Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
SALAAM ZA PONGEZI KWA WABUNGE WATEULE WA EALA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kutoa salaam za pongezi kwa wabunge wateule wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka kundi C, kutokana na nafasi mbili za CHADEMA, waliopatikana leo baada ya uchaguzi uliofanywa na Bunge la Tanzania; Josephine Lamoyan na Pamela Maassay.
Chama kina imani kubwa kuwa wabunge hao wateule wa EALA watakuwa wawakilishi bora wa nchi yetu kwenye bunge hilo wakizingatia manufaa, maslahi na matakwa ya Watanzania na wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Kupitia uwezo, uzoefu na utayari walionao wa kujifunza na kupokea maarifa mapya; Lemoyan na Maassay watabeba matumaini ya MABADILIKO ya Watanzania, ambao wangependa kuona ushirikiano wa EAC unakuwa na nguvu za kiuchumi na kisiasa uliojengwa katika misingi ya kidemokrasia kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi.
Hivyo, chama kinawaahidi ushirikiano wakati wowote watakapohitaji ili waweze kutimiza wajibu na majukumu hayo kwenye uwakilishi wa EALA na EAC kwa ujumla kwa niaba ya nchi yetu.
Imetolewa Jumatano, Mei 10, 2017 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA