Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,096
- 828,932
Ndugu Watanzania!
Tuna taarifa kuwa Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. John Heche alipokwenda kuhutubia Kariakoo. Tumezungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara) Mhe Amani Golugwa alisema kuwa wamefika vituo vyote vya Polisi katika Jiji waliambiwa hayupo katika vituo hivyo.
Kwanza tunapenda kueleza kusikitshwa kwetu kwa jinsi ubaguzi na unyanyasaji unavyozidi kukua katika nchi yetu kwa sababu za kuzuia mikutano ya CHADEMA Kariakoo hazina nguvu ya kisheria na pia hazina mashiko.
Soma Pia: John Heche akamatwa na Polisi Kariakoo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwahi pia kufika kuongea na wafanyabishara Kariakoo. Je, hiyo haikuwa ni kusumbua biashara bali ilikuwa ni habari njema ya malaika Gabrieli kwa Mariamu na Elizabeti? Waziri Mkuu aliwahi kufika Kariakoo pia. Je, Polisi hiyo haikuwa ni kuleta usumbufu katika eneo la biashara, bali ilikuwa ni kama habari ya uponyaji ya malaika Rafaeli kwa Tobia?
Rais Samia aliwahi pia kufika Kariakoo. Je, hiyo haikuwa ni kuleta usumbufu kwa biashara bali ilikuwa ni habari ya baraka kwao kama taarifa ya malaika Mikaeli kwa Danieli? Je, ujumbe wa John Heche hapo Kariakoo ni ujumbe kutoka kwa Lucifer, yule malaika mkuu wa uasi?
Sisi tunaona kuwa watawala wameamua kwa makusudi kutumia Jeshi la Polisi kunyanyasa wapinzani na kuwatisha watu. Hali hii kamwe haiwezi kuruhusiwa kuendelea. Ni lazima sisi sote tuungane kuikemea na tuwaseme watu hawa bila kuwaonea aibu na bila kuwaogopa!
Leo tukifumbia macho ubaguzi na unyanyasaji huo kufanywa kwa viongozi na wanasiasa, siku nyingine utahamia katika makundi mengine na hatimaye nchi yetu itakuwa imetumbukia katika lindi la matatizo. Kama Jeshi la polisi lilikuwa na sababu ya kisheria ya kumkamata kwa nini lisimpeleke moja kwa moja kituoni badala yake hisia zinatanda kuwa wako naye kwenye gari moja wanazunguka naye?
Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kumuachia John Heche usiku huu bila masharti yeyote!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 22 Aprili 2025; saa 1:30 usiku