Sam Mahela wa ITV na kipindi cha upande mmoja

Nadhani ndio uwezo wa Sam huo. Amefikia kikomo. Hawezi kufanya vizuri zaidi ya hapo. Kwa kweli siyo kipindi cha maswali na majibu. Ni kipindi cha propaganda za CCM na serikali yake. Inasikitisha kwa kweli.
 
Mahela kipindi chako kinakosa mvuto. wanangalia wachache.

Mosi, unauliza mambo ambayo ni ama huyajui au umedangishwa. Maswali mengi uliyomuliza jafo ilifaa umulize Mtendaji wa Kata au Mek (Mratibu wa elimu kata)

Pili, kipindi kinakosa mvuto kwa kuwa kuna fanani/ msimuliaji tu na hadhira hairuhusiwi kuliza maswali.

Tatu, maswali unayouliza siyo fikirishi yanampa muulizwaji nafasi ya kuelezea hisia badala ya actual facts. Mfano wewe unasemaje? Hupaswi kumuliza waziri hivyo kwakuwa hujamwalika kama mtu binafsi umeialika wizara.

Nne, unatumia vibaya gesture? Kuongeza chunvi yale unayoyaongea.huwapi watazamaji uhuru wa kuamua juu ya unachohoji.

Nakifananisha kipindi hiki na mazungumzo baada ya habari, bwana Juma Ngondai alikuwa ananiacha na maswali mengi sana pasi na majibu lakini sasa najua alikuwa anadanganya, kutisha na kuogofya watu.

Mahela boresha kipindi, ruhusu simu toka kwa walaji

Kwakweli mkuu hicho kipindi hakina mvuto kabisa,sijui waandishi wetu wana nini. Hili ombwe sijui nani atajaliziba.
Hivi hakuna mwandishi kijana anayetamani kuwa kama Tido Mhando?
 
Una muda wa mchezo sana..kwangu mm marufuku clouds FM, clouds TV, radio one, TBC, ITV. Ni marufuku kwangu..!! Habari naangalia azam two ..nikitaka mpira dstv, nikitaka yanga azam anatosha..nikitaka mziki MTV base, Chanel e ya majizo basi..!! Wanafki hawana nafsi kwangu.

Tena habari nyingi now nazipata jf zikiwa hazijaeditiwa. Miziki YouTube.

ebu angalia mtangazaji anavyomuhoji Rais wa France..mahela kujipendekeza tu..tatzo hatobadilika ataona km tunamchukia.

Kidogo charles hilary/nurdin suleman/ivona na Muhuza wanaweza kumweka mtu kitimoto na kumchapa maswali ya maana.. Poor ITV..
Kwa hio mkuu kwako una dishi mbili kwa Mpigo, Ya DSTV&AZAM sio?
 
Jamaa unakuta anamuuliza Waziri wa JPM eti "KWA UJUMLA UNAONAJE KASI YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWENYE SERIKALI HII?

Hivi hapo unategemea utapata jibu gani sasa kwa waziri husika.
 
Remote, remote baba; I mean remote imeshikwa na mtu mwingine kuhakikisha vyombo vya habari vinatangaza yanayo takiwa tu and hence mwandishi hapaswi kuuliza maswali ya maana labda awe kamualika mpinzani
 
ITV sasa haina mvuto sasa kipindi kile sijui anategemea waziri atasemaje au atapinga kwamba serikali haifanyi vizuri?? kwakweli ITV kuweni creative na baadhi ya vipindi mfano kipindi THIS WEEK IN PERSPECTIVE japo sitazamagi TBC lakini huwa nalazimika kutazama.
 
Hao ITV tokea wapigwe faini.kwa "kosa" la kureport taarifa ya kituo cha LHRC

Hivi sasa wamekuwa kama TBC..
Siku hizi wanajifungia na kujipiga faini wao wenyewe. Wameweka 'precedence' kwa watu wa ulimwengu wote, haikuwahi kutokea! Nasikia watu wa Guinness Records wanataka kuiingiza kwenye records zao!
 
n
Sio lazima kupiga simu maana hata wapiga simu huwa wanapangwa waulize nini. ilitakiwa kipindi kina uliza maswali bila kumpa mgeni kutoa ngonjera kuiga sio kubaya hivi hawaoni BBC Hardtalk, unapigwa maswali kama boxing unawekwa corner hakuna hadithi.
nafikiri media zetu zinapaswa kuwa na watu wa aina ya bulendu sio hawa wakina enock bwigane wanywa konyagi za kupima mjini
 
Mahela kipindi chako kinakosa mvuto. wanangalia wachache.

Mosi, unauliza mambo ambayo ni ama huyajui au umedangishwa. Maswali mengi uliyomuliza jafo ilifaa umulize Mtendaji wa Kata au Mek (Mratibu wa elimu kata)

Pili, kipindi kinakosa mvuto kwa kuwa kuna fanani/ msimuliaji tu na hadhira hairuhusiwi kuliza maswali.

Tatu, maswali unayouliza siyo fikirishi yanampa muulizwaji nafasi ya kuelezea hisia badala ya actual facts. Mfano wewe unasemaje? Hupaswi kumuliza waziri hivyo kwakuwa hujamwalika kama mtu binafsi umeialika wizara.

Nne, unatumia vibaya gesture? Kuongeza chunvi yale unayoyaongea.huwapi watazamaji uhuru wa kuamua juu ya unachohoji.

Nakifananisha kipindi hiki na mazungumzo baada ya habari, bwana Juma Ngondai alikuwa ananiacha na maswali mengi sana pasi na majibu lakini sasa najua alikuwa anadanganya, kutisha na kuogofya watu.

Mahela boresha kipindi, ruhusu simu toka kwa walaji

Kumbe bado unaangalia ITV? Una moyo kweli. Hawana tofauti na Star Tv au TBC. Wana kipindi chao cha kipima joto (katikati ya habari), wanaowauliza maswali ni madereva taxi wa pale Kijitonyama-Opposite na LAPF Millenium Towers. Habari za Upinzani wanaripoti yale yaliyo positive tu kwa Serikali.
 
Habari wanajukwaa la siasa.

Ktk kipindi cha ITV dk 45, waziri wa Tamisemi mheshimiwa selemani Jafo amekuwa akihojiwa kwa majuma mawili ambapo alimaliza mahojiano yake Jana.

Sam Mahela ambaye ndiye host wa kipindi alimuaga Mheshimiwa Jafo kwa kumuambia " Nakuona kwa macho yangu ukitoka hapo ulipo na kushika nafasi ya juu kabisa serikalini "
 
Back
Top Bottom