GAMBLER
JF-Expert Member
- Nov 22, 2009
- 303
- 11
Nina wasiwasi mkubwa kuhusu hawa samaki, hasa ukizingatia taasisi walizopewa hao samaki, kama vituo vya kulelea watoto yatima, wafungwa na wanafunzi. Tujiulize maswali 2, kwa nini hawa samaki wauzwe baada ya kushindwa zoezi la kuwauza? Na kwa nini watu wakatae kuwanunua? Ukienda soko la samaki ferry, utaona watu wengi wako wanahitaji samaki, na hakuna samaki wa kutosha. Hawa samaki wa magufuli ni aina ya jodari, ni samaki wenye soko sana, inakuwaje pale serekali ilipotangaza kuwauza, hawakuuzika??