Samani za Benki ya Exim nchini kupigwa mnada

Samani za Benki ya Exim nchini kupigwa mnada

Ni kweli fedha haiwezi kutosha. Lakini kama ukisoma taarifa ya Exim ni kuwa inaonyesha kama Mteja ametumia njia hiyo kama presha kwa benki kulipa deni

Sent using Jamii Forums mobile app

Inaweza kuwa njia ya kuipa presha benki lakini ni njia isiyo na tija. Kuidai benki kubwa kama Exim unaanza kwa kuuza samani ni mpango wa chini sana. Wanasheria wake wamefanya kazi nzuri kusaidia kushinda kesi lakini wanataka kumalizia vibaya kwenye namna ya malipo.
 
Kama hawawezi kulipa 1 billion wanafanya kazi gani?

Vipi ikiwa vilivyopigwa mnada havitakuwa na thamani ya pesa hiyo?

Shida haijirudii
 
Nataka kujua exim walichotaje mil 800 kwny a/c ya mteja wao?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Inaweza kuwa njia ya kuipa presha benki lakini ni njia isiyo na tija. Kuidai benki kubwa kama Exim unaanza kwa kuuza samani ni mpango wa chini sana. Wanasheria wake wamefanya kazi nzuri kusaidia kushinda kesi lakini wanataka kumalizia vibaya kwenye namna ya malipo.
Bado naona ni njia nzuri.
Unajua kwa Taasisi kama Benki ni jambo la fedheha kubwa kufanyiwa kitendo kama hicho! Kwa mteja ambaye huna jina kubwa unatumia mbinu yeyote kuhakikisha deni kama hilo unalipwa la utapigwa danadana sana.

Nakuhakikishia kama angekuwa Mengi au Mo kaibiwa angeshalipwa zamani sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hao madalali nao hovyo sasa Hela zote zilizojaa benki wewe unaenda kukamata meza Na viti?! Hapana aisee
 
Kwani huwezi kuchangia bila ya kuandika matusi? Sio kila member anafurahia kusoma michango yenye kebehi na matusi ndani yake. Kila mtu ana mtazamo wake tofauti juu ya mambo mbalimbali pia uwezo wa kuchambua mambo tunatofautiana. Lilikua ni jambo simple ungemwambia tu kistaarabu au ungemwambia afafanue uhusika wa Jpm. Sasa wewe unakurupuka tu unatukana tukana tu ovyo kwa sisi wenye akili tunakuona wewe ni mtu mwenye gonorrhea ya akili na wala siwezi kukaa nikajadiliana na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani unateseka sana?

"PILIPILI USIYOILA.............. "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pongezi Kwa Pendaeli Mollel

tangia 2013 unashindana na Exim Bank mahakamani si mchezo...

Exim Bank walibug wakumtapeli.!!

Mmasai mjanja...walidhani anamiliki Billions ki local kumbe yupo very smart

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Kutiana umaskini tu aisee, umepoteza milioni mia nane ya mtu miaka mitano aisee kuuza furniture is an insult, hivyo viti ndiyo vitafikisha bilioni?!!!! Benki kuu iingilie kati aisee hii ni dhurma!
 
Jinsi wanavojisikiaga wakienda kuuza Nyumba ya mtu ndivo na Mollel anajisikia saiv
 
Samani za Benki za Exim katika Matawi yote hapa nchini zitapigwa mnada kwa amri ya Mahakama baada ya benki hiyo kushindwa kulipa deni LA mteja wao ambapo pamoja na gharama mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka 13 ,limefika kiwango cha zaidi ya sh,Bilioni 1.

Maamuzi ya Mahakama yalifanyika Jana na utekelezaji wake unaanza muda huu

Hivi sasa Dalali wa Mahakama yupo ndani ya benki hiyo tawi la Arusha ili kuanza utekelezaji wa kutoa vitu nje ikiwemo viti,meza, laptops,Kompyuta na vingine jambo litakalo walazimu wateza na wafanyakazi wa benki hiyo kukaa chini ya sakafu .

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ,zoezi hilo litatekelezwa katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo hapa nchini.

View attachment 1015065

View attachment 1015066

View attachment 1015067

UPDATES:

Wafanyakazi wa benki ya EXIM tawi la Arusha wamelazimika kufanyakazi wakiwa wamesimama wakati wakiwahudumia wateja wao huku huduma zingine zikisimama baada ya samani za benki hiyo kukamatwa na kupigwa mnada kwa amri ya mahakama kutokana na benki hiyo kushindwa kulipa deni la sh,Bilioni 1.37 inayodaiwa na mteja wake.


Zoezi hilo la ukamataji wa mali za benki hiyo linatekelezwa na wakala wa mahakama kutoka kampuni ya First World Investment (Cout BROKER)na litatekelezwa katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo mkoa wa Arusha,baada ya mteja wa benki hiyo Pendael Mollel kushinda kesi ya msingi aliyoifungulia benki hiyo akiidai shi, billion 1.37

Mali zilizokamatwa ni pamoja na Meza,Viti,Makabati na Kompyuta,ambapo wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo meneja wa tawi wamelazimika kufanyakazi wakiwa wamesimama na wengine kukaa kwenye sakafu wakiwemo wateja .

Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo lililoanza mapema jana katika tawi la Arusha,Mdai wa benki hiyo ,Pendael Mollel alisema kuwa akiwa mteja wa benki hiyo alipoteza fedha zake kiasi cha shilingi milioni 800 zilizokuwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo mwaka 2013.

Alisema baada ya jitihada za kufuatilia fedha zake, benki hiyo ilionyesha nia ya kurejesha fedha hizo lakini iliendelea kuahidi bila kutekeleza ndipo mwaka 2014,Julai alipokimbilia mahakamani kuu kanda ya Arusha na kufungua kesi ya madai namba 9 ya 2014 .

Pendaeli Alisema mbali na kesi hiyo ambayo uamuzi wake ulimpa ushindi julai 2015 ,benki hiyo iliendelea kupinga maamuzi mbalimbali ya mahakama kwa kufungua kesi mbalimbali ,hata hivyo kesi hizo zilimpa ushindi Pendael, na ilipofika desemba 30,mwaka 2018 alishinda tena kesi iliyokuwa mahakama ya rufaa na baadae kukaza hukumu ambapo utekeelzaji wake umeanza kufanyika kuifilisi benki hiyo.

Amesema gharama za uendeshaji wa kesi hiyo katika kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2014 ,riba na malimbikizo mengine,Mahakama imeridhia benki hiyo imlipe mdai hiyo kiasi hicho cha sh,billion 1.37.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo imesema kuwa kesi hiyo bado ni endelevu na wanakusudia kukata rufaa ili kusimamisha utekelezaji wa zoezi la uuzwaji wa samani za benki hiyo .

Naye wakala wa mahakama,anayetekeleza zoezi hilo,kutoka kampuni ya farst world investiment,Allan Rubben amesema kuwa kampuni yake inatekeelza amri ya mahakama kutoka kwa mdai Pendael Mollel aliyefungua shauri hilo mahakamani akiidai benki ya Eximu.

Amesema utekelezaji wa zoezi hilo utalenga kupiga mnada samani za benki hiyo katika matawi yote Mkoani Arusha na Leo utekelezaji umeendelea katika tawi la EXIM Corporation lililopo Barabara ya Kijenge jijini hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mabenki yote yana deposit bank kuu kwani mahakama isiimaru benki ilipe hizo pesa badala ya kuangaika na thamani?
 
Kwaiyo bank kama EXIM inakosa billion mmoja na milion 370 ya kumlipa jamaa, aisee nawasikitikia walioweka pesa zao hapo.
 
Inasemekana watauza samani inji nzima mpaka hiyo 1.3b ipatikane. Hapo Arusha ni mwanzo tu
 
Back
Top Bottom