- Source #1
- View Source #1
kuna uvumi wa taarifa inayosambaa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan akiri kuwa amekosea . Je taarifa hii ni ya kweli ama ni uzushi?
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na Poster yenye ujumbe unaodai kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan "Nimekiri nimewakosea".
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo ama nukuu hiyo si ya kweli bali ni ya kubuni tu. Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa Taarifa hiyo haijachapishwa na chanzo chochote kila cha kuaminika.
Baadhiya watumiaji waliochapisha poster hiyo hawajaweka maelezo ya ziadia kuonesha ni lini na wapi kiongozi huyo aliyazungumza maneno hayo kwa ajili ya rejea.
Aidha poster yenye utambulisho huo imekuwa ikichapisha mara kadhaa taarifa ama nukuu ambazo si za kweli bali za kubuni kwa ajili ya kutimiza azma yao.