Salim Chipata wa South Beach Afariki ghafla!

Salim Chipata wa South Beach Afariki ghafla!

Chanazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2010
Posts
212
Reaction score
72
Yule mmiliki wa hotel ya South Beach ya kigamboni.. Aliye tuhumiwa kumuua raia kwa moto nae ameuonja umauti leo..

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Funguka mkuu, sisi wengine hatukuwahi kuijuwa hiyo stori, eenhe... alituhumiwa kumuuwa mtu kwa kumchoma moto???, ilikuwaje sasa mpaka kufikia kufanya unyama huo?? ...na vp hakuwahi kuchukuliwa hatua yoyote?
 
Na wewe si ukamgooggle basi, kha.
Maswali mengi mno.

Funguka mkuu, sisi wengine hatukuwahi kuijuwa hiyo stori, eenhe... alituhumiwa kumuuwa mtu kwa kumchoma moto???, ilikuwaje sasa mpaka kufikia kufanya unyama huo?? ...na vp hakuwahi kuchukuliwa hatua yoyote?
 
Funguka mkuu, sisi wengine hatukuwahi kuijuwa hiyo stori, eenhe... alituhumiwa kumuuwa mtu kwa kumchoma moto???, ilikuwaje sasa mpaka kufikia kufanya unyama huo?? ...na vp hakuwahi kuchukuliwa hatua yoyote?
Nyanidume ... King'asti

Yule mwananchi aliyechomwa moto kwa kosa la kuzamia Disco amefariki dunia. Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu Lillah alifariki dunia juzi jioni na amezikwa jana jioni katika makaburi ya mji mwema kigamboni.

Marehemu Lilah ambaye alikuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwa waendao Beach za Kigamboni, alikumbwa na mauti baada ya kukutwa ndani ya Disco akiwa hana tiketi maalumu inayovaliwa mkononi kwa wale wote wanaoingia ndani ya ukumbi huo wa South Beach.

Spoti na Starehe ni mmoja wa marafiki wa marehemu kwani alikuwa akitembelea na kuuza bidhaa zake katika fukwe Mbalimbali za Kigamboni ikiwemo Chadibwa Beach. Marehemu Lillah alikamatwa na walinzi wa fukwe ya South Beach Jumapili iliyopita kwa kudaiwa kuingia bila kulipa kiingilio kwenye Disco linalopigwa mwishoni kwa kila wiki fukweni hapo, Lillah hatimaye alipelekwa kwa meneja wa hoteli hiyo ambaye aliamrisha achomwe moto.

Akionge kwa taabu na Muandishi wetu katika Hospitali ya Kigamboni kabla ya kuhamishiwa Muhimbili alikoagia dunia, Marehemu Lillah alisema hata Kupona mpaka pale anamshukuru Mungu kwani hakutegemea kupona kutokana na kipigo na maumivu ya moto ule. Tunaomba haki itendeke ili kukomesha unyama huu, hata kama Marehemu Lilah alikuwa mkosaji au kibaka kama walivyodai hapaswi mtu yeyote kutoa hukumu ambayo Lillah amepata.

Huu ni mfululizo wa kujichukulia sheria mikononi ambapo wezi na vibaka wamekuwa wakichomwa moto na wakati mwingine bila hatia yeyote, kwani matukio mengine yakitokea akishakamatwa anatafutwa aliyeibiwa haonekani. Mwanzoni mwa mwaka kijana mmoja alipoteza maisha maeneno ya Mwenge kwa kuitwa mwizi ilihali yeye ndio alikuwa ameibiwa Laptop yake na alipojaribu kuwakimbiza wezi walimgeuzia kibao na hatimaye wananchi walimvamia na akapoteza maisha. Marehemu Lillah ameacha mke na watoto.

​

More:

1. http://uniqueentertz.blogspot.com/2011/04/muuaji-wa-south-beach-akamatwa-uwanja.html
2. http://lukemusicfactory.blogspot.com/2011/04/achomwa-moto-kwa-kuzamia-south-beach.html
3. http://zamaradimketema.blogspot.com/2011/04/yule-mwananchi-aliyechomwa-moto-kwa.html
4. https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/184458-waliomuua-kijana-south-beach-resort-kigamboni-wafutiwa-mashitaka-2.html
.
 
Last edited by a moderator:
Good to hear that the killer also died. Hawa waraabu wakija Tanzania hujisahau sana!
 
Pia kuna mtoto aliuawa pale southbeach...ktk mazingira yasiyoeleweka ni km alinyongwa...wakt wanamtafuta hakuoneka..akaja kuonekana asubuhi pembeni ya swimming pool...km si mpango n nini
 
japo hujaweka taarifa kamili mkuu tujikumbushe tena na tena,
kila nafsi itaonja mauti
ikiwa ni pamoja na mimi na wewe mkuu!
 
Huyo alikaidi amri hivyo kupigwa na kuchomwa moto ilikuwa halali yake according to Pinda!

Tiba
 
Pia kuna mtoto aliuawa pale southbeach...ktk mazingira yasiyoeleweka ni km alinyongwa...wakt wanamtafuta hakuoneka..akaja kuonekana asubuhi pembeni ya swimming pool...km si mpango n nini

Bila kusahau yule mfanyakazi aliyepigwa risasi na mwenzake walipokuwa huko south beach.
 
funguka mkuu kuhusu mazingira ya kifo!
Nakumbuka huu utesaji wa pale south beach ulizua tafrani sana.
 
Huyo alikaidi amri hivyo kupigwa na kuchomwa moto ilikuwa halali yake according to Pinda!

Tiba
Hapa unataka kusema mweshimiwa pinda katika kauli yake alirejea hukumu iliyowahi kutolewa na salim chipata. hapo viongozi hawa majanga!
 
Hapa unataka kusema mweshimiwa pinda katika kauli yake alirejea hukumu iliyowahi kutolewa na salim chipata. hapo viongozi hawa majanga!

Mkuu Ego,

Tuko pamoja kabisa!!!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom