Samaki wa kupaka (grilled fish with coconut sauce)

Mahitaji

1)Samaki mkubwa...
2)nyanya 2..
3)kitunguu thomu 1 teaspoon..
4)tangawizi 1 teaspoon
5)bizari ya njano kiasi
6)bizari ya pilau 1 teaspoon...
7)ndimu 2...
8)kitunguu maji 1..
9)chumvi kiasi
10)pilipili manga 1 teaspoon
11)pilipili mbuzi 1
12)tomato sauce
13)tui la nazi 1-1.5 kikombe...

Namna ya kutaarisha samaki

1)safisha vizuri samaki wako na umeweke alama kwa kisu ili viungo viingie ndani ya samaki..muache akolee viungo for 30minutes

2)weka samaki kwenye trey na umuunge kwa pilipili manga,chumvi,ndimu 1,bizari ya pilau,kitunguu saumu na tangawizi...

3)muweke kwenye oven moto kiasi ili awive vizuri....akiwiva upande mmoja mgeuze upande wa pili...

4)ukishawiva pande zote mbili weka samaki kwenye sahani.....


Namna ya kutaarisha sauce

1)saga nyanya,pilipili mbuzi na kitunguu maji weka maji kidogo sana au unaweza tumia tui badala ya maji..

2)weka tui jikoni,mimina mchanganyiko wako uliosaga,weka na bizari...koroga na wacha vichemke vizuri

3)weka tomato paste kiasi ili sauce iwe nzito nzito...

4)weka ndimu....acha ichemke kwa dakika 5 then epua

5)mimina sauce yako juu ya samaki ulimtaarisha kabla



Samaki wa kupaka (grilled chicken with coconut sauce) tayari kwa kuliwa...
thanks for menu sir..
 
Huku saa hizi ni saa sita kasoro tano, ubao umenishika lunchi ni hii Sandwich ya Kizungu na wewe ndo kwanza unaongelea samaki wa kuchora sijui kupaka????

Hapo! Mate debe.
 
Huku saa hizi ni saa sita kasoro tano, ubao umenishika lunchi ni hii Sandwich ya Kizungu na wewe ndo kwanza unaongelea samaki wa kuchora sijui kupaka????

Hapo! Mate debe.

Poleeee..

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
farkhina ahsante yani samaki napenda sana kwa wiki zaidi ya mara 3 lazima nile ila si wajua usela sina oven so nampika kama unavyosema ila simgril anakuwa mbichi na mtamu balaa.Watu wanashangaaga kwa nini mbichi afu hana shombo?ha ha ha mapishi mwaya.
Shem wako juzi kaniambia kanunua oven yani atanikoma mapishi na hivi apenda kula mapenzi yatazidi wallah atatangaza ndoa lol
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom