Belladonna Alkaloid
Member
- Dec 22, 2023
- 74
- 81
Habarini za weekend na poleni kwa mlioguswa na hukumu kwa mwenyekiti wa Chadema, ndugu Tundu Lissu.
Twende kwenye mada husika, lengo la serikali ni zuri kuhusu mpango huu wa kuongeza madaktari bingwa nchini pamoja na wabobezi katika kada nyingine lakini wanaosimamia huu mpango hapo wizara ya afya ni wazembe wasio wawajibikaji.
Tarehe 06.08.2026 lilitoka tangazo la ufadhili wa masomo kupitia mpango huu ambapo deadline ya kufanya application ilikuwa 5.09.2026 cha ajabu hadi leo yapata wiki mbili zimepita toka vyuo vifunguliwe lakini hawajatoa majina ya waliofanikiwa kupata ufadhili kupitia mpango huu. Yaani applicants maximum 1000 wanawashinda kufanya screening ndani ya miezi 2. Watumishi wengi serikalini tunategemea fursa hapa tulipo tumeshindwa kufanya usajili na dirisha la usajili katika vyuo vingi limefungwa.
Wito wangu mtoe majina ya waliopata ili waendelee na registration ili waliokosa warudi vituoni kwao ili waendelee na majukumu. Naomba waziri wa afya ndugu Mohammed Mchengerwa ufuatilia swala hili au yeyote atakaesoma ujumbe na yupo wizara ya afya na ana mamlaka ya kushughulikia swala hili afanye hivyo.
Shukrani sana nipo hapa Mwanza Buzuruga stand aliyeko karibu aje tule ugali wa udaga na nyama choma.