Samehe yaliyopita

  • Thread starter Prince Naahjum Alsina
  • Start date

Prince Naahjum Alsina

Prince Naahjum Alsina

Senior Member
Joined
Jun 13, 2016
Messages
138
Likes
123
Points
60
Age
28
Prince Naahjum Alsina

Prince Naahjum Alsina

Senior Member
Joined Jun 13, 2016
138 123 60
Samehe yaliyopita. Weka huru nafsi yako. Najua sasa hivi waweza kuwa unafikiria ni kwa jinsi gani maisha yako yangalikuwa ya furaha kama ungalifanya jambo fulani tofauti na ulivyofanya.

Unajaribu kutizama nyuma na kutaka kubadilisha yale unayofikiri yalikuwa makosa huko nyuma. Ila mimi ninachokuomba ni kusamehe nafsi yako.

Ni vigumu sana kumfuta kichwani mtu uliyempenda. Na hauwezi kupita njia ya mkato katika barabara ambayo Mungu ameamua akupitishe kufikia lile tumaini jema. Naam tumaini la kuwa na furaha pasipo ukomo.

Hivyo basi samehe yaliyopita na jivunie nafsi yako kwa vile yaloyopita yamekupa busara, yamekupa moyo, na mtizamo chanya. Ni vyema na busara kuikana nafsi yako kwa yale machungu na magumu tunayopitia.

Na muda mwingine makosa ambayo tumekwisha yafanya huweka alama mioyoni mwetu hua ni kama kilainishi cha kutufikisha kule ambako tunatakiwa tuwepo, kule kwenye matumaini na furaha tele.

Inawezekana ulisomesha mchumba na mwisho wa siku amekugeuka, sio kosa lako chukulia kama ulitoa msaada na samehe yaliyopita.

Au yawezekana uliolewa, mambo yalikuwa mazuri mwanzoni ila sasa hali si hali, umerudi kwenu huitamani tena ndoa. Samehe yaliyopita jipange upya. Thamani yako bado ipo.

Unazo baraka tele zinakuja upande wako. Kila gumu unalopitia linakuandaa kupokea jema linalo kuja.

Busara yangu, "No relationship is ever a waste of time if it didn't bring u what u want it taught you what u don't, as soon as your EX sees you smiling thats the minute they want you back"

Mungu akuvushe katika magumu unayopitia. AMEN!
 
hewizet

hewizet

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2013
Messages
1,785
Likes
518
Points
280
hewizet

hewizet

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2013
1,785 518 280
Umenipa morali na ujasiri pia nmeanza kutia mashaka huku nlipo maana sio mfatiliaji mzuri wa relationship!!
Shukran

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Lusajo11

Lusajo11

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Messages
1,898
Likes
1,658
Points
280
Lusajo11

Lusajo11

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2014
1,898 1,658 280
Labda mimi nina matatizo, mbona ma ex wangu nawasahau kabisa? Nishaurini jamani.
Ila kuna mmoja huyu ananiumiza kichwa!!
 

Forum statistics

Threads 1,237,227
Members 475,501
Posts 29,282,165