenye u-spika huku kapotea kabisa....serikali ina say kubwa kwa wafanyabiashara wake kuhusu wapi watrade na wapi wasi-trade....mfano hai kuna mfanyabiashara wa mchele alikuwa akinunua maeneo ya shinyanga na mwanza kipindi cha nyuma....guesss what mara ya mwisho kupigiwa simu alisema hatoweza kuendelea na hiyo business kwa sasa kwa sababu ya hali ya kisiasa kati ya tZ na RW,"hali ikikaa vizuri tutaendelea" (Kayumba)...alafu umbali si issue sana kama ukiritimba na rushwa za hapa zinapelekea gharama kuongezeka hata zaidi ya gharama za umbali wa km 1000....jua gharama za umbali zinajulikana kabla predetermined ila rushwa na ukiritimba mwingine haupo predetermined .....they will definitely choose the best option....nakubali ushauri alotoa....zile nyingine zilikuwa longo longo tu.....
 
Well done mr s.sitta tunapenda sana siasa zako za kujenga na sio blah blah zinazojenga chuki,In reality we need rwanda,burundi and uganda for the growth of our economy
 
Hapa inaonekana,hata sita mwenyewe yupo,upande wa kagame.mbona kipindi hiki haja fwatuka,namaneno yake kama anapo washambulia wabunge,waviti maalum,napia kama waziri wadhamana haja wauliza wenzake mawaziri,hivyo vikao vyao vya nchi tatu badala ya nchi tano maana yake nini?east afrika ya sasa niunafiki.
 
Well said sitta

mmh.....sitta alifaa abaki tu kwenye u-spika huku kapotea kabisa....serikali ina say kubwa kwa wafanyabiashara wake kuhusu wapi watrade na wapi wasi-trade....mfano hai kuna mfanyabiashara wa mchele alikuwa akinunua maeneo ya shinyanga na mwanza kipindi cha nyuma....guesss what mara ya mwisho kupigiwa simu alisema hatoweza kuendelea na hiyo business kwa sasa kwa sababu ya hali ya kisiasa kati ya tZ na RW,"hali ikikaa vizuri tutaendelea" (Kayumba)...alafu umbali si issue sana kama ukiritimba na rushwa za hapa zinapelekea gharama kuongezeka hata zaidi ya gharama za umbali wa km 1000....jua gharama za umbali zinajulikana kabla predetermined ila rushwa na ukiritimba mwingine haupo predetermined .....they will definitely choose the best option....nakubali ushauri alotoa....zile nyingine zilikuwa longo longo tu.....
 
Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !

Ben unashangaa nini tena na wewe? Hawa watu sasa hivi ni shagalabagala, hakuna uongozi wa pamoja ndani ya serikali. Kila mtu anatoa tamko lake kama alivyofikiri usiku akiwa na wife kisha linakuwa la serikali.
Mwisho wa siku jambo moja Rais kalisemea vile,waziri vile,Nape kivyake na hata watendaji wengine vyao. Utadhani tafrija yenye pombe nyingi kuliko waalikwa.
 
Well done mr s.sitta tunapenda sana siasa zako za kujenga na sio blah blah zinazojenga chuki,In reality we need rwanda,burundi and uganda for the growth of our economy
Burundi hawana tatizo kwani kikao walikaa Marais watatu ni kweli mombasa ni mbali sana lakini Mombasa hawana usumbufu bandarini kama Dsm na pengine gharama za usumbufu ni kubwa kuliko umbali toka mombasa hadi Uganda na Rwanda ikumbukwe pia wakati mwingine mizigo ya Rwanda hupita Sirari Tarime hadi kagera na kuingia Rwanda je?wakiamua kuhama Dsm kwenda mombasa hawatapitia Tanzania?
 
Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !

Mkuu Ben Saanane huu ndio udhaifu mkubwa wa serikali iliyoko madarakani,kila kiongozi anaongea lake!!!
 
Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !
hapa sitta kaongea in context, kwamba hata kama kunakuwepo na tofauti kati ya watu wawili, basi hiyo effect kama una akili haita wasumbua watu wengine, mfano mkeo agombane na jirani, au wanawake wapishane, na labda mkeo ni mkorofi au huyo wa jirani ndio mkorofi, sasa wewe na akili zako utagombana na Mumewe? au na huyo Mwanamke kama Mkeo ndio aliye kosea au nduguyo ndiye aliye kosea.
 
Ben unashangaa nini tena na wewe? Hawa watu sasa hivi ni shagalabagala, hakuna uongozi wa pamoja ndani ya serikali. Kila mtu anatoa tamko lake kama alivyofikiri usiku akiwa na wife kisha linakuwa la serikali.
Mwisho wa siku jambo moja Rais kalisemea vile,waziri vile,Nape kivyake na hata watendaji wengine vyao. Utadhani tafrija yenye pombe nyingi kuliko waalikwa.

Hahahah!! Hii nimeipenda. "Utadhani tafrija yenye pombe nyingi kuliko waalikwa"
 
Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !
Na wewe unakuwa kama mtoto ambaye hajasoma wapi sitta kamtaja jk na kagame? Yeye kasema wanasiasa wawili wewe unajuaje kuwa ni jk na kagame kama siyo umbea,kwa nini isiwe slaa na jk au kagame na slaa au kenyatha na jk au vinginevyo acha kuwekea maneno watu mdomoni.
 
Ben unashangaa nini tena na wewe? Hawa watu sasa hivi ni shagalabagala, hakuna uongozi wa pamoja ndani ya serikali. Kila mtu anatoa tamko lake kama alivyofikiri usiku akiwa na wife kisha linakuwa la serikali.
Mwisho wa siku jambo moja Rais kalisemea vile,waziri vile,Nape kivyake na hata watendaji wengine vyao. Utadhani tafrija yenye pombe nyingi kuliko waalikwa.

Umenivunja mbavu.Damn!
 
Na wewe unakuwa kama mtoto ambaye hajasoma wapi sitta kamtaja jk na kagame? Yeye kasema wanasiasa wawili wewe unajuaje kuwa ni jk na kagame kama siyo umbea,kwa nini isiwe slaa na jk au kagame na slaa au kenyatha na jk au vinginevyo acha kuwekea maneno watu mdomoni.

Umesoma habari yote na kuielewa?
 
Hili swala la huu mgogoro wa kidiplomasia kati ya Rwanda Tanzania binafsi limenichosha! Ukweli huu mgogoro Upo ata Kama wanasiasa wapishane kikauli, lakini ukweli utabaki palepale hili tatizo lipo! Tutumie busara Sisi watanzania katika hili swala! Tuwaache hao waganda na Rwanda waendelee na mambo Yao! Tanzania bila hao wapenda vita kamwe haiwezi kutetereka! Ila chondechonde wanasiasa msituingize vitani!
 
Na wewe unakuwa kama mtoto ambaye hajasoma wapi sitta kamtaja jk na kagame? Yeye kasema wanasiasa wawili wewe unajuaje kuwa ni jk na kagame kama siyo umbea,kwa nini isiwe slaa na jk au kagame na slaa au kenyatha na jk au vinginevyo acha kuwekea maneno watu mdomoni.
ndugu how old are you?
 
Back
Top Bottom