Samson Mwigamba: Hatutakusahau Mizengo Kayanza Peter Pinda
HUKO nyuma niliwahi kusema na leo narudia kusema kwamba katika historia ya nchi hii wamepita mawaziri wakuu wengi, lakini hajawahi kutokea waziri mkuu wa aina ya Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Nimewahi kwa mfano kusema ukifuatilia sana majibu yake, hasa kwa maswali ya papo kwa papo bungeni, ukifuatilia hotuba zake, hakuna kitu anasema kwa uhakika kwamba "mimi kama waziri mkuu naagiza hiki ama kile, natamka hivi ama vile".
Niliwahi kutoa mfano siku moja akiwa ziarani, nadhani ni Mtwara ama mkoa mmojawapo wa kusini mwa nchi. Akakutana na sakata la Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ambaye ametaifisha mradi wa maji wa wananchi badala yake anachota maji na kuwauzia wananchi wale wale.
Baada ya maelezo ya wananchi na majibu ya ubabaishaji ya mtendaji huyo wa halmashauri, nikiwa namshuhudia kwa macho na masikio yangu kupitia luninga, Pinda akasema: "Mkurugenzi fika mahali uwahurumie wananchi hawa maskini."
Nilishangazwa na kauli ile ya Waziri Mkuu kwa mkurugenzi mhuni ambaye amezuia mradi wa maji wa wananchi uliohudumiwa kwa pesa za walipa kodi, halafu yeye kwa makusudi akakataa kuufungua mradi ule badala yake anachota yale maji na kubeba kwenye lori na kwenda kuwauzia wananchi wale wale. Kauli ya bosi wake sitaisahau maisha yangu yote.
Pinda akiulizwa swali anasema; "mimi nafikiri…, mimi nadhani…, tufike mahali…, ngoja tujaribu kuona…, mimi ningedhani…". Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ambaye muda wote anadhani, anafikiri, anajaribu kuona, nk, atatufikisha wapi?
Amekuwa waziri mkuu toka 2008, lakini hakuna kitu kikubwa kilichotokana na ubunifu na ushupavu na uchapakazi wa waziri mkuu. Hakuna tamko zito alilowahi kutoa wananchi wakasema tuna waziri mkuu.
Fredrick Sumaye aliwahi kutamka; "kama kuna mwenye daladala asiyependa kubeba wanafunzi kwenye daladala yake, hiyo daladala aiegeshe nyumbani asiiweke barabarani." Hata kauli fupi hiyo, lakini yenye kuonesha mamlaka haijawahi kutolewa na Waziri Mkuu Pinda.
Majanga mengi yametokea wakati wake kuliko hata wakati wa Edward Sokoine, hali ya nchi imeharibika kuliko hata wakati mawaziri wakuu wote waliopita, lakini waziri mkuu wetu kama vile hayupo. Mambo ya Pinda ni mengi mno! Lakini nikumbushe jambo moja la hivi karibuni ambalo limenikumbusha mbali hadi nikaamua kuandika tena leo juu yake.
Pinda alikuwepo bungeni kwenye mkutano wa Bunge ulioisha Februari 8 mwaka huu. Pale kuliletwa hoja binafsi zipatazo mbili ambazo ziligusa moja kwa moja suala la elimu ya vijana wetu kwenye ngazi ya msingi, sekondari na sekondari ya juu.
Hoja ya kwanza ilikuwa ni ya James Mbatia (NCCR-Mageuzi) iliyoainisha upungufu kibao kwenye mfumo wa elimu.
Mbatia alikuwa wazi, kwani hoja yake binafsi alitamka wazi kwamba ni juu ya udhaifu kwenye mfumo wa elimu ya Tanzania. Hoja yake ingekubaliwa, Bunge lingeunda kamati teule ambayo ingekwenda kuhoji serikali, hasa viongozi na watendaji wa Wizara ya Elimu, ingehoji mamlaka za elimu (kama Taasisi ya Elimu Tanzania, Taasisi ya Ukuzaji Mitaala, Baraza la Ithibati, nk), ingewahoji wanafunzi, ingewahoji walimu, ingehoji wachapishaji vitabu vya elimu, ingehoji kila anayeonekana kuwa ni mdau katika elimu ya Mtanzania. Ili kupata hasa chanzo cha kuporomoka kwa elimu ya Mtanzania ni nini na hatimaye waje na suluhisho.
Lakini kulikuwa na hoja ya pili ya Joshua Nassari. Hii ilikuwa ni juu ya mfumo mbaya wa utendaji na uendeshaji wa Baraza la Mitihani Tanzania na athari zake kwenye mfumo wa elimu ya Tanzania. Hii nayo ilihitaji kuundiwa kamati teule.
Kama suala lingekuwa ni gharama, mimi sidhani kama ni dhambi kukubaliana kwamba iundwe kamati moja nzito kwa maana ya kuwa na idadi ya kutosha ya wabunge wa pande zote, wenye utaalamu tofauti tofauti na wenye uzoefu na masuala haya ya elimu ya Tanzania ili ishughulikie hoja zote mbili.
Pale kwenye Baraza la Mitihani pia kuna mambo ya kufanyiwa kazi haraka, ikiwezekana hata kubadili mfumo wa mitihani yetu ama kulifumua kabisa baraza hilo na kuliunda upya.
Sikiliza kilichotokea: Hoja zote hizi pamoja na hoja nyingine kama ile ya John Mnyika zilikuwa nyeti na za maslahi makubwa kwa taifa hili. Lakini CCM wakakaa kwenye vikao vyao vya wabunge wa chama chao na kuazimia kuzipiga chini hoja zote hizo.
Naomba nikuambie msomaji wangu sababu ya kwanini CCM waliamua kuzipiga chini hoja hizi nyeti zilizoletwa na wapinzani. Sababu yao ilikuwa moja tu: Hoja hizi ni nyeti na kwa hiyo zikipita zitawapa sifa wapinzani. Basi!!!
Upuuzi huu uko katika nchi hii tu. Yaani tukatae jambo jema na nyeti lenye manufaa makubwa kwa nchi yetu, kwa sababu tu limeletwa na mpinzani wetu kisiasa na litampatia sifa kubwa kisiasa? Niliwahi kusema CCM ni chama cha uchaguzi sikueleweka, lakini naamini nitazidi kueleweka kadiri siku zinavyokwenda.
Waziri mkuu Pinda alikuwepo bungeni na kwa wasiojua, yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya wabunge wa CCM na chini ya uenyekiti wake ndipo uamuzi huo ulifanyika na kuwekewa msimamo mkali, na bungeni walikwenda kutimiza tu walichokwishaamua.
Halafu mtakumbuka niliwahi kusema mabadiliko yanayotokea sasa na yanayoijia nchi hii ni mpango wa Mungu. Hazikupita hata wiki mbili tangu wazitupe hizo hoja matokeo ya kidato cha nne yakatoka, ambapo kati ya watoto laki nne waliofanya mtihani, laki mbili na 60 wamepata daraja sifuri.
Waziri Mkuu Pinda anaunda tume ikachunguze kwanini watoto wamefeli. Tume yake haina tija maana serikali yake haiwezi kujichunguza.
Nawasihi wale ambao Pinda si bosi wao wa moja kwa moja kama Chama cha Walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu, hamna sababu ya kuhojiwa na tume yake.
Haina tija zaidi ya kuunguza pesa za walipa kodi na hakuna chochote tutakachoambulia kwenye ripoti yao. Tafakarini sana!
Source: Tanzania Daima