Salma Kikwete: Bajeti hii itaboresha maisha

Wonders will never end!!!Does she know anything about economics? I thought her area of proficiency was family affairs and music!
Indeed wonders will never end! Somebody tell me who is mama Kikwete in JK's administration... She sounds like a minister or PS
 
MAMA SALMA KIKWETE ANASTAHILI PONGEZI.

1.Amejipambanua kwa matendo kumtetea mtoto wa kike hasa yule wa kijijini.Tunafahamu vijana wa kike wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na mfumo dume ambao umewapelekea kubeba mimba wakiwa shuleni na kutelekezwa.

2.Amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya watu.Ni mama wa kipekee asiye na majivuno kama wake wa marais wengine.

3.Si mropokaji wa hovyo kama tunavyoona baadhi ya wanasiasa.Tumeona kwa wenye macho na tumesikia kwa wenye masikio mambo aliyofanya kupitia taasisi anayoiongoza ya WAMA.

4.J.K Nyerere alikuwa mwalimu kitaaluma na aliachana na ualimu wake ili kuwatetea wanyonge wa nchi hii.Vivyohivyo kwa mama salma kikwete ameachana na ualimu wa darasani na kujikita vizuri katika ualimu wa nje ya darasa kwa kuelimisha watoto wa kike kujiepusha na vishawishi n.k.

TUACHE CHUKI BINAFSI HAZIFAI.UNAWEZA KUPINGA LAKINI SI KUKARIRI KUPINGA KUWA KILA KITU KINACHOFANYWA NA SERIKALI AU SALMA HAKIFAI AU NI KIBAYA.WALIMWENGU NDIO WABAYA SIKU ZOTE MAMA SALMA ALUTA CONTINUA !!!
Upuuzi mtupu,

Yule mmama hana lolote labda mahaba kwa Mh. RAIS. Hana Jipya, labda kucheza taarab, kusoma udaku na umbea! Wanaomu-admire ni wale wahudumu wake, vilaza, wenye fikra rojo n.k.
 
kutenga 30% kwenda kulipa madeni yao nje ndo anasema bajeti nzuri? alikuwa wapi miaka mingine ya maumivu?
halafu anasema na yeye alipangiwa kijijini hivyo walimu waende tu, anafikiri wote watakuwa mafisadilady?
n way baba rizi1 cku hizi matawi hatafuti walimu tena, ndo mana yeye na mapipa
 
MAMA SALMA KIKWETE ANASTAHILI PONGEZI.

1.Amejipambanua kwa matendo kumtetea mtoto wa kike hasa yule wa kijijini.Tunafahamu vijana wa kike wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na mfumo dume ambao umewapelekea kubeba mimba wakiwa shuleni na kutelekezwa.

2.Amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya watu.Ni mama wa kipekee asiye na majivuno kama wake wa marais wengine.
3.Si mropokaji wa hovyo kama tunavyoona baadhi ya wanasiasa.Tumeona kwa wenye macho na tumesikia kwa wenye masikio mambo aliyofanya kupitia taasisi anayoiongoza ya WAMA.

4.J.K Nyerere alikuwa mwalimu kitaaluma na aliachana na ualimu wake ili kuwatetea wanyonge wa nchi hii.Vivyohivyo kwa mama salma kikwete ameachana na ualimu wa darasani na kujikita vizuri katika ualimu wa nje ya darasa kwa kuelimisha watoto wa kike kujiepusha na vishawishi n.k.

TUACHE CHUKI BINAFSI HAZIFAI.UNAWEZA KUPINGA LAKINI SI KUKARIRI KUPINGA KUWA KILA KITU KINACHOFANYWA NA SERIKALI AU SALMA HAKIFAI AU NI KIBAYA.WALIMWENGU NDIO WABAYA SIKU ZOTE MAMA SALMA ALUTA CONTINUA !!!
Kujibu hoja zako ndugu,

1. Amejipambanua kuwatetea watoto wa kike hasa wa kijinini, kijiji gani yeye mwenyewe alikuwa anafundisha kinondoni primary school huyo mtoto wa kike alimkomboa lini ? kuhusu watoto kupata mimba mama kikwete alifanya nini kupunguza mimba mashuleni kwa maana kwa mujibu wa takwimu za wizara ya elimu zinaongezeka na mumewe mwenyewe alishawahi kuwakashifu kwa kuwaambia kuwa wanapata mimba kwa sababu ya kiherehere chao utafikiri yeye hajawahi kufanya makosa maisha yake yote.

2. Amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya watu, watu gani ungekuwa unatoa mfano angalau mmoja wa maendeleo hayo aliyoyafanya na kuhusu swala la majivuno labda hukuwahi kufatilia uchaguzi mwaka jana hakuna mama mwenye majivuno kama huyu kwa kukataa kupanda usafiri wa kawaida wa ndege kwenda mwanza kwenye kampeni badala yake kukodishiwa ndege binafsi kwa dola 15,000. mpaka mwanza wakati mkoani kwake Lindi ndio kunaongoza kwa watoto wenye malazi ya kwashakoo ameshasahau alikotoka dola 15,000 zingeweza kuwasaidia watoto
wangapi kama zingeingizwa kwenye mradi wa chakula na lishe huko Lindi ??

3. Tumeona kwa macho yetu na kusikia kwa masikio yetu mamboaliyoyafanya na WAMA once again mambo gani toa mifano ndugu. Kwa taarifa yako WAMA ni mradi wa wakubwa na ndio maana unaendeshewa ikulu na wamekuwa wagumu kutoa vitabu vyao vya hesabu hadharani kwani huo ni mradi wao kumbuka yaliyotokea wakati wa mama mkapa uwizi alioufanya kupitia taasisi kama hii ya fursa sawa. Kama kweli ana nia ya kuwasaidia watu be ready to open up the books tuone ndani kuna nini??

4. Hilo la mwisho la kumfananisha mwl. nyerere na mama kikwete sina haja ya kulijibu maana linajieleza wazi jinsi usivyo makini. Kuhusu kuwakomboa watu amefanya ninii kuwakomboa watu?? Chini ya utawala wa mumewe asimilia 33 ya budget inaliwa na mafisadi na haya siyo maneno yetu ni maneno ya JK mwenyewe lini mama JK alishwahi kusimama kukemea hali hiyo. swala la kuelimisha watoto wa kike siyo swala lake hilo linawahusu watoto hao na wazazi wao. yeye aende akamuelimishe Ridhwani tabia yake mbaya ya kuita press conference na kuwatukana watu wazima waomzidi umri mpaka baba yake mzazi kabla ya kutaka kuwaelimisha watoto wa wengine.
 
toka lini kiazi kikalijua andazi? hiyo bajeti kweli forged, hadi huyu anaicampaignia?
 
MKE wa Rais, Salma Kikwete, amesifu bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha na kusema kwamba imeonesha dhamira ya dhati ya Rais Jakaya Kikwete, kuwaletea Watanzania maisha bora kwa kuboresha sekta ya elimu.

Katika hatua nyingine, Mama Kikwete amewataka walimu wanaopangiwa kwenda kufundisha katika shule za msingi zilizopo vijijini, kuitikia hatua hiyo ili kuiwezesha serikali kufanikiwa katika uboreshaji wa elimu inayotolewa kwenye shule za sekondari za kata.

Ameeleza msimamo wake pia kuhusu mtazamo wa wadau kutaka watoto wa kike kuruhusiwa kurudi shuleni na kuendelea na masomo baada ya kupewa mimba na kujifungua kwa kusema kuwa kwa maoni yake binafsi na si kama mke wa Rais, mtazamo huo si wa kukurupukia.

Ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akiwahutubia wadau wa kongamano la kujadili mikakati ya kuwawezesha na kuwaendeleza kielimu watoto wa kike wanaotoka katika mazingira hatarishi na yatima waliopo shuleni, lililoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Camfed Tanzania.

Akizungumzia uboreshaji wa sekta ya elimu, Mama Kikwete alisema serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha sekta ya elimu na kumkomboa mtoto wa kike ili kumjengea maisha bora ya hapo baadaye.Alisema bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni kielelezo cha jitihada hizo.

“Shule za Sekondari za Kata ni moja ya vielelezo vinavyodhihirisha azma hii ya Rais Kikwete, pamoja na kuwepo kwa changamoto zinazozikabili. Kabla ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani, watoto walikuwa wanafaulu lakini wanakosa nafasi za kuendelea na masomo kwa ukosefu wa shule, lakini sasa wote wanakwenda shule.”

Amesema, kielezo kingine ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alichosema ni gumzo sasa kwa mataifa mbalimbali Duniani kutokana na kuwa na vyuo sita ndani yake kikiwemo Chuo cha Elimu ambacho kina uwezo wa kuwachukua wanafunzi 15,000 kwa pamoja wanaosomea kozi ya Ualimu.

Kuhusu walimu wanaopangiwa kufundisha shule za vijijini lakini wanakaidi agizo hilo, Mama Kikwete amelaani vikali hatua hiyo na kusema inarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu na hasa katika sekondari za kata.

“Mimi pia nilianzia ualimu vijijini wakati huo nilikuwa sijaolewa nikiitwa Salma Rashid. Nakumbuka mara ya kwanza nilipangiwa kufundisha Shule ya Msingi Chiponji iliyopo katika Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi na nakumbuka kufika kijijini hapo wakati ule hakukuwa na usafiri wa basi na ilibidi nipande trekta. Ni vizuri walimu wakawa wazalendo kwa kukubali kufundisha vijijini,” amesema.

Akizungumzia mtazamo wa wadau wa elimu kutaka wanafunzi wa kike wanaopewa mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua, Mama Kikwete pamoja na kusema kuwa suala hilo linatazamwa kisheria hivi sasa, lakini alitoa msimamo wake binafsi.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Camfed Tanzania, Msaada Balula, amesema shirika hilo limepata mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya mtoto wa kike nchini kwa kuwajengea uwezo kielimu, kimaarifa na kiuchumi.
Ni kweli Bageti Hii Itaboresha Maisha ya RZ1 na The family, Huyu mama hiyo analysis kaitoa wapi!!! Hata Hasomi KILAZA HUYO
 
HUYO MAMA Yuko kisiasa zaidi

Maswala ya uchumi kayajulia wapi?
 
Back
Top Bottom