Samuel Sitta amekwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu ya miguu

Rebo Tz

Senior Member
Sep 26, 2016
169
124
Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta amekwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu ya miguu.

Mwanawe, Benjamin Sitta amesema: “Anachoumwa ni miguu. Baba yupo katika hali nzuri, yupo salama tu, achaneni na taarifa za mitandao.” Alikuwa akirejea taarifa zilizoenea kwenye mitandao kwamba baba yake yu mahututi.

Septemba 19, Rais John Magufuli alimtembelea Sitta nyumbani kwake ambako alimueleza kuwa hali yake inaendelea vizuri. Taarifa ya Ikulu ilieleza mwanasiasa huyo mkongwe alikuwa jijini kwa ajili ya matibabu bila kueleza ugonjwa unaomsumbua.

Siku moja baada ya Rais kumtembelea, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye alikwenda kumjulia hali. Vivyo hivyo, Septemba 21 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alimtembelea Sitta alipokuwa amelazwa katika hospitali moja jijini hapa.

Sitta ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba na waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti, ni miongoni mwa wanachama zaidi ya 40 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana.

Hata hivyo, baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kumuondoa, alitangaza kustaafu masuala ya siasa.
 
Kweli shati zuri jeupe kiboko yake doa dogo sana. jinsi Sita alivyoendesha bunge watu wengi tulimpenda na hasa alivyowalea kwa kuwapa nafasi wapinzan ktk bunge la spid na viwango, this was 6 i knew. lkn alichokifanya kwny katiba yetu na amin hata yeye huko aliko anajutia sbb ukwel hata mtoto mdogo aliuona alivyosimamia shoo kwa namna ya kipekee. nakuombea upone haraka na uwe na maisha marefu.
 
Tumuombee Mungu ampe nafuu ya haraka arudi kuwa na familia yake.

Mwanadamu si mkamilifu hufanya makosa.

Hata Mwl Nyerere alikiri ktk utawala wake kuna makosa aliyafanya.
 
Back
Top Bottom