watangazaji wengi wa bongo wanamwiga Salim Kikeke, hili halina mjadala.
Kama utakumbuka kabla ya Salim, watangazaji wengi kama si wote walikuwa wanasoma habari kama wanashusha bendera ya taifa, yaani wamenyoka nyooo, hakuna kutabasam wala nini!
Lakini siku hizi wanajifanya wanasoma kwa mbwembwe. Mara wapinde utafikiri wamekalia kitu cha moto, mara watoe ishara kama wanamsomea kiziwi, mara watoe maoni yao kwenye habari yaani tabu tupu!
Hao akina sam hata mwongozo wa habari siku hizi hawafati, anajiongelea atakavyoona yeye inafaa.