Samata na Ulimwengu waonja ubingwa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
LUBUMBASHI, DR Congo
WASHAMBULIAJI wawili wa Tanzania, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamefanikiwa kutwaa taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya DR Congo baada ya timu ya TP Mazembe kuichapa DC Motema Pembe mabao 2-0.

TP Mazembe mabingwa wa Afrika 2009, 2010 ilitwaa ubingwa huo wa ligi ya DR Congo baada ya AS Vita Club iliyokuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa huo kutoka suluhu na CS Don Bosco.

Katika mechi dhidi ya DC Motema Pembe nyota hao wa Tanzania walikuwa kwenye benchi kuishudia timu yao TP Mazembe ilipata mabao yake kupitia Rainford Kalaba raia wa Zambia na mshambuliaji wa Mali, Cheibane Traore.

Kwa ushindi huo TP Mazembe ilifikisha pointi 30 ikiwa imeizidi AS Vita Club pointi nne, lakini timu hiyo bado ina mechi moja mkononi, na hata ikishinda mechi itafikisha pointi 29.

Hii ni mara ya 11 klabu ya TP Mazembe ya Lubumbashi inatwaa ubingwa wa DR Congo, ingawa timu za Kinshasa ndizo zimetwaa ubingwa huo mara nyingi kwa sababu AS Vita Club na DC Motema Pembe zimeishawahi kutwaa ubingwa huo mara 12.

Ubingwa huu wa Ligi Kuu ya DR Congo umeifariji timu hiyo ambayo ilikuwa na hasira ya kuondolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF katika Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mazembe na AS Vita Club zitaiwakilisha DR Congo katika Fainali za Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2012.
 
Let them shine, they deserve! Kila la kheri Samata na Ulimwengu. Habari hizi zinatufariji kidogo kwa upande wa soka la kimataifa kwa watanzania. I wish hatakama mngecheza hiyo mechi dhidi ya DC Motema Pembe ushindi ungepatikana tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom