Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Uchambuzi uchwala huo.. hivi unamjua giroud wewe?? Giroud ana ufundi gani au anakaba?? Uliza ni msimu wa ngapi yupo EPL..

Kuna aina mbili au tatu za namba 9... kuna ile aina ya Firmino , aina ya Aguero na aina ya Samatta..wanaojua mpira wamenielewa..

BTW kocha kaona aina ya uchezaji wake tangu Genk na bado kamsajiri sasa wewe ni nani toka Tz useme hawezi fit Aston villa??
Watu kama wewe kwenye vijiwe vya Kahawa naweza nikakupiga mdomo.
 
Daah umenikumbusha mbali sana mambo ya Ruud van Nesteroy mtaalamu wa kumalizia tu hakua na mambo mengi huyu jamaa!! hao jamaa wanao mponda samata watakua Wachawi!! Watanzania tunalogana sisi wenyewe badala ya kumtakia mtu baraka na fanaka tele!! Eti hatamaliza maada za kipumbavu kama hizi huwa sizipendi zinanichefua sana
duuh, aisee
 
Jamaa walikubeza sana na huyo post ya kwanza akakuita mwanga kabisa,watu wakamshangilia. Unaona mbali sana mashabiki wengi Tz wana mihemko tu ya soka,lakini soka lenyewe hawalijui. Hasa hawa mashabiki wa simba na manara wamechangia kiasi kikubwa kuharibu soka la bongo. Naamini hata hao waliokupinga ndio hao wengi
 
Najua nitashambuliwa kwasababu waTz hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakina kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia . Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahis kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..
Sikubaliani na wewe hata kidogo,kwanza jiulize samatta amekaa uingereza muda gani?na je toka alipofika aliqeza kupata nafasi ya kuzoeana na wenzie?.Toka alipofika hakufanikiwa kuwa na wachezaji wenzie kwa muda mrefu ikaja corona,kwahiyo hakuweza kufanya kazi na wenzie kwa muda mrefu ili aweze kuuzoea mchezo wa uingereza
Unasema samatta hawezi kujitafutia mwenyewe,hivi unataka kuniambia washambuliaji wote wa uingereza wanajitafutia wenyewe mipira?
Jambo la muhimu hapa,ni kutambua juhudi za samatta na kumuomba huko aendako akapate mafanikio mengi,sio kumzodoa kiasi hicho ulichofanya wewe,wakati wewe huna hata uwezo wa kuchezea timu ya wazee wa uingereza
 
Back
Top Bottom