Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Binafsi kucheza ulaya tu ni hatua kubwa. Habari ya lig gan acheze na ip asicheze ni mipango ya Mungu.
Kumewahi kuwa wachezaji mahiri sana na walioshindwa kuwika EPL
Majina Kama Deco, Shevi, hawakuwah kufany vizuri EPL pamoja na uwezo wao walikotoka.
Mbwana kaonesha njia, kumponda hakutuongezei wala hakutupunguzii. Wengine hata Yanga au Simba tu tumeshindwa kufika.
#Haina Kufeli
Shida ni kwamba watu wanafanya analysis ya kitu walichokiona , hafu wao wanaleta zarau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kusema hili kwa uzuri tu. Sio kwasababu ya wivu lakini ilikua UHALISIA. Naona tunaanza kuyaona, kitu muhimu ni kuandaa watoto tokea chini kabisa kwaajili ya masafa ya ligi kama EPL. Hongera kwake pia kwa kutuandikia historia ambayo haijawahi kuandikwa na yeyote yule
Hongera kwako pia mkuu kwa kuwa na jicho la tatu, very few people can see beyond.
 
Huyu Samatta soon atapelekwa Uturuki kumalizia mpira wake baada ya timu yake kuwa imeshuka daraja.

Hana mpira wa kucheza EPL yule, ni kweli alibahatisha tu kwani hata spidi ya EPL hawezi.
Ili Ni Kaburi la tar 24 June,

Marehemu Alkua na mdomo Sana
 
Najua nitashambuliwa kwasababu watanzania hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie, inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia Samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakuna kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia . Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahisi kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..
yametimia na iyo sentensi ya mwisho ndio imetimia zaidi...
 
Mleta maada pongezi kwa kuona kile ambacho wengi hatukuona au pale tulipoona, kama ulivyoandika tuliona haya kusema kama kawaida yetu.

Mods: Napendekeza hii thread iwe sticky ili tuitumie kama rejea na kutanua wigo wa mjadala. Kwamba ikiwa mpambanaji kama Samatta kashindwa kufanya kazi epl, tunajifunza nini.

Binafsi nimejifunza mengi. Kwa leo nijadili hili moja. Kwamba "mfumo wetu wa soka hauna uwezo wa kuandaa mchezaji wa kiwango cha epl".

Baada tu ya mchezo wake wa kwanza Samatta alinukuliwa akisema kuwa dk 90 za epl ni sawa na kucheza mechi 2 mpaka 3 kwa Ubelgiji. Hivyo alichoka mapema na kufanya ishara ya kumtaarifu kocha kuwa afanyiwe mabadiliko (alikwenda chini).

Pia akadai kuwa kucheza pale kunahitaji nguvu sana ambayo hakuwa nayo hivyo akanuiya kuongeza mazoezi ya kujenga mwili (gym), kitu ambacho anakifanya mpaka sasa.

Kwa maneno yake yeye mwenyewe (kupitia Shaffi Dauda) ni kwamba angetumia zaidi advantage ya kasi na wepesi alionao ili kupata anachotaka.

Pendekezo:

Suala la shule za soka (vituo vya kukuzia watoto wanasoka) tusilichukulie kiutani utani tena. Serikali na TFF waje na mkakati thabiti wa kuhakikisha tunakuwa na vituo bora vya aina hii (soccer academies).

Huku tunajua watoto wataanza kupikwa mapema katika kila nyanja kuanzia ubongo, mtazamo, miguu, mpaka lishe bora. Lishe duni kwa wanamichezo ni sababu mojawapo ya kutokidhi ubora wa kimataifa wanapokua (hili liko dhahili).

Binafsi naamini kwamba huenda hata Samatta alianza kupata lishe bora (kwa mwanasoka) alipofika TP Mazembe! Unategemea nini hapo!

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom