Samsung galaxy s5 vs tecno camon c9

mah si kigezo cha ukaaji chaji pekee, simu kama xperia z3 compact inapita almost michina yote yenye 5000mah japo yenyewe ina 2600mah tu.
A9-4000mah
j7 na c7 3300mah
s6 active ni 3500mah
mAh sio kigezo?! Kuwa objective na sio subjective. Kupenda brand fulani si kwamba hata penye ukweli uwe uongo. Si kila brand kubwa lazima iwe na quality ya kutisha sana. Techno hata watengeneze simu ya kiwango kuzidi sumsung interms of quality bando sokoni sumsung brand sokoni itakuwa juu.
 
mkuu unaposema mah ni kama kwenye gari unazungumzia tank la mafuta, inategemea na engine (soc) inakunywa vipi hayo mafuta.

kuna magari yana matank makubwa ya mafuta ila yanakula sana mafuta wakati magari mengine matank yao ni madogo lakini hayanywi sana mafuta.

mah si kigezo pekee cha simu kukaa na chaji,
-display inapozidi kuwa na resolution kubwa na nzuri ndio jinsi inavyokula chaji
-soc au processor inaplay role kubwa kwenye ukaaji chaji, simu yenye snapdragon 625 (soc inayoongoza kutunza chaji kwa sasa) huwezi ilinganisha na simu ya mediatek helio x20
-optimization ya manufacture, simu zote kampuni kubwa wana optimization nzuri na wanajua jinsi ya kudesign na kupangilia simu compare na makampuni madogo.

tuje mifano halisi hasa hapo kwenye soc natumia simu mbili hapa
- motorola moto z play yenye snapdragon 625 na battery ya 3500mah
-xiaomi redmi note 4 yenye mediatek helio x20 na battery ya 4000mah

kwa logic yako ungesema redmi note 4 ni kali sababu ina 4000mah ila huu ndio ukaaji chaji




ukiangalia hapo simu yenye 3500mah imeipita kila idara simu yenye 4000mah tena test nyengine kama ya video moto z ina masaa 18 wakati redmi note 4 ni masaa 9 tu,

sasa 4000mah unaangalia masaa 9 na 3500mah unaangalia masaa 18 bado unataka uniaminishe kuwa mah kubwa ni bora zaidi bila kuangalia soc husika?
 
Nina Sony Xperia S. MAH 1800 inakaa na chaji mpaka naichukia. Naingia social networks frequently lakin huwa naichaji hata mara 1 ndani ya saa 48
 
Mkuu chief mkwawa nataka nichukue samsung galaxy A8 2016 vipi ni nzuri?
 
Mkuu chief mkwawa nataka nichukue samsung galaxy A8 2016 vipi ni nzuri?
yap ni nzuri, ni almost kama galaxy note 5, hivyo itategemea na bei na unachotaka kuitumia, pia hakikisha ina band 800 maana zipo ambazo hazina.
 
yap ni nzuri, ni almost kama galaxy note 5, hivyo itategemea na bei na unachotaka kuitumia, pia hakikisha ina band 800 maana zipo ambazo hazina.
Ahaa, je kati ya hiyo na samsung galaxy s7 edge nichukue ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…