Samani za Benki ya Exim nchini kupigwa mnada

Samani za Benki ya Exim nchini kupigwa mnada

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Samani za Benki za Exim katika Matawi yote hapa nchini zitapigwa mnada kwa amri ya Mahakama baada ya benki hiyo kushindwa kulipa deni LA mteja wao ambapo pamoja na gharama mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka 13 ,limefika kiwango cha zaidi ya sh,Bilioni 1.

Maamuzi ya Mahakama yalifanyika Jana na utekelezaji wake unaanza muda huu

Hivi sasa Dalali wa Mahakama yupo ndani ya benki hiyo tawi la Arusha ili kuanza utekelezaji wa kutoa vitu nje ikiwemo viti,meza, laptops,Kompyuta na vingine jambo litakalo walazimu wateza na wafanyakazi wa benki hiyo kukaa chini ya sakafu .

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ,zoezi hilo litatekelezwa katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo hapa nchini.

exim3.jpg


exim5.jpg


exim.jpg


UPDATES:

Wafanyakazi wa benki ya EXIM tawi la Arusha wamelazimika kufanyakazi wakiwa wamesimama wakati wakiwahudumia wateja wao huku huduma zingine zikisimama baada ya samani za benki hiyo kukamatwa na kupigwa mnada kwa amri ya mahakama kutokana na benki hiyo kushindwa kulipa deni la sh,Bilioni 1.37 inayodaiwa na mteja wake.


Zoezi hilo la ukamataji wa mali za benki hiyo linatekelezwa na wakala wa mahakama kutoka kampuni ya First World Investment (Cout BROKER)na litatekelezwa katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo mkoa wa Arusha,baada ya mteja wa benki hiyo Pendael Mollel kushinda kesi ya msingi aliyoifungulia benki hiyo akiidai shi, billion 1.37

Mali zilizokamatwa ni pamoja na Meza,Viti,Makabati na Kompyuta,ambapo wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo meneja wa tawi wamelazimika kufanyakazi wakiwa wamesimama na wengine kukaa kwenye sakafu wakiwemo wateja .

Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo lililoanza mapema jana katika tawi la Arusha,Mdai wa benki hiyo ,Pendael Mollel alisema kuwa akiwa mteja wa benki hiyo alipoteza fedha zake kiasi cha shilingi milioni 800 zilizokuwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo mwaka 2013.

Alisema baada ya jitihada za kufuatilia fedha zake, benki hiyo ilionyesha nia ya kurejesha fedha hizo lakini iliendelea kuahidi bila kutekeleza ndipo mwaka 2014,Julai alipokimbilia mahakamani kuu kanda ya Arusha na kufungua kesi ya madai namba 9 ya 2014 .

Pendaeli Alisema mbali na kesi hiyo ambayo uamuzi wake ulimpa ushindi julai 2015 ,benki hiyo iliendelea kupinga maamuzi mbalimbali ya mahakama kwa kufungua kesi mbalimbali ,hata hivyo kesi hizo zilimpa ushindi Pendael, na ilipofika desemba 30,mwaka 2018 alishinda tena kesi iliyokuwa mahakama ya rufaa na baadae kukaza hukumu ambapo utekeelzaji wake umeanza kufanyika kuifilisi benki hiyo.

Amesema gharama za uendeshaji wa kesi hiyo katika kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2014 ,riba na malimbikizo mengine,Mahakama imeridhia benki hiyo imlipe mdai hiyo kiasi hicho cha sh,billion 1.37.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo imesema kuwa kesi hiyo bado ni endelevu na wanakusudia kukata rufaa ili kusimamisha utekelezaji wa zoezi la uuzwaji wa samani za benki hiyo .

Naye wakala wa mahakama,anayetekeleza zoezi hilo,kutoka kampuni ya farst world investiment,Allan Rubben amesema kuwa kampuni yake inatekeelza amri ya mahakama kutoka kwa mdai Pendael Mollel aliyefungua shauri hilo mahakamani akiidai benki ya Eximu.

Amesema utekelezaji wa zoezi hilo utalenga kupiga mnada samani za benki hiyo katika matawi yote Mkoani Arusha na Leo utekelezaji umeendelea katika tawi la EXIM Corporation lililopo Barabara ya Kijenge jijini hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabenki JPM ili kutoharibu uchumi, aliangalie sana. NI ushauri tu maana benki moja inapokufa kuna athari sana, hasa kwa wananchi wenye kutumia huduma za kibenki
 
Inayopigwa mnada ni bank au samani? Rekebisha heading.
 
PUMBAVU THAAAAANA...!!! JPM kaanza kutawala TZ kabla ya hiyo miaka 13?

Na bado jipu lililotumbuliwa kwa vyeti feki, utanyoooka tu hadi ubaki mdogo km sisimizi kwa chuki zako binafsi dhidi ya serikali ya JPM.
PUMBAVU THAAAAANA...!!!



Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani huwezi kuchangia bila ya kuandika matusi? Sio kila member anafurahia kusoma michango yenye kebehi na matusi ndani yake. Kila mtu ana mtazamo wake tofauti juu ya mambo mbalimbali pia uwezo wa kuchambua mambo tunatofautiana. Lilikua ni jambo simple ungemwambia tu kistaarabu au ungemwambia afafanue uhusika wa Jpm. Sasa wewe unakurupuka tu unatukana tukana tu ovyo kwa sisi wenye akili tunakuona wewe ni mtu mwenye gonorrhea ya akili na wala siwezi kukaa nikajadiliana na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbona taarifa yko ya kindezi yan bank iuziwe furniture zake kisa den la 1b wakat kwa mwaka inaingiza mara 20 ya hyo as profit


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Dadavua vizuri basi!
Nime maanisha hivi,

Hadi kufikia bank kupigwa mnada thamani zake kutokana na kushindwa kulipa deni ni tafsiri ya "Gearing ratio kuwa ndogo" (yaani uwezo wa kampuni kulipa madeni ya mda mrefu kwa wakati) ni mdogo

Mali za bank zinaweza kuwa magari,majengo, viwanja,uwekezaji makampuni mengine uwekezaji mashirika ya umma n.k

Kwa mantiki hii, Bank zote zipo chini ya bank kuu na zinaendeshwa na zinasimamiwa na sheria mbali mbali kama vile "bank and financial serv act 2006", company act 2002, Central Bank act n.k n.k Ambapo sheria zote hizi zinazitaka bank husika ziwe Audited na Independent auditor ambaye mwisho wa siku ataleta findings ya kuonesha GEARING RATIO na mambo mengine kama LIQUIDITY ya bank husika ni ndogo.

Baada ya hapo BOT ndio inaona kama bank inashindwa kulipa madeni ya muda mrefu na mfupi je kuna uwezekano wa mitaji na amana za wateja kuwa salama?

Pia mtoa mada amesema samani za bank zinapigwa mnada na wafanya kazi na wateja watakaa Chini. ndo hapo nkaibua hoja je BOT haikuona hili suala na kutathmini hali ya mitaji na amana za wateja?.

Anyway mambo ni mengi sana ya kutiririka ila muda nao ni mali ila hiki ndicho nilichomaanisha kwa ufupi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom