Salim Himidi katika picha, katika mazungumzo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
SALIM HIMIDI KATIKA PICHA KATIKA MAZUNGUMZO

Mtu anapoondokewa na wake akili inahangaika sana lakini mara mtu anasahau na maisha yanaendelea.

Hizi ni katika rehma za Allah vinginevyo maisha yetu yote duniani yangetawaliwa na huzuni kwa misiba inayotufika.

Picha ya mwanzo kushoto ni Salim Himidi, Ahmed Rajab na Simba Waziri, London Trafalgar Square mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Hao wote ni kaka zangu watu wangu wa karibu sana.

Bado kijana mdogo mgeni London Ahmed Rajab kanichukua Trafalgar Square kunionyesha kituo cha treni kwa safari zangu nikija mjini nikitokea Finsbury Park.

Simba Waziri mimi nakua Dar es Salaam namuona.

Salim Himidi nimemjua Tanga kupitia rafiki yake Mohamed Mshangama na fikra zetu zikawa sawa ikawa kila akija Tanzania tunakuwa sote kwa muda mrefu kwa mazungumzo yasiyokwisha.

Niko Berlin Zentrum Moderner Orient kwa mwezi mzima kwa shughuli za utafiti na kuandika.

Ratiba niliyopangiwa ni kwenda ofisini Jumatatu na Alkhamis kwa shuguli za kazi.
Siku tano nikae nyumbani.

Kwangu huu ukawa ni muhali nikawaomba wenyeji wangu kuwa niende kazini siku zote ila Jumamosi na Jumapili.

Hii ilinisaidia kwa kuwa kazi niliyopewa nikawa nimeikamilisha mapema sana.
Sasa nafanya nini?

Berlin ni katika miji migumu niliyopata kufiika duniani.
Wajerumani saa 24 nyuso kama wamekunywa shubiri,

Stoneface,
Hakuchekei.

Charles Dickens amesema, ''If you are tired of London you are tired of life.''
Berlin naomba siku zishe nrejee Tanga.

Katika hali kama hii ikanijia fikra.

Kwa nini nisiende Paris kumtembelea Salim Himidi kisha The Hague nikamuone kaka yangu Prof. Mgone kisha Geneva nitokane na upweke wa Berlin?

Nikajitoma kwenye treni jioni na asubuhi siku ya pili niko Paris na rafiki kaka yangu Salim nimemkuta stesheni ananisubiri.

Ilikuwa asubuhi ananifuata hoteli tunatoka.

Nilikuwa sinywi chai hotelini namsubiri Salim tunakwenda hoteli moja ya Muhindi tunapata chai kwa sambusa na kababu utadhani tuko Tanga au Dar es Salaam.
Njiani mimi nakuwa nimeingia darasani na mwalimu wangu ni Salim Himidi.

Inategemea nimemchokoza kwa lipi.
Ikiwa Russian Revolution ataanza na ''Stanilists.''

Na ''lecture,''itakwenda tunakata mitaa, tupo hoteli ya Muhindi wetu wa Paris, tunakunywa chai au tuko ndani ya treni tunakwenda mbali kidogo.
Picha hiyo Salim kavaa kanzu ya rangi ya udongo nimempiga hapo hoteli kwenye chai.

Tulikuwa na meza yetu maalum tukikaa pale tunaona nje vyema kabisa.
Rafiki yake mmoja kaniletea kidogo kuhusu Salim na ubingwa wake wa lugha.

Ameniandikia:

''Salim Kipaji kimoja alichokuwa nacho Salim ni ufasaha wa Kiingereza alicholelewa nacho kutokana na elimu yake Zanzibar na Kifaransa ambapo aliwapiku wengi Ufaransa alikosoma baadae.

Wakati wa mkutano wa Nchi za Afrika na Ufaransa Francophonie 1977 ambapo alimuwakilisha Ali Soilihi, Salim alimkosha Rais Leopold Sedar Senghor jinsi alivyokuwa akizungumza Kifaransa safi. Senghor baadae alitaka kumjua vyema Salim akamuuliza juu ya maisha yake na Salim akamwambia alisoma Zanzibar na Kifaransa alisoma Ufaransa.

Senghor aliyekuwa mwana falsafa maarufu na bingwa wa Kifaransa, wakati wote baada ya mkutano akiuliza ''Ou est mon fils,Salim?'' Yuko wapi mwanangu Salim?''

Sasa mimi nimebahatika kumsikia Salim tukiwa katika mazungumzo nasikiliza lecture zake.

Mwisho wa lecture mwanafunzi nitamuuliza mwalimu wangu lini atayaandika hayo na jibu lilikuwa halibadiliki ni lile lile alilonipa Tanga, Dar es Salaam na Paris, ''Sheikh Mohamed Insha Allah nitaandika.''

Hivi niandikapo ni kama vile namuona na namsikia.

Kama vile namuona na naisikia sauti yake ananisomesha.
wenye treni jioni na asubuhi siku ya pili niko Paris na rafiki kaka yangu Salim nimemkuta stesheni ananisubiri.

1615370884403.png

1615370431627.png
 
Attachments

  • 1615370277947.png
    1615370277947.png
    60.1 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom