Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Wakulima wa tangawizi katika wilaya Same mkoani kilimanjaro wamesema hawana soko la uhakika la zao hilo baada kiwanda cha kuchakata tangawizi cha Mamba kushindwa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka mitatu.
Wakulima hao wamesema kiwanda hicho ambacho walikitegemea kwa ajili ya kuuza tangawizi kwa sasa kimegeuka kero kutokana na wakulima kulazimika kuuza tangawizi kwa walanguzi kwa bei ndogo ya kati ya shilingi 700 hadi 1000 kwa kilo badala ya shilingi 2000.
Wamesema wanatumia gharama kubwa lakini wamekuwa wakipata hasara huku wengi wao wakikata tamaa kutokana na gharama za pembejeo zikiwa kubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Goha Bw. Evance Mbalazi amesema tangu kujengwa kwa kiwanda hicho wananchi hawajawahi kuuza tangawizi badala yake wakulima walikopesha tangawizi ambayo ilitupwa baada ya kuoza kwa madai kuwa mitambo iliyofungwa katika kiwanda hicho imeshindwa kuchakata tangawizi.