Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa Igunga mkoani Tabora leo, Jumatano Septemba 10, 2025, ametoa wito kwa wafugaji wa mkoa huo kupeleka mifugo yao kwenye chanjo na utambuzi ili kuiweka Tanzania katika viwango vinavyokubalika kimataifa katika soko la mifugo na bidhaa zake.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wilayani humo, katika muendelezo wa kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dk. Samia pia ameahidi kuendeleza utaratibu wa ruzuku kwa wafugaji na wakulima nchini endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena Tanzania kwa kipindi cha pili.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020/2025, Dkt. Samia amesema Serikali ya Awamu ya Sita ilitoa tani 876 za mbolea ya ruzuku kwa Wilaya ya Igunga pamoja na matrekta 38 kwa ajili ya wakulima, yaliyotolewa kwa bei nafuu kwa kila ekari ili kuongeza tija kwenye kilimo na kumuinua mkulima kiuchumi.
Aidha, ameahidi kuendelea na ujenzi wa majosho, uchimbaji wa mabwawa na utoaji wa ruzuku za chanjo za mifugo kwa wafugaji na wakulima nchini endapo atachaguliwa tena katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.