Salum Mwalimu: Wanakinondoni mkimchagua mbunge dhaifu, mtaendelea kuwa dhaifu kwa miaka mitatu ijayo

Kanguyeyejr

Senior Member
Jan 27, 2018
105
91
Amani iwe nanyi, Leo hii akihutubia Morocco Salum Mwalim amewaasa wana Kinondoni kutomchagua mbunge dhaifu kwani watakuwa dhaifu kwa miaka mitatu ijayo.

Amewaomba wanakinondoni kutumia vizuri kodi yao takribani sh billion moja inayotumika kulipia gharama za uchaguzi huo wa marudio unaofanyika kufuatia kujiuzulu kwa mh Mtulia kwa madai anamuunga mkono mwenyekiti wa CCM.

Amewataka wapiga kura kujitokeza na kumpigia kura za kutosha kwani hatawasaliti na hanunuliki, ova
 
Tundu Lissu ameianika nchi yetu duniani kuwa wanaminya demokrasia.....

Kwa hiyo CCM wataogopa kufanya "madudu" yao waliyoyafanya kwenye chaguzi za madiwani

Kwenye uchaguzi huu kama Chadema watazithibiti kura zitazopigwa basi ushindi ni dhahiri!
 
Tundu Lissu ameianika nchi yetu duniani kuwa wanaminya demokrasia.....

Kwa hiyo CCM wataogopa kufanya "madudu" yao waliyoyafanya kwenye chaguzi za madiwani

Kwenye uchaguzi huu kama Chadema watazithibiti kura zitazopigwa basi ushindi ni dhahiri!
Mm naomba kusiwepo na maagizo kutoka mbinguni yatavuruga uchaguzi wote
 
Ccm wanajua wazi kuwa watashindwa uchaguzi huu lakini watajianda kuiba na kupora kura kwa sababu hawana sera za kumkomboa mtanzania
 
Sasa wenzake wanalalamikia 1bn yeye anashauri itumbuliwe vizuri.. ha ha haaaaaaaa

Hivi huwa hamna washauri.. eti dhaifu.. mbona hasemi kivipi!! Maana kuhama tu chama haitoshi.. hapo hata nondo hana za kushusha.. na mie nazofikiria siwaandikii hata kidùnchu..

Kituko.. jamani tutumbue pesa hiyo.. 1bn halafu tumpigie kura wa CCM kama kawa.. sawa wana upinzani.. eeeeeh
 
Back
Top Bottom