Samani za Benki ya Exim nchini kupigwa mnada

Samani za Benki ya Exim nchini kupigwa mnada

Sasa mbona hivyo vitu walivyosomba thamani yake hata theluthi ya hilo deni haifiki,.au ni auction endelevu???
 
Mabenki JPM ili kutoharibu uchumi, aliangalie sana. NI ushauri tu maana benki moja inapokufa kuna athari sana, hasa kwa wananchi wenye kutumia huduma za kibenki
Hujui kitu
Huyo mteja aliibiw pesa na mfanyakazi wa hiyo benki miaka 13 iliopita akaenda mahakamani akashinda
Magufuli anaingiaje hapo?
 
wanapouza izo thamani za benk,hela itakayopatikana ndo itaweza kufidia iyo bilioni moja ? na isipofikia hiyo hela itakuwaje hapo
 
IMG-20190206-WA0012.jpg
 
Wafanyakazi wa benki ya EXIM tawi la Arusha wamelazimika kufanyakazi wakiwa wamesimama wakati wakiwahudumia wateja wao huku huduma zingine zikisimama baada ya samani za benki hiyo kukamatwa na kupigwa mnada kwa amri ya mahakama kutokana na benki hiyo kushindwa kulipa deni la sh,Bilioni 1.37 inayodaiwa na mteja wake.


Zoezi hilo la ukamataji wa mali za benki hiyo linatekelezwa na wakala wa mahakama kutoka kampuni ya First World Investment (Cout BROKER)na litatekelezwa katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo mkoa wa Arusha,baada ya mteja wa benki hiyo Pendael Mollel kushinda kesi ya msingi aliyoifungulia benki hiyo akiidai shi, billion 1.37

Mali zilizokamatwa ni pamoja na Meza,Viti,Makabati na Kompyuta,ambapo wafanyakazi wa benki hiyo akiwemo meneja wa tawi wamelazimika kufanyakazi wakiwa wamesimama na wengine kukaa kwenye sakafu wakiwemo wateja .

Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo lililoanza mapema jana katika tawi la Arusha,Mdai wa benki hiyo ,Pendael Mollel alisema kuwa akiwa mteja wa benki hiyo alipoteza fedha zake kiasi cha shilingi milioni 800 zilizokuwa kwenye akaunti yake katika benki hiyo mwaka 2013.

Alisema baada ya jitihada za kufuatilia fedha zake, benki hiyo ilionyesha nia ya kurejesha fedha hizo lakini iliendelea kuahidi bila kutekeleza ndipo mwaka 2014,Julai alipokimbilia mahakamani kuu kanda ya Arusha na kufungua kesi ya madai namba 9 ya 2014 .

Pendaeli Alisema mbali na kesi hiyo ambayo uamuzi wake ulimpa ushindi julai 2015 ,benki hiyo iliendelea kupinga maamuzi mbalimbali ya mahakama kwa kufungua kesi mbalimbali ,hata hivyo kesi hizo zilimpa ushindi Pendael, na ilipofika desemba 30,mwaka 2018 alishinda tena kesi iliyokuwa mahakama ya rufaa na baadae kukaza hukumu ambapo utekeelzaji wake umeanza kufanyika kuifilisi benki hiyo.

Amesema gharama za uendeshaji wa kesi hiyo katika kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2014 ,riba na malimbikizo mengine,Mahakama imeridhia benki hiyo imlipe mdai hiyo kiasi hicho cha sh,billion 1.37.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo imesema kuwa kesi hiyo bado ni endelevu na wanakusudia kukata rufaa ili kusimamisha utekelezaji wa zoezi la uuzwaji wa samani za benki hiyo .

Naye wakala wa mahakama,anayetekeleza zoezi hilo,kutoka kampuni ya farst world investiment,Allan Rubben amesema kuwa kampuni yake inatekeelza amri ya mahakama kutoka kwa mdai Pendael Mollel aliyefungua shauri hilo mahakamani akiidai benki ya Eximu.

Amesema utekelezaji wa zoezi hilo utalenga kupiga mnada samani za benki hiyo katika matawi yote Mkoani Arusha na Leo utekelezaji umeendelea katika tawi la EXIM Corporation lililopo Barabara ya Kijenge jijini hapa.

IMG_20190205_173056.jpeg
IMG_20190205_173319.jpeg
IMG_20190205_151148.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hizo pesa anazodai bwana mollel mbna Ni nyingi tofauti na samani wanazouza
 
Hapa iko namna, 1.3 B hata kama wakiuza hilo tawi na wafanyakazi wake wote pamoja na walinzi haipatikani hiyo pesa.
Kama mahakama imeshaamua mteja alipwe, si ingetosha tu kupewa muda mpunga uingie kwenye akaunt?
 
Sasa hivyo viti nani atanunua? Na vinaweza fika thamani ya deni kweli?
 
Sasa hivyo viti nani atanunua? Na vinaweza fika thamani ya deni kweli?
Dalali atapiga mnada kwa mujibu wa taratibu, zisipotosha watakamata magari na vitu vingine, zisipotosha benki itafilisiwa na watalipwa na BOT, ofisi zao wamepanga kwa hiyo hawawezi kupiga mnada
 
Hapa iko namna, 1.3 B hata kama wakiuza hilo tawi na wafanyakazi wake wote pamoja na walinzi haipatikani hiyo pesa.
Kama mahakama imeshaamua mteja alipwe, si ingetosha tu kupewa muda mpunga uingie kwenye akaunt?
Ni kweli fedha haiwezi kutosha. Lakini kama ukisoma taarifa ya Exim ni kuwa inaonyesha kama Mteja ametumia njia hiyo kama presha kwa benki kulipa deni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom