Samsung wazitangaza rasmi simu za Galaxy S7

Samsung wazitangaza rasmi simu za Galaxy S7

iphone 18 promax

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2012
Posts
2,918
Reaction score
2,153
Samsung wameshatoa mzigo wa sumsung galaxy s7 mzigo hatari na matata kabisa huku ukiwa na battery la 3000mah.
======

S7.jpg

Kampuni ya Samsung imezitangaza rasmi simu za Galaxy S7 na S7 edge kwenye tukio la tamasha a simu liliofanyika mjini Barcelona nchini Hispania ambapo mwanzishi wa Facebook, Mark Zuckernberk alishitukiza wahudhuriaji kwa kutokea bila kutarajiwa na kuongelea ushikiano na Samsung katika baadhi ya technolojia.

Kama ilivyo ada toleo jipya huja na maboresho kulingana na tokeo la nyuma yake na Samsung wameweza kufanya kweli kwenye simu zao mpya hasa ukiinganisha na mshindani wake mkuu kwa sasa Apple ambae anatoa simu za iPhone.

Kutoingia Maji: Samsung wamesema Galaxy S7 haiingizi maji kwa kiwango cha IP68 ambapo maji wala vumbi hayaingii ikimaanisha inaweza kwenda chini ya maji zaidi ya mita moja na kukaa humo kwa angalau nusu saa bila kudhurika.

Unaweza kuongeza uhifadhi kumbukumbu wa simu mpaka GB 200 na inawekwa kwenye trey inayowekwa kadi ya simu.

Betri kubwa: Galaxy S7 ikiwa na betri ya 3,000 mAh na edge ikipachikwa betri ya 3,600 mAh wakimuacha iPhone akiwa na betri zake za 1,715 na 2,750 mAh kwa simu zake hivyo kuwa na uwezekano wa kukaa zaidi.

Pamoja na hayo pia samsung wameweka kamera ambayo inaweza kulinda ubora wa picha zinazopigwa kwenye mwanga hafifu.

Pamoja na mazuri yake mengi yaliyoongezwa kwenye uwezo wa simu lakini samsung wamebaki na muundo unaofanana sana na wa kale kitu ambacho kinaweza kisiwasisimue sana wateja wanaojali matoleo kwa kuangalia.
 
Nahisi march 11 itakuwa released.... Hiyo kama sikosei ni announced....
 
Samsung hawana jipya,mambo mengi wanayotoa alishatoa sony tangu tangu 2012,duniani kuna simu mbili tu nazo ni sony na nokia(r.i.p),na nokia wanarudi this year,nashangaa watu wanapenda umbo jipya kila toleo,s3 na s5 utadhan n manufacturer tofauti,hii ni dalili kuwa bado hawajakomaa,thats why ni rahisi kupata simu china kwa bei lakin zenye mwonekano sawa na samsung,kupata copy/fake ya sony z5 premium au nokia pure view ni ndoto
 
juzi kidogo nishikishwee sony clone
 
Back
Top Bottom