Heko mbunge Mwidau kwa kuliona hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heko mbunge Mwidau kwa kuliona hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMAPILI, SEPTEMBA 16, 2012 08:08 NA BAKARI KIMWANGA, PANGANI

  BUNGE ni moja ya mhimili wa nchi ambao umekuwa na wabunge ambao huwa ni wajumbe wa chombo hicho kwa ajili ya kutunga sheria za nchi. Kutokana na hali hiyo kwa muda mrefu tangu taifa letu lilipopata Uhuru wake mwaka 1961 lilikuwa likijulikana kama Bunge la Tanganyika na hata baada ya Muungano bado chombo hiki kimekuwa na uwakilishi wa pande mbili za Muungano.

  Mwaka 1995 Tanzania ilifanya uchaguzi wake wa kwanza ambao ulishirikisha mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao wakati huo tuliweza kuona namna Bunge lilivyokuwa na uwakilishi ambao haukuwa stahiki.

  Hata katika uchaguzi uliofuata wa mwaka 2000, 2005 na hata 2010 tumeona namna Bunge lilivyokuwa na wingi wa wabunge kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku ikifuatiwa na Chadema ambayo ina wabunge 47, CUF 36, NCCR-Mageuzi wanne wakati TLP na UDP vikiwa na wabunge mmoja mmoja.

  Kutokana na hali hiyo tafakuri yetu ya wiki imebahatika kukutana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), ambaye pamoja na mambo mengine anasema sasa umefika wakati kwa watanzania kukataa kuongeza wingi wa wabunge kutoka CCM.

  Katika Bunge hili la 10, jina la Amina Mwidau ni jina ambalo si geni katika masikio ya watu kutokana na umahili wake ndani na nje ya Bunge.

  Mbunge huyo pia amebahatika kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika la Umma, na hata kuwa sehemu ya wasimamizi wakuu wa rasilimali za umma hasa mashirika.

  Mwidau anasema ikiwa wananchi sasa wataamua kuchangua wabunge wengi katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kutoka vyama vya upinzani inaweza kuimarisha demokrasia ya kweli ndani ya chombo hicho cha uwakilishi.

  Anasema hali ilivyo sasa wengi wa wabunge wa CCM kazi kubwa wanayoifanya ni kuzomea wenzao kutoka vyama vya upinzani hata zinapokuwa zinajadiliwa hoja za msingi na zenye maslahi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  “Wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekuwa ni kikwazo kwa wabunge wa upinzani huku wengi wao wana kazi ya kuzomea wabunge wenzao hata yanapojadiliwa masuala ya taifa.

  “Kutokana na hatua hiyo mbunge huyo amewataka wananchi kuhakikisha wanawakataa katika masanduku ya kura itakapofika mwaka 2015 ili Bunge hilo liwe na wabunge wengi kutoka vyama vya upinzani,” anasema Mwidau.

  Anasema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa chini ya mabadiliko ya 5 na 14 ya Katiba ya Tanzania, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linao wabunge wa aina sita.

  Akitaja wabunge hao ni pamoja na wabunge wa kuchaguliwa na wananchi kuwakilisha majimbo yao ya uchaguzi ambao kwa sasa idadi yao kutoka Tanzania Bara ni 189 na wanaotoka Tanzania Visiwani ni 50. Kadhalika, Bunge hili linao wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

  Mwidau anasema ukiachia hao, wapo pia wabunge wa viti maalumu wanawake ambao idadi yao ni 102. Idadi hiyo inaifanya jumla ya wabunge wa viti maalumu wanawake kuwa sawa na asilimia 30 ya wabunge wote bungeni. Wabunge wote kwa sasa ni 352.

  “Huku wabunge wengine 10 wa huteuliwa na Rais. Hadi sasa, Bunge linao wabunge saba wa kuteuliwa na Rais.

  “Utaratibu wa Bunge la Tanzania ni kuwa na uwakilishi wenye mfumo wa kambi na katika vipindi viwili mfulizo chama chetu ya CUF kimekuwa kikiiongoza kambi ya Upinzani lakini safari hii imekuwa ni zamu ya Chadema.

  “Wajibu wa Kambi ya upinzani ni kuiwajibisha na kuikosoa serikali kwa kuhoji utendaji wake hasa katika maeneo yenye upungufu ya utendaji na sera lakini kwa mfumo huu wa Bunge letu ambao wabunge wengi ni wa CCM tumekuwa tukipambana nao kwa kila jambo.

  “Mfumo wowote imara wa demokrasia unahitaji upinzani imara na katika Bunge la Tanzania, licha ya uchache wa wabunge hao, wabunge wa upinzani wamekuwa na mchango mkubwa katika Bunge,” anasema Mbunge Mwidau.

  Kama ilivyo kwa Serikali ya Chama Tawala kuwa na mawaziri, Kambi ya Upinzani nayo huwa na mawaziri wanaoitwa ‘Waziri Kivuli”.

  Akihutubia mkutano wa Kijiji cha Mwera Wilayani Pangani katika ziara yake kama mbunge anayewajibika na mkoa wake wa Tanga, anasema ni wajibu kwa wawakilishi wa wananchi kutambua wajibu wao ikiwamo na kutatua kero zinazowakabili kwa wakati.

  Katika mkutano huo Mwidau, alikabidhi msaada wa pampu ya kusukumia maji kwa wananchi wa Kijiji cha Mwera na kusema kuwa ili taifa liweze kuingia katika demokrasia ya kweli umefika wakati wa kuikataa na kuichukia CCM kwa vitendo.

  “Leo nchi imekuwa na matatizo kila kona kutokana na kukosekana wabunge wa kweli ambao wana uchungu wa kuwatetea wananchi na ninayasema haya mchana kweupe … idadi ya wabunge wengi wa CCM imekuwa ni kikwazo kwetu sisi wapinzani.

  ‘Kwa zaidi ya miaka miwili sasa hajarudi tena na hata leo hii mna tatizo la maji kwa mota kuungua hana habari nanyi.

  “Ili kuweza kupambana na mfumo huu mbovu ulioandaliwa na CCM kutokana na sera zake kuwa mbovu tunahitaji kujenga nchi kwa kuwa na viongozi jasiri kama Profesa Lipumba ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania haki za Watanzania.

  “Ninakabidhi mashine hii yenye thamani zaidi ya Sh milioni tano kuweza kutatua kero ya maji katika Kijiji hiki cha Mwera. ‘Ninajua uchungu wa maji kwani hali hii iliyopo sasa wanaopata taabu ni wanawake wenzangu na watoto ambao hutumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za uzalishaji maji,” anasema Mwidau.

  Mbunge huyo wa viti maalum anaonyesha wasiwasi wake wa kukwama kwa Malengo ya Milenia kutokana na Serikali kuwa na sera mbovu hasa katika kuwaongoza wananchi bila kujua matatizo yanayowakabili.

  “Tunahitaji kuwa na mipango endelevu na kupitia CUF tumejipanga kuwa na jamii imara iliyostawi kwa kuiwezesha kwa kuipatia mahitaji muhimu ya jamii sambamba na kuwapo vifaa kama vya hospitali, shule na hata katika kuimarisha sekta ya maji na barabara,” anasema.

  Anasema yeye kama mwakilishi wa wananchi ambao ndiyo waajiri wake wanayo sababu na haki kumtaka atoe maelezo kwa mujibu wa sheria yakiwamo yaliyotokea katika mikutano ya Bunge.

  “Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma niliibua na kufichua ufisadi uliofanywa na Serikali na watendaji ambao kwa sasa ndiyo wamekuwa waketelezaji wa ilani dhaifu ya CCM,” anasema Mbunge huyo.

  Mwidau anasema wakati anayafanya hayo wakati wote anaongozwa na dhamira safi ya chama chake cha CUF ambacho kimekuwa kinara katika kupigani misingi ya misingi ya utawala bora, haki, usawa na utawala wa sheria katika kuwezesha na kujenga ustawi wa taifa.


  bkimwanga@yahoo,com
  0715 247 327

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Mbunge wa CUF anatoa ZAWADI haswa kwenye hizo Ziara zake Mkoani TANGA; Anatoa Mabati, Sukari, Mchelle, Anapata Wanachama Wapya

  Wanavaa throws za CUF sijui CUF wamezinunua kwa kiasi GANI... Huyu Mama naona Anagombea Jimbo Moja huko TANGA...

  Na Inaonyesha Anapendwa kweli kila sehemu ana watu...

  Swali; Anavyofanya hizo ZIARA KAMA MBUNGE WA VITI MAALUMU; anaruhusiwa kufanya hizo campaign? Sasa kuna utofauti gani na za CHADEMA?

  Kwasababu pia MWINGULU NCHEMBA pia anafanya Mikutano huko NZEGA; Nachanganyikiwa sielewi ni WAPI hao CHADEMA wanakosea???
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Au ndio kujipromote ili kati ya CDM na CCM wamwone.Kipindi cha usajili kimeanza na timu nyingine hazilipi sana.
   
Loading...