Same: Watu 11 wafariki kwa ajali ya gari

Shida ya kuwa na madereva wasio na weledi. Bust ya tairi ya nyuma haiwezi kufanya gari ipoteze uelekeo iwapo dereva hakukanyaga break.Hutakiwi kukanyaga break pale tairi inapopasuka,.Eneo la Same lina Upepo mkali muda wote. hutakiwi kwenda kasi inayozidi km 80 kwa saa.Hapa ni uzoefu ulikosekana. Pole kwa wafiwa, na Mungu awajalie wepesi wa kupona wale majeruhi.
 
Alphad imechomoka tairi ikakosa muelekeo ndio ikagonga haisi ilio kua na abiria wanao toka hedaru kuelekea same, na hata hvyo tumepoteza majirani zetu na ndugu pia. Innalillah wainna ilayranjuin.
Tairi inapotaka kuchomoka lazima utasikia ishara ya gari kuvaibrate na kelele upande husika. Luck of Skill
 
Shida ya kuwa na madereva wasio na weledi. Bust ya tairi ya nyuma haiwezi kufanya gari ipoteze uelekeo iwapo dereva hakukanyaga break.Hutakiwi kukanyaga break pale tairi inapopasuka,.Eneo la Same lina Upepo mkali muda wote. hutakiwi kwenda kasi inayozidi km 80 kwa saa.Hapa ni uzoefu ulikosekana. Pole kwa wafiwa, na Mungu awajalie wepesi wa kupona wale majeruhi.
kuna watu washakariri kika hitilafu ye anakimbilia brake kama mkomboz wake, burst ya nyuma ukituliza akili na kupanic unaokoka
 
Gari sio kuliendesha na umahiri wa kuliendesha.
Gari hukaguliwa unalizunguka unakagua Matairi na Berring kwa kutikisa magurudumu

Gari hufanyiwa Service na Maintanace kama ulieda Off road ukirudi lichunguze Wheel nuts na bolts

Hata ukiwa Dereva mahiri vipi gurudumu likichomoka wakati mnapishana na gari nyingine hakuna ujanja hiyo huwa uso kwa uso.
 
Baadhi ya waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo jioni Jumanne Aprili 13, 2021 baada ya gari aina ya Toyota Alphard kugongana uso kwa uso na gari jingine aina ya Toyota Noah,
Amesema abiria waliokuwamo katika Alphard walikuwa wakitokea Arusha kwenda Lushoto kwenye msiba na kwamba Noah ilikuwa ikitoka Hedaru kwenda Same.
“Alphard ilipata tyre bust (kupasuka gurudumu) ya nyuma ikayumba ikaenda kugongana na hiyo Hiace na wamekufa watu 10 na majeruhi 12. Watu 12 waliojeruhiwa walipelekwa hospitali ya wilaya ya Same.”
Mara Noah mara Hiece

Karne hii mtu hajui kutofautisha Hiece na Noah!!!?
 
Idadi ya vifo vilivyotokea katika ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro vimeongezeka na kufikia 11 baada ya majeruhi mmoja kati ya saba waliolazwa Hospitali ya Wilaya ya Same kufariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amesema hali za majeruhi wawili kati ya sita si nzuri na wamekimbizwa katika katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC huku wanne hali zao zinaendelea vizuri baada ya majibu ya X-ray kuonyesha wamepata majeraha madogo madogo.

Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Same ambapo magari mawili yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na majeruhi 12 kati ya hao sita walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same na wengine saba Hospitali ya KCMC.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom