Salma Kikwete: Bajeti hii itaboresha maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salma Kikwete: Bajeti hii itaboresha maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 11, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 991
  Trophy Points: 280
  MKE wa Rais, Salma Kikwete, amesifu bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha na kusema kwamba imeonesha dhamira ya dhati ya Rais Jakaya Kikwete, kuwaletea Watanzania maisha bora kwa kuboresha sekta ya elimu.

  Katika hatua nyingine, Mama Kikwete amewataka walimu wanaopangiwa kwenda kufundisha katika shule za msingi zilizopo vijijini, kuitikia hatua hiyo ili kuiwezesha serikali kufanikiwa katika uboreshaji wa elimu inayotolewa kwenye shule za sekondari za kata.

  Ameeleza msimamo wake pia kuhusu mtazamo wa wadau kutaka watoto wa kike kuruhusiwa kurudi shuleni na kuendelea na masomo baada ya kupewa mimba na kujifungua kwa kusema kuwa kwa maoni yake binafsi na si kama mke wa Rais, mtazamo huo si wa kukurupukia.

  Ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akiwahutubia wadau wa kongamano la kujadili mikakati ya kuwawezesha na kuwaendeleza kielimu watoto wa kike wanaotoka katika mazingira hatarishi na yatima waliopo shuleni, lililoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Camfed Tanzania.

  Akizungumzia uboreshaji wa sekta ya elimu, Mama Kikwete alisema serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha sekta ya elimu na kumkomboa mtoto wa kike ili kumjengea maisha bora ya hapo baadaye.Alisema bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni kielelezo cha jitihada hizo.

  "Shule za Sekondari za Kata ni moja ya vielelezo vinavyodhihirisha azma hii ya Rais Kikwete, pamoja na kuwepo kwa changamoto zinazozikabili. Kabla ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani, watoto walikuwa wanafaulu lakini wanakosa nafasi za kuendelea na masomo kwa ukosefu wa shule, lakini sasa wote wanakwenda shule."

  Amesema, kielezo kingine ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alichosema ni gumzo sasa kwa mataifa mbalimbali Duniani kutokana na kuwa na vyuo sita ndani yake kikiwemo Chuo cha Elimu ambacho kina uwezo wa kuwachukua wanafunzi 15,000 kwa pamoja wanaosomea kozi ya Ualimu.

  Kuhusu walimu wanaopangiwa kufundisha shule za vijijini lakini wanakaidi agizo hilo, Mama Kikwete amelaani vikali hatua hiyo na kusema inarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu na hasa katika sekondari za kata.

  "Mimi pia nilianzia ualimu vijijini wakati huo nilikuwa sijaolewa nikiitwa Salma Rashid. Nakumbuka mara ya kwanza nilipangiwa kufundisha Shule ya Msingi Chiponji iliyopo katika Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi na nakumbuka kufika kijijini hapo wakati ule hakukuwa na usafiri wa basi na ilibidi nipande trekta. Ni vizuri walimu wakawa wazalendo kwa kukubali kufundisha vijijini," amesema.

  Akizungumzia mtazamo wa wadau wa elimu kutaka wanafunzi wa kike wanaopewa mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua, Mama Kikwete pamoja na kusema kuwa suala hilo linatazamwa kisheria hivi sasa, lakini alitoa msimamo wake binafsi.

  Awali Kaimu Mkurugenzi wa Camfed Tanzania, Msaada Balula, amesema shirika hilo limepata mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya mtoto wa kike nchini kwa kuwajengea uwezo kielimu, kimaarifa na kiuchumi.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Huyu mwanamke ni taipu ya....kabisa. ningekuwa mumewe ningemwambia asijiweke kwenye spotlight, ila nadhani wamekutana wa aina moja
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,132
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Uuugh!!
   
 4. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kichefuchefu kingine ooogh!
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  yaani siku hizi ukimwona runingani anajifanya anajua kuongeeea. nadhani alipelekwa kozi ya kuongea. ila kila nikimsikiliza naona aibu kuendelea kumtazama
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  nina uhakika hajasoma hata mistari miwili ya bajeti.pengine hata kuona tu kwa macho bajeti yenyewe.ila atakuwa amesikia sikia!!!
   
 7. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  mpe pole sana uyu mama kwanza ajitambui ataitabuaje nchi. ndenge warangi 1 uruka pamoja,mke mume wote sawa mungu ni mwema
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Bajeti itaboresha maisha? kivipi? au itaboresha matatizo kama ambavyo imekuwa kwa miaka 5 iliyopita?

  Sijui kwa nini huyu mama anaongelea siasa? Mama Anna Mkapa pamoja na mapungufu yake nampenda kwa kitu kimoja - hakujiingiza kwenye front line politics. hatukusikia hata siku moja Mama Ana akidai taarifa na utekezaji za mikoa! au anakodishiwa ndege kwenda kumfanyia campaign mumewe. Sijui wanafikiri nini huko magogoni lakini binafsi naona kuongea kwa huyu mama anaharibu zaidi kuliko kujenga.
   
 9. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Aisee huyu mama ana kiherehere kama wanafunzi wanaopata ujauzito mashuleni au wale wanaoathirika na hiv kama mume wake alivyosema!!
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ukimwona mwanaume aliyeoa anashindwa kufanya maamuzi mazito basi gundua kuwa nyuma yake kuna mwanamke kilaza zaidi (Lyangalo, 2011)
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Angetafuta mahojiano na vyombo vya habari ili aeleze huo uzuri wa bajeti sio kwenye majukwaa kuhutubia watu..
   
 12. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,972
  Likes Received: 20,334
  Trophy Points: 280
  Huyu first lady anapaswa aige tabia ya mama BWM hasa linapokuja kwenye suala la urais, anavyojiweka sasa ni kama urais ni wa familia, kila kitu wao na wanae, mbona hatukuyaona haya katika awamu tatu zilizopita. Anavyoongea na anavyosoma huwa nakuwa na mashaka kama ni mwalimu aliyehitimu
   
 13. s

  siraji Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAMA SALMA KIKWETE ANASTAHILI PONGEZI.

  1.Amejipambanua kwa matendo kumtetea mtoto wa kike hasa yule wa kijijini.Tunafahamu vijana wa kike wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na mfumo dume ambao umewapelekea kubeba mimba wakiwa shuleni na kutelekezwa.

  2.Amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya watu.Ni mama wa kipekee asiye na majivuno kama wake wa marais wengine.

  3.Si mropokaji wa hovyo kama tunavyoona baadhi ya wanasiasa.Tumeona kwa wenye macho na tumesikia kwa wenye masikio mambo aliyofanya kupitia taasisi anayoiongoza ya WAMA.

  4.J.K Nyerere alikuwa mwalimu kitaaluma na aliachana na ualimu wake ili kuwatetea wanyonge wa nchi hii.Vivyohivyo kwa mama salma kikwete ameachana na ualimu wa darasani na kujikita vizuri katika ualimu wa nje ya darasa kwa kuelimisha watoto wa kike kujiepusha na vishawishi n.k.

  TUACHE CHUKI BINAFSI HAZIFAI.UNAWEZA KUPINGA LAKINI SI KUKARIRI KUPINGA KUWA KILA KITU KINACHOFANYWA NA SERIKALI AU SALMA HAKIFAI AU NI KIBAYA.WALIMWENGU NDIO WABAYA SIKU ZOTE MAMA SALMA ALUTA CONTINUA !!!
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wonders will never end!!!

  Does she know anything about economics? I thought her area of proficiency was family affairs and music!
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,593
  Likes Received: 4,703
  Trophy Points: 280
  Sindimba
   
 16. M

  Mkali wa Leo Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ukichunguza kwa makini, wote waliosema huyu mama Salma ni kichefuchefu ni wanawake ambao km kawaida yao wana wivu. Jamani wanawake ndo mana hatuendelei, chuki si mtaji.

  Mimi binafsi siyo CCM na wala sipo CDM lakini huyu mama mchango wake kwenye jamii ni mkubwa mno na hasa kwa vijana wetu wa kike. HEBU ACHENI MAJUNGU BASI. Mazuri myasifu looool, wanawake wengine bora mngezaliwa Libya maana mngekuwa mmeshakufa kwenye vita pamoja na hiyo mijidume yenye tabia ya wivu na chuki kama wanawake.
   
 17. J

  JMafux Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anafurahisha umati, yaani kuwategemea wafadhili ndiyo bajeti nzuri?
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kusema tu, mbona ni rahisi? Angesupport kwa data ningemsifu!
   
 19. L

  Lua JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  itaboresha maisha ya akina nani? kama ya chama cha magamba ni sawa.
   
 20. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mediocre Tanzania first ladies:Anna,Sitti na Salma.

  Money mongerers!
   
Loading...